Projects kubwa ziwe na wahandisi wa nje!

Projects kubwa ziwe na wahandisi wa nje!

Ndio nitamlaumu Injinia...
Kwa hiyo utamlaumu injinia kwa kuleta mvua kubwa?
Aliyefundishwa kukariri kwamba ajenge daraja linalokaa imara only in dry weather ikinyesha mvua tu tatizo...
Kwanza hatujafundishwa kukariri na wala hatukariri, mpaka hapa naomba tuelewane! Pili, ni wapi nimesema daraja linajengwa ili liwe imara wakati wa dry wether only? Mbona unaleta mada ambazo hazipo?
Mkuu sijui kwa nini unawatetea...
Sijatetea mtu.
Kujenga Becky haitaji Degree ya uhandisi kujua kwamba sio Past History peke yake inayokuwa kama factors za ku determine mradi ujengwe kivipi, bali na Future inakua calculated..duration na future risks za mradi ...kwa mfano Floods
Kwa hii sentensi nadiriki kusema hujaelewa nilichosema. Na hapa wewe ndio umekariri na kujibu bila kuelewa nilicho maanisha.
Sasa kama mnajenga madaraja kutegemea past history,then tuna tatizo kwenye mfumo wa Elimu yetu ya wahandisi,yaani hapa umeonyesha jinsi kulivyo na gap kwenye Elimu yetu 🙄 🙄
Naona kuna kitu uko nacho lakini hutaki kusema!!

Nikupe mfano mwingine,

Katika mto A ndani ya mwezi huu maji yana kina cha mita 4, ila mwaka jana maji yalifikia kina cha mita 6 na mwaka juzi maji yalifikia kina cha mita 7.5, je unadhani uta design daraja kwa kuangalia kina cha mwezi huu ambacho ni kidogo(mita4)? au utatumia kina cha mwaka juzi (mita 7.5) ili kuweka daraja lako katika safe side kwamba hata kama maji yakija mita 7.5 kama mwaka juzi basi daraja lako litahimili?

(Naomba hii pointi uijibu ukiwa huna mihemko, kama una mihemko bora usijibu).
 
Barabara inajengwa chini ya level ya ardhi kila siku inasumbua watu kufagia michanga tena zinajengwa bila kuweka kingo na kusababisha kubomoka kuanzia pembeni ,INA maana nyinyi mainjinia mnashindwa hata kujua kwanini barabara zenu mnazo jenga zimejaa michanga na vumbi na maudongo pumbaavu zenu kabisa mfano utakuta sehemu za MAUA level ya udongo IPO juu kuliko barabara matokeo ni udongo kuingia barabarani tazama barabara ya airport dar yani ni mambo ya ajabu sana nakumbuka vituo vya mabasi vinajengwa bila ya kuzingatia basic things mfano vyoo pale brt palikuwa hakuna vyoo !!!! Kweli nyinyi ni wapumbaavu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi sisi ni wapumbavu kwa sababu tunatumia ujuzi wetu ulio tukuka kutengeneza platfom ambayo WAPUMBAVU KAMA WEWE mnatumia kututukana!

Sisi ni wapumbavu kwa sababu tunatengeneza mifumo ya mawasiliano inayo wawezesha WAPUMBAVU KAMA WEWE kununu kabando ka jero na kututukana!

Sisi ni wapumbavu kwa sababu tunajenga barabara ambazo WAPUMBAVU KAMA WEWE mnapitapita na tu vitz twenu alafu mkofika nyumbani (tena nyumba tulizo tumia elimu yetu zikajengwa) mnakaa kwenye kochi na kuanza kututukana!!

Kwa hiyo nakubaliana na wewe wenda sisi ni wapumbavu maana TUNATUMIA ELIMU ZETU kuwatengenezea mazingira mazuri VILAZA na WAPUMBAVU KAMA WEWE kukaa na kuandika upuuzi!!
 
Kwa hiyo utamlaumu injinia kwa kuleta mvua kubwa?

Kwanza hatujafundishwa kukariri na wala hatukariri, mpaka hapa naomba tuelewane! Pili, ni wapi nimesema daraja linajengwa ili liwe imara wakati wa dry wether only? Mbona unaleta mada ambazo hazipo?

