ROKY
Senior Member
- May 4, 2011
- 182
- 70
Habari ya siku mkuu!
Vp mchakato wako wa kilimo unaendeleaje?
Mimi msimu huu sijalima chochote kwa sababu za kifedha.
Nataka nianze msimu wa vuli ( September 2013 - December 2013), kwa sasa najikusanya kwa ajili ya msimu huo.
Kuna wakati uliulizia kuhusu mashamba ya kukodi, vipi bado unahitaji ?
Kama bado unahitaji, naweza kukuunganisha na jamaa wenye mashamba karibu na mto Ruvu.
Kule ardhi ni nzuri sana, na ukilima kwa umwagiliaji, una hakika ya mavuno.