Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Badala ya kuwekeza kwenye jeshi na teknolojia nyie mnawekeza kwa machawa, Sifa anazopewa Rwanda ni za kweli....Maisha ni kitu cha wazi sana kila mtu anaona.
Rwanda haina chochote cha kweli.

Msumbiji kaenda kulinda makampuni ya Mfaransa na Ufaransa ndiyo imetoa hiyo tenda kwa Rwanda.

Congo anapigana na wanamgambo, Congo haina jeshi.

Vikosi ya Malawi, Afrika ya Kusini na Tanzania vimeenda kule kwa mission ya amani na wala si ya vita. Aliyekuwepo kwenye vita ni Rwanda.

Hata hivyo vikosi vya Sadc vinaingozwa na South Africa ambao nao wanapokea maelekezo kutoka UN na mfano wake ni juzi waliambiwa wasiendelee na mapambano.

Rwanda ni mwepesi hana nguvu ya namna yoyote. Nguvu pekee aliyokuwa nayo ni ya propaganda anayotumia kuwajaza watu hofu na kuwajaza wa-Rwanda ujinga kuwa nchi yao ni kubwa na ina uwezo wa kukabiliana na taifa lolote hapa Afrika. Huu ni ujinga! Na hii ni dunia, ni vizuri ukaifahamu nafasi yako.

Jwtz lipo Mtwara! Limefanya kazi kubwa sana kuleta amani na kuwafukuza magaidi wa Msumbiji.

Pauline wakazi wa Mtwara hali ya usalama awali ilikuwaje na sasa ipoje! Magaidi walikuwa wanataka kumege Mtwara na kisha kuelekea Lindi.

Nyinyi wa mikoa mengine huko isiyokuwa na kambi au hampo mipakani hamjui mambo yanayoendelea huko! Hivyo mnaandika chochote matakachojisikia.

Waulize wakazi wa Mtwara au lipia nauli nenda kajionee mwenyewe!
 
Moja ya kosa linalofanywa na wapinzani ni kufikiri wao wakipewa nchi wataongoza watu tofauti na Watanzania waliopo sasa. Ni muhimu kwenye mambo serious yanayogusa future ya nchi yetu hasa mambo ya ulinzi wa nchi, wote tuwe na sauti moja bila kujali wewe ni upinzani au chama tawala. Jeshi ndiyo chombo pekee cha ulinzi wa mipaka ya nchi yetu. Halistahili kubezwa hata kidogo. Kwa hapa East and Central Africa tuna jeshi Imara na bora sana.

Hakuna future kwa nchi inayoshindwa uwezo wa kuprovide maji kwa wananchi.

Kama nchi ina migao ya maji wakati imezunguukwa na ziwa victoria, Tanganyika, Nyasa, Bahari ya hindi jua hiyo nchi ikipambana na Rwanda ya Kiongozi Smart itachakazwa vibaya sana.

Sisi tunaweza kudeal na mzee Kibao, Soka, Mawazo, Abdu Nondo lakini vitu vya maana hatuwezi.
 
Vita ni pamoja na kuwa na kuwa na viongozi wenye ufahamu . Kama una watu wanaogeuza binoculars kuangalia mazoezi ya Kijeshi halafu ndo mawaziri wenye dhamana ya majeshi, unadhani hao wanaweza kufanya jeshi liwe bora?

Lakini je unataka nimuonee wivu Kagame na jeshi lake zuri?.

Ubora wa jeshi letu hautakuja kwa kuionea wivu Rwanda.
Jeshini wapo wanaulinda Taasisi, wapo wanaolinda rais na wapo wanaolinda nchi na nafikiri umenielewa.

Huyo mama yupo kukamilisha taratibu za kisiasa kulingana na kanuni na mwongozo wa kisheria unavyotaka.

Ila mengineyo wapo ambao wanaoyasimamia.

Hakuna ambaye anayemuonea wivu Kagame. Suala ni usalama wa nchi, kama mambo huyafahamu omba ufahamishwe.
 