Sijatetea mtu.

Kwa hii sentensi nadiriki kusema hujaelewa nilichosema. Na hapa wewe ndio umekariri na kujibu bila kuelewa nilicho maanisha.

Naona kuna kitu uko nacho lakini hutaki kusema!!

Nikupe mfano mwingine,

Katika mto A ndani ya mwezi huu maji yana kina cha mita 4, ila mwaka jana maji yalifikia kina cha mita 6 na mwaka juzi maji yalifikia kina cha mita 7.5, je unadhani uta design daraja kwa kuangalia kina cha mwezi huu ambacho ni kidogo(mita4)? au utatumia kina cha mwaka juzi (mita 7.5) ili kuweka daraja lako katika safe side kwamba hata kama maji yakija mita 7.5 kama mwaka juzi basi daraja lako litahimili?

(Naomba hii pointi uijibu ukiwa huna mihemko, kama una mihemko bora usijibu).

Hujitambui,...kuandika bila kuwa objective ni shidaaa,.. unabakia kukosoa kila sentensi...pole mkuu kama tumewaacha uchi,majibu yako kwenye hii thread yanafanya more damage than good,yanaakisi kiukweli watu wetu mnakosea sio tu kukosea bali pia mko tayari kudefend makosa yenu...lack of responsibility/accountability..............................tena ningemshauri Rais wetu awe anavalidate license thenu regularily ,wale wote mliojenga madaraja mabovu muwe sifted hakuna kupata future tenda.....nakwambia nchi za ulaya zimejengwa karne hizo..badala ya kunipa majibu tunakosea wapi eti unanipa mfano mwingine...mnhh
 
Kusoma uinjinia na kuitwa injinia (kama wabongo wengi wanavyopenda) ni tofauti kabisa na ufanisi wa kazi. Hapa kwetu tuna wasomi wa kwenye makaratasi waliokariri ili kushinda mitihani na siyo wataalam. Na ni sekta zote, siyo ujenzi tu. Kwenye udaktari, ujenzi, uhasibu, kilimo, sheria.... kote huko mambo ni bora liende. Sikatai kuwa wako wachache wenye weledi wa kazi lakini impact yao inamezwa na wazembe ambao ndiyo wengi. Ukiwa Dar maeneo mengi yenye barabara mpya kuna barabara zimejengwa... du... inasikitisha. Ukiziangalia unajiuliza hizi ni injinia aliyekaa darasani akafuzu amejezijenga au ni watoto wa chekechea. Waswahili husema chema chajiuza na kibaya chajitembeza. Sisi waswahili tumebaki kujitembeza na visingizio viiiiiiingi lakini ukweli ni kuwa hatuna uwezo wa kujisimamia. Tu wavivu, wazembe na wezi.
Tunasoma ili tupate cheti
 
labda basics,ntakua wa mwisho kuamini vitabu vya nje na ndani ni sawa,sababu nje mara nyingi wanaangalia nini kinahitajika katika mazingira yao,baada ya kugundua nini kinahitajika ndio wanaandika syllabus na sio vice versa...so sidhani kama mnatumia vitabu sawa..otherwise mbona madaraja yao hayavunjiki kama mnasoma vitu sawa??...budget sio sababu
Tatizo ni 10 percent yako madaraja yaliyojengwa na watanzania toka El nino hadi Sasa yanadunda Ila hayo mengine ni roho mkononi
 
We jamaa una matatizo si kidogo!! Nchi za Ulaya zipi?! Umeangalia kiwango cha corruption kwa hizo nchi unazoamini hakuna hilo tatizo?!

Narudia... kwa Afrika, and elsewhere, Corruption ni sehemu ya gharama za miradi!! Hakuna mkandarasi anayejitambua anayeweza kuchukua Injinia Kihiyo kama unavyodhani!

Wakandarasi wa barabara including madaraja, majengo makubwa and the like, hawa ni makandarasi wakubwa ambao hawawezi kutumia Engineers wasio na sifa! Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kudiriki kusema eti Tanzania kuna uhaba wa Wahandisi wasio na sifa!

Hata hivyo, Mkandarasi asiye na sifa nae anaweza kupewa mradi ambao upo nje ya uwezo wake in terms of resources. Na ikitokea basi sababu ni ile ile.. CORRUPTION ama kupeana tenda kwa kujuana ambayo na yenyewe ni another form of corruption!!

Wasimamizi wa miradi kutoka serikalini nao wanaweza kutoa green light kwa completed project hata kama ipo substandard! Sio kwamba hawajui mradi upo substandard, kwa sababu na wenyewe wanakuwa wamechukua chao!!

Hapa unayefanya utetezi usio na msingi ni wewe... unatetea jambo lililo wazi kwamba, construction industry imejaa rushwa!!! Na ukishaendekeza corruption kwenye sekta ya ujenzi, kitakachofuata hapo ni projects zisizo na viwango!
Hao mainjinia wazuri wamefanya nini kizuri ndugu yangu wee, kama siyo kudai neno ''injinia'' liwekwe kabla ya majina yao hayajatamkwa? Siku zote chema chajiuza na kibaya chajitembeza... Tuache visingizio visivyo na kichwa wala miguu. Na siyo mainjinia tu nimekumbia bali ni sekta zote. Sasa hivi dunia inapigina na virus wa corona. Sehemu nyingine wataalam wanahangaika na hawalali kufanya research ya kuwaelewa zaidi hawa virus, kupata chanjo na dawa. Sisi huku kwetu kimyaa... Naomba tusijitetee na kuhamisha udhaifu wetu sehemu nyingine. Namna hii hatutajirekebisha.
 
Nimependa uliposema hili sio eneo lako la ujuzi ukimaanisha katika sekta hii wewe ni mjinga (sio tusi).

Kwanza unatakiwa ujue kuna tofauti kati ya mkandarasi (anaye jenga mradi) na injinia/consultant anaye design mradi.

Hata wewe unaweza kuwa mkandarasi as long as una vifaa na mtaji ila kamwe huwezi kuwa injinia kama hujaenda chuo na kusomea hiyo fani.

Miradi mingi wanapewa watu wa nje wajenge simply because wana mtaji na vifaa vya kutosha pia mara nyingi ni matakwa ya mkopo kwamba tunapopewa mkopo basi ni sharti tutumie contractors wa nchi iliyotupa mkopo... (kwa kesi hii usitarajie kampun ya bongo ipewe project hata kama wana uwezo).

Miradi mingi wanao design ni wahandisi wetu wa ndani (na ujue bila design mkandarasi hafanyi kazi) ila utekelezaji wanafanya wakandarasi wa nje kwa sababu nlizotaja hapo juu.

Wazo lako la ku engage watu wa nje na ndani ni zuri na ndicho kinachofanyika maana mkandarasi huwa ana simamiwa na mhandisi wa ndan kuhakikisha anafwata design aliyo pewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu weee mbona unataka kutuchezea mchezo wa karata wa kekundu hapa. Wahandisi ndiyo wawajibikaji wakuu kwenye site. Kuna mifano mingi hapa Bongo ya wahandisi waliopo serikalini kufanya kazi chini ya viwango au kwa uzembe kutotimiza kabisa majukumu yao.
 
Acha kuamini watu wa nje wewe. Unadhani vitabu vya nje na ndani ni tofauti??
Skills ni zile zile. Point hapa ni ufinyu wa budget tuu hamna kingine usidanganyike ndugu
Kwanini tusiwaamini watu wa nje? Tumiaa akili hata ya Division 4,linganisha Ikulu ya Magogoni waliojenga watu wa nje kabla hata Babu yako hajazaliwa,alafu angalia na Ikulu ya chamwino ambayo mmejenga wenyewe, utafikili machinga complex,ili uamini chukua picha hizo za Ikulu ya Magogoni na chamwino, alafu mpe mtoto mwambie achague,kisha uludi hapa jamvini
 
Attachments

  • 2350362_images_4.jpeg
    2350362_images_4.jpeg
    33.6 KB · Views: 1
  • 2350364_images_3.jpeg
    2350364_images_3.jpeg
    31.3 KB · Views: 1
Kwanini tusiwaamini watu wa nje? Tumiaa akili hata ya Division 4,linganisha Ikulu ya Magogoni waliojenga watu wa nje kabla hata Babu yako hajazaliwa,alafu angalia na Ikulu ya chamwino ambayo mmejenga wenyewe, utafikili machinga complex,ili uamini chukua picha hizo za Ikulu ya Magogoni na chamwino, alafu mpe mtoto mwambie achague,kisha uludi hapa jamvini
Nadhani hujui hata tofauti ya mhandisi na architect ni nini!! Nakushauri ukajifunze tofauti ya architect na injinia sio unalia lia tu!!

Ku design mwonekano wa jengo sio kazi ya injinia ni kazi ya architect!
 
Mimi mwenyewe nimeshangaa ikulu ya mkoloni ni nzuri Zaid ya Ile sijui Tanzania tuna feli wapi
Tunapo feli ni kwamba hujui tofauti ya mhandisi na architect, mwonekano wa jengo mbaya lawama unamrushia mhandisi!! Kazi ipo!
 
Jamani mambo mengine tuwe wa kweli bila kumung’unya maneno...
Engineering kwa Bongo ni bado sana huwezi kutafuta sababu yoyote ya msingi kujitetea kwamba sijui nini wala nini kimsingi teknolojia yetu ni ndogo sana pia elimu yetu ni nadharia sio vitendo hii inatokana na umaskini wetu kabla hujaanza kupiga kelele za kijinga kutetea Engineering bongo angalia ada kwanza unayolipa wewe halafu angalia vyuo bora kwa Engineering wanalipa ada kiasi gani hapo utaelewa kwa nini wao ni Engineers wazuri kuliko sisi period..
 
Uko sahihi sisi ni wapumbavu kwa sababu tunatumia ujuzi wetu ulio tukuka kutengeneza platfom ambayo WAPUMBAVU KAMA WEWE mnatumia kututukana!

Sisi ni wapumbavu kwa sababu tunatengeneza mifumo ya mawasiliano inayo wawezesha WAPUMBAVU KAMA WEWE kununu kabando ka jero na kututukana!

Sisi ni wapumbavu kwa sababu tunajenga barabara ambazo WAPUMBAVU KAMA WEWE mnapitapita na tu vitz twenu alafu mkofika nyumbani (tena nyumba tulizo tumia elimu yetu zikajengwa) mnakaa kwenye kochi na kuanza kututukana!!

Kwa hiyo nakubaliana na wewe wenda sisi ni wapumbavu maana TUNATUMIA ELIMU ZETU kuwatengenezea mazingira mazuri VILAZA na WAPUMBAVU KAMA WEWE kukaa na kuandika upuuzi!!
Ngojeni magufuli akushikeni matako ndiyo mtajua kuwa ni wapuuzi umeshindwa hata kujibu hoja unakuja na ngonjera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika masuala ya uhandisi kuna changamoto nyingi ambazo ni kama zifuatazo.
1. Bajeti ndogo sana katika ujenzi wa miradi kwa hiyo miradi inajengwa chini ya kiwango. Au mradi unakuwa na design life ndogo.
2. Rushwa na 10%, pamoja na bajeti ndogo bado hiyohiyo ndogo bado watu wanataka rushwa na mgao na hivyo kuwakandamiza wahandisi zaidi.
3. Kukosekana kwa taarifa za kihandisi katika sehemu husika. Tanzania kuna upungufu wa taarifa ambazo zinatumika kusanifu miradi mfano kina cha maji ndani ya mto kwa kipindi cha miaka 100 au kasi ya maji katika mto kwa miaka 100. Taarifa kama hizo nchini hazipo na hazina usahihi na wengi wanajenga kwa kubahatisha tu.
4. Mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta mvua nyingi kupita kiasi ambazo zinatarajiwa kwa hiyo ikinyesha mvua kama hizo lazima miundombinu lazima iharibike.
5. Formula za kudesign nyingi zimetungwa na wazungu ambazo haziendani na hali halisi ya kiafrika. Mfano mito ya kiafrika ni mito korofi sana kuzidi ya kizungu, mito ya kiafrika mvua ikinyesha mto unaweza kuongezeka kina na pia mto unaweza kupanuka zaidi na hivyo kuvunja daraja kabisa ila katika kusanifu kutumia fomular za kizungu wao wanaanglia kina cha mto pekee ila mpanuko hawaangalii. Pia mito ya kiafrika kutokana na kutotunzwa na shughuli za kibinadamu mito inakuwa na madongo na matope mengi hivyo maji yake yanakuwa na nguvu sana kuliko formular.
6. Wanasiasa wamejigeuza wahandisi kwa hiyo tegemea madudu tu.
7. Uwezo mdogo wa wakandarasi wazawa hasa mitaji na mitambo ya kujengea kwa hiyo inaweza kusababisha ujenzi uwe chini ya kiwango. Hao wakandarasi kutoka nje wanapewa mitaji toka nchi zao na mikopo yenye riba ndogo kama 3% wanapewa mpaka mitambo yenye thamani ya 30B tshs kwahiyo mradi wowote mkubwa wanaweza kujenga.
8. Kusoma kwa kingereza kunafanya watu tukariri kuliko kuelewa. Bora tungesoma kwa kiswahili tu. Hao wachina wanasoma kwa kichina mpaka chuo kikuu ndio wanaojenga madude ya kushangaza ulimwengu. Tusome kwa kiswahili tu.

Sijapinga wazo lako ila kumbuka hata hao wataalam toka nje ya nchi na wenyewe kuna mahali wanakwama tu mfano ni daraja la hapo jangwani hilo daraja limejengwa na Strabag ambao ni wakandarasi toka nje ya nchi lakini bado mafuriko yapo palepale, je usomi wao kwa nini haujasadia? Mimi nadhani ni formula walizotumia ambazo kwao ni sahihi ila kwa mazingira ya jangwani sio sahihi maana pale jangwani ni mdomo wa kupeleka maji baharini na madongo yanajaa pale.

Halafu hao wahandisi wa nje wakija bongo huwa wanakuwa wachoyo kutoa ujuzi wao na uzoefu wao maana wanakuwa na hofu kwamba wanaweza kukosa kazi. Labda watanzania waende kusoma huko nje na uwekwe mfumo wa kuwalazimisha kurudi nchini kufanya kazi maana wabongo ukiwapeleka wanazamia kabisa na wanagoma kurudi.

Nimemaliza.
 
Naunga mkoni hoja zako, ila nukta ya kwanza na ya pili, nazitupia kwa wahandisi wenyewe na sio wanao omba rushwa. Hapa Wahandisi wanafeli kwa kutosimamia misingi ya fani bali maslahi, na ile hali ya kuendelea kupata kazi zaidi lakini mwisho wake kuharibu kazi.

Rushwa iko popote, ila wenzetu wa nje kidogo wametuzidi kwa kusimamia kwao misingi ya fani, wenzetu hawafanyi kazi eti ili wapewe kazi nyingine hapo baadae,wao wabafanya kazi kulingana na kazi inataka nini na wakisema hili wanasimamia hilo hilo, hutaki wanakuachia kazi yako ufanye unavyojua wewe, sisi kibongo bongo tunashindwa kusimamia fani tukiogopa tutanyimwa kazi baadae.

Ila mimi nalia na wana siasa, wanachofanya ni balaa tupu. Tushawahi kuambiwa tukamilishe kazi ya 7km kwa kwa siku tatu au nne, ukiangalia changamoto ya kuchelewesha kazi wanaijua. Acha kabisa.
 
Tanzania tunao Wahandisi kibao tena wanajua kazi. Tatizi kuna ukiritimba mwingi na siasa imetawala fani, haya sisi tumeyashuhudia site.
Kama mpo kama mpo kama mpo mbona amkosoi kazi mbovu zinazofanywa na mainjinia mafisadi wanao ujumu nchi sijawai kusikia mainjinia mkikosoa kazi za mainjinia wenzeni na hiyo ni kithibitisho kuwa nyinyi ni feki wrote mfano mimi siyo injinia ila nashangaa kwanini mnapo jenga barabara mnajenga chini ya level ya dongo na kusababisha kazi za kufagia michanga kila siku tazama tanesco na Ttcl minguzo yao ilivyo fungwa fungwa nyaya ovyo utazani mtoto wa chekechea kafunga wewe pita mjini nguzo moja baada ya nyingine kisha uje hapa na upuuzi wa kusema tunao injinia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom