Kuwawezesha kwanza kabisa ndio kuwapa ujuzi badala ya kuwakaririsha wafaulu mitihani ya multiple choice na kuwapa maGPA ya uongo, kama mtu hajapata ujuzi kumkopesha ni kupoteza pesa kwa uhakika kabisa, kijana aliyeiva wala hahitaji kuelekezwa wapi atapata mtaji, yani ana maarifa na anaona resources zote! Huyu wa kuomba elfu 2 mkuu, ukimpa milioni 2 huo mtaji si ataenda kubet? Mikopo ina taratibu zake za kulinda value ya pesa na kuifanya iwe na tija, hamna serikali duniani inatoa tu ila inaweza kuweka pesa mahali (iwe bank au taasisi nyingine) then wenye ujuzi, nia na attitude sahihi wanatangaziwa wakaombe mikopo wenyewe, so kila anayejitambua anakwenda na inakuwa ni mkataba kati yake na hiyo taasisi kwa niaba ya serikali!