Vita ni pamoja na kuwa na kuwa na viongozi wenye ufahamu . Kama una watu wanaogeuza binoculars kuangalia mazoezi ya Kijeshi halafu ndo mawaziri wenye dhamana ya majeshi, unadhani hao wanaweza kufanya jeshi liwe bora?

Lakini je unataka nimuonee wivu Kagame na jeshi lake zuri?.

Ubora wa jeshi letu hautakuja kwa kuionea wivu Rwanda.

Mkuu uliwahi kushika Binacular ya aina yoyote?
Mimi ninayo Moja ambayo matumizi yake inategemea unataka kuangalia wapi na kuna sehemu mbili za adjustments, Moja ya umbali au ukaribu, ya pili ukiigeuza unaweza kubadili lenzi za Binacular kwa kuadjust tuu. Yaani mbele kukawa nyuma nyuma kukawa mbele.

Hakuna anayemuonea Wivu Kagame Wala Warwanda Mkuu.

Wewe upo na Mkeo alafu kutwa Mkeo anamsifu Taikon Master huku akikudharau wewe unayemlinda. Hiyo kwako inamaanisha kitu gani?
 
Jeshi limesaliti wananchi wake wanaopotezwa na halitoi tamko lolote jeshi limesaliti wananchi wake kuendelea kulinda chama tawala kushinda chaguzi hivyo Hilo sio jeshi la nchi ni la chama tawala hizi sio zama za mazuzu kudanganyana
Majukumu muhimu ya Jwtz ni yapi?
 
Duh .. kwahiyo mtu alisema bajeti ya jeshi la Rwanda ni Dola z kimarekani 5.3 milioni analidunisha jeshi la Bongo?
 
Kushinda vita vya kijeshi kunahitaji mchanganyiko wa mambo mengi, na hakuna formula moja rahisi. Hapa kuna baadhi ya mambo muhimu ambayo yanaweza kuchangia ushindi:

## 1. Nguvu ya Kijeshi

  • Wanajeshi: Kuwa na jeshi kubwa lenye askari wengi wenye mafunzo mazuri na vifaa vya kisasa.
  • Vifaa vya Kijeshi: Kumiliki silaha za kisasa, kama vile ndege za kivita, meli za kivita, magari ya kivita, na mifumo ya ulinzi.
  • Teknolojia: Kuwa na teknolojia ya kijeshi ya hali ya juu, kama vile mifumo ya ujasusi, mawasiliano, na silaha za kisasa.

## 2. Mkakati na Uongozi

  • Mkakati: Kuwa na mkakati mzuri wa kijeshi ambao unaeleza jinsi ya kufikia malengo ya vita.
  • Uongozi: Kuwa na viongozi wenye uwezo na uzoefu ambao wanaweza kuongoza jeshi kwa ufanisi.

## 3. Uchumi

  • Rasilimali: Kuwa na rasilimali za kutosha kugharimia vita, kama vile fedha, chakula, mafuta, na vifaa vingine.
  • Uzalishaji: Kuwa na uwezo wa kuzalisha silaha na vifaa vingine vya kijeshi.

## 4. Morali

  • Morali ya Wanajeshi: Wanajeshi kuwa na morali ya juu na imani katika ushindi.
  • Umoja wa Kitaifa: Wananchi kuwa na umoja na kuunga mkono vita.

## 5. Diplomasia

  • Washirika: Kuwa na washirika wa kimataifa ambao wanaweza kusaidia katika vita.
  • Mazungumzo: Kuwa tayari kufanya mazungumzo ya amani ili kumaliza vita.

## 6. Mambo Mengine

  • Hali ya Hewa: Hali ya hewa inaweza kuwa na jukumu katika vita.
  • Jiografia: Jiografia ya eneo la vita inaweza kuwa na jukumu.
  • Bahati: Wakati mwingine, bahati inaweza kuwa na jukumu katika vita.

Ni muhimu kuzingatia kwamba vita ni jambo ngumu na lisilotabirika. Hata kama una mambo yote hapo juu, bado kunaweza kuwa na sababu ambazo zinaweza kusababisha kushindwa.

## Mwisho

Kushinda vita kunahitaji mchanganyiko wa mambo mengi, na hakuna uhakika wa ushindi. Ni muhimu kuzingatia kwamba vita vina madhara makubwa na vinapaswa kuepukwa kwa gharama zote.


Gemini AI
Uwezo wa nchi unapimwa kwa mambo ya msingi.

Nchi ambayo bado inapewa misaada ya matundu ya vyoo na ambayo inapoteza watoto wadogo wenye damu ya kisiasa inayochemka kama akina Soka nakuhakikishia, nchi hiyo ni failure ktk anga zote.

Akili isiyoweza kusolve matatizo ya msingi kama vile maji, matundu ya vyoo, madawati usitegemee inaweza kuwa nzuri kwenye mambo complex kama ya ulinzi ktk geopolitics.
 
A very poor hypothesis, as the matter of fact it's rubbish.
Theories zako ni za kitoto mno, jeshi imara linajengwa kuanzia kwenye recruiting(si hawa wetu wanaoingia kwa vimemo, siku hizi hata TISS mpaka uwe UVCCM) na training.

Utawezaje ku-recruite watu ambao wanamitazamo hasi, mioyo ya hofu, wasio na Nidhamu, na wasio na Imani.
Au unafikiri Jeshini ni Jela la kufundisha watu Nidhamu?
Jeshini wanatakiwa watu ambao tayari Wana Nidhamu.

Kuhusu hayo ya UVCCM kuingizwa huko kwenye jeshi au TISS kimagumashi kama kuna Jambo hilo serikali iliangalie.
Vigezo vifuatwe

Back in the day things were different.
As long as things on the ground zinatuonyesha kuwa jeshi la PK liko vizuri haiwezekani watu
Embu toa hizo Takwimu zinazoonyesha kwa ground Jeshi la Rwanda liko vizuri kushinda Jeshi Letu.


wasiseme, kukwepa kusema yale yanayooneka ni hypocrisy na haiwezi kusaidia kulijenga jeshi letu. Jeshi halijengwi kwa kupigiwa upatu mitandaoni au wanajeshi hawawezi kujengea kwa sababu tu wanasifiwa mitandaoni, wapate mafunzo na wajengwe nidhamu ambayo pia iwaimarishe mental strength ila recruitment iwe ya maana.
Ni kihoja kusema comments za mitandaoni zitaathiri uwezo wa jeshi hata kama lipo vizuri kiuhalisia on the ground.

Unaposema Comments za mitandaoni unamaanisha nini?
 
Soma vizuri uelewe Mkuu.
Naelewa mantiki yako but kiukweli lazima tujipange zaidi hasa tusisifie ubora wetu ardhini. Vita Leo imehamia hewani ndege bila rubani. Tusibweteke hata huko ardhini tuhakikidhe mifumo Bora ya ulinzi.
Nb.
Mfumo wa namna rec ruitment wapatikanavyo utizamwe . Waingie vijana wenye mori kweli kweli. Adui hatumjui vyema.
Lakini nikuulize boss Kuna chochote Cha ajabu kati yetu na wanyarwa?
 
Hakuna future kwa nchi inayoshindwa uwezo wa kuprovide maji kwa wananchi.

Kama nchi ina migao ya maji wakati imezunguukwa na ziwa victoria, Tanganyika, Nyasa, Bahari ya hindi jua hiyo nchi ikipambana na Rwanda ya Kiongozi Smart itachakazwa vibaya sana.

Sisi tunaweza kudeal na mzee Kibao, Soka, Mawazo, Abdu Nondo lakini vitu vya maana hatuwezi.

Mkuu, nchi kushindwa baadhi ya ishu ni mchanganyiko wa Sababu nyingi Sana.

Mojawapo ni watu kutokuwajibika, viongozi na wananchi kutokuwajibika.

Kwa uelewa wako, kuchimba shimo la Choo kwa Watu na kutengeneza Choo kunahitaji msaada WA serikali au mataifa mengine?

Kule Kwetu Makanya, Same na Mkoa wa Kilimanjaro
Ujenzi wa madarasa, matundu ya Choo kwa sehemu kubwa unafanywa na wanakijiji wenyewe au Wanafunzi.

Mfano, shuleni kwetu kulikuwa na utaratibu, mwanafunzi akipata F Moja anapiga matofali 20 siku za wikiendi.

Mimi nilifanya kosa la kwenda shule ya jirani kwenye michezo bila kufuata taratibu. Nikapewa adhabu ya kupiga tofali mia Tatu. Nikafyatua na inatakiwa uyakabidhi yakiwa mazima.

Matofali Yale yalitumika kujenga madarasa, na vyoo.

Ujenzi wa mitaro na barabarani au MiTo ya kumwagilia mashambani Kule kwetu hufanyika kwa misaragambo.
Serikali Kazi yake ni kutoa mchango kidogo tuu

Kufupisha, wananchi wanapaswa wawajibike.

Kule kwetu mwanamke na mwanaume lazima wote wafanye Kazi.

Sio unampa mtu Lawama mtu mwingine kwa Jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako.

Serikali ya Tanzania na nyingi za kiafrika zinafeli kwa sehemu kubwa kwa sababu wananchi wake hawataki kuwajibika na wanazalisha viongozi wasiowajibika.
Wanapenda mambo ya Burebure
 
Naelewa mantiki yako but kiukweli lazima tujipange zaidi hasa tusisifie ubora wetu ardhini. Vita Leo imehamia hewani ndege bila rubani. Tusibweteke hata huko ardhini tuhakikidhe mifumo Bora ya ulinzi.
Nb.
Mfumo wa namna rec ruitment wapatikanavyo utizamwe . Waingie vijana wenye mori kweli kweli. Adui hatumjui vyema.
Lakini nikuulize boss Kuna chochote Cha ajabu kati yetu na wanyarwa?

Sahihi Kabisa.
Kuna Sababu mbalimbali za vijana kuwa na morali.
Hizo propaganda zinafifisha Morali za Watanzania
 
Msichanganye siasa na usalama wa nchi, ukiona watu wamekaa kimya basi jua wamepima na wameona hakuna shida,

vyombo vya ulinzi vikiamua lake hata ujifiche wap na kikundi chako mtadakwa tu.

Siasa zisiwadanganye mkaona nchi ipo ipo tu ki-hasara hasara,

Kuna watu baadhi nawafahamu ambao nyumbani kwenye familia yake anaonekana kwa mwaka mara 1.

Ikitokea umesikia story za hawa jamaa ndio utajua haujui.
 
PROPAGANDA ZA KUKUZA UWEZO WA RWANDA KIJESHI ZINAHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU HAPO BAADAYE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kuna tabia ambayo imekomaa miongoni mwa watu ya kuisifia, kuitukuza, kuipamba, kuipa uwezo hata usiofaa nchi ya Rwanda katika sekta mbalimbali. Na Leo nitajikita kwenye sekta ya Ulinzi na usalama na hapa tunazungumzia Jeshi na Mbinu za kimedani.

Kwa Sisi Watibeli, Jeshi sio kuwa na watu wengi.
Jeshi sio kuwa na vifaa vya kisasa na vya kiteknolojia.
Jeshi sio ukubwa wa Miili au maumbile.
Jeshi sio kuwa na uchumi Mkubwa.

Jeshi ni zaidi ya hayo. Hayo ni Mambo madogo Sana Jeshini na yanatokea Nje ya Mwanajeshi.
Uanajeshi ni lazima uanzie ndani ya mwanajeshi mwenyewe.

Jeshi ni Mtazamo
Jeshi ni Imani
Jeshi ni Nidhamu
Jeshi ni Moyo wa Ujasiri
Hayo yote yapo ndani ya mwanajeshi. Mwanajeshi ili awe Mwanajeshi lazima awe na hayo Kwanza ndipo mafunzo, silaha, Mbinu n.k. ndio apewe.

Kwa namna hiyo Basi, utagundua lengo kubwa la Propaganda ni kuangusha ujasiri, Imani, mtazