Project kubwa ya kilimo RUVU!

Habari ya siku mkuu!
Vp mchakato wako wa kilimo unaendeleaje?

Mimi msimu huu sijalima chochote kwa sababu za kifedha.
Nataka nianze msimu wa vuli ( September 2013 - December 2013), kwa sasa najikusanya kwa ajili ya msimu huo.
Kuna wakati uliulizia kuhusu mashamba ya kukodi, vipi bado unahitaji ?
Kama bado unahitaji, naweza kukuunganisha na jamaa wenye mashamba karibu na mto Ruvu.
Kule ardhi ni nzuri sana, na ukilima kwa umwagiliaji, una hakika ya mavuno.
 
Ni kweli mkuu bado nahitaji maana uliniambia kwamba muda mzuri ni kuanzia mwezi wa sita mwishoni maana watakua wameshavuna mpunga?

By the way ntakuwekea PM!
 
Hongera kwa ujasiriamili wa kilimo tupeane update
 
Vipi Wizi.. wanyama wahribifu?!
 
Vipi Wizi.. wanyama wahribifu?!

Swala la wizi lipo kwa kiasi kidogo sana kwa sababu mashamba yetu yako mbali sana na makazi ya watu, na pia ni mbali sana na barabara kuu.
Changamoto kubwa ni wanyama waharibifu kama vile nguruwe pori, nyani na ngedere.
Pia kuna changamoto ya wafugaji. Wafugaji ni wasumbusu sana.
Usipolinda shamba wanaingiza mifugo kwa makusudi.
Lakini ukiweka ulinzi, swala la mifugo sio kero kubwa, kero ni wanyama pori.
 
Mkuu nahitaji kulima matikiti hapo ruvu,jee msimu wake ni kuanzia lini?maana mie ningependa kuanza sasa au kabla ya tar 15 mwezi wa sita.
 
Mkuu nahitaji kulima matikiti hapo ruvu,jee msimu wake ni kuanzia lini?maana mie ningependa kuanza sasa au kabla ya tar 15 mwezi wa sita.

Kule tulipo sisi kwenye kijiji cha Kitomondo, wakulima huanza kulima matikiti baada ya kuvuna mpunga mwezi wa July na nuendelea.
Ila kuna mashamba ya kukodi kwa wenyeji wa huko, maana mara nyingi wenyeji hawalimi mashamba yao yote, hivyo unaweza kupata mwezi June.
Changamoto ya mwezi huo June nu uwepo wa maji yaliotuama mashambani kama mvua hizi zitaendelea.
Wakulima wengi hupenda kulima karibu na mto Ruvu ili kuwa na uhalika wa maji ya kumwagilia, hivyo sisitiza kukodo mashamba yaliyo karibu na mto.
Mashamba haya ndio ambayo huwa yanatuamisha maji wakati huu wa mvua.
Nakutumia PM ya namba ya mmoja wa wenyeji wa huko ili uwasiliane naye akupe maelezo zaidi. Utapata shamba la kukodi toka kwa mwanakijiji huyu.
 
Mkuu nahitaji kulima matikiti hapo ruvu,jee msimu wake ni kuanzia lini?maana mie ningependa kuanza sasa au kabla ya tar 15 mwezi wa sita.
Ndugu zangu nawashauri tufikirie zaidi kufanya kilimo ndan ya greenhouses. Pale ruvu mto unatiririsha maji 24/7. Hivyo hatukutakiwa kabisa kuongelea kilimo cha msimu.

Na ukiweza kulima tikiti/nyanya ndani ya greenhouse utaweza vuna tikiti msimu wote na utafetch high price mana utakuwa unavuna muda ambao wakulima wengine wanaofanya open agriculture wanasubiria msimu. Aidha, wanakadiria kuwa heka moja inatoa 10times ya open agriculture. Greenhouse agric is the way forward. Kama vijana wa karne ya 21 hebu tuondokane na kilimo cha kuvizia msimu. Kutengeneza greenhouses sio that expensive relative to its returns.
 

Mkuu heshima yako,natumaini u mzima!naomba ni PM number ya huyo mwenyeji wa huko ambaye anaweza nisaidia kupata mashamba!
 

Mkuu nataka kujaribu green house but sijui how to start?
 
 
Mkuu nataka kujaribu green house but sijui how to start?
Its good thing to do, nimejitahd sana kuifahamu naona wenzetu huku ndicho wanachokifanya, na wanasema ukitaka kuwa tajiri, unatakiwa ucopy strategy za tajiri. Cheki hii clip inaweza ikakupa mwanga wa pakuanzia Low cost greenhouse farming - YouTube .Kwa kilimo cha ruvu, ukiwa na heka 3 za greenhouse utakuwa far better than kulima heka 20 za open agric kwa maana ya costs and benefits involved.
 
Ahsante mkuu!
Najaribu kucheck kama kuna wanaolima tikiti kwenye greenhouses, kwa bahat mbaya sijaona one. So inaweza ikahitaj kuwauliza wataalam wa kilimo kupitia hizo number kwenye hizo clips za Syngenta. Nikiwa karibu ntakutafuta tuone km tunaweza badalishana mawazo mawil matatu eneo hili coz I like sana kilimo na nadhan ni njia nzuri ya kutokea.
 
Hebu tuwasiliane kwa 0652136131 tuongee
 
Mkuu nataka kujaribu green house but sijui how to start?



Kuna mashamba ya Maua Arusha wanaweza kukufundisha au hata kukuazima wataalam wakakutengenezee kwa shamba lako, kuna bingwa mmoja majuzi tu alitengenezewa shambani kwake ajaribu kulima uyoga.

Nitajitahidi kukutafutia mawasiliano yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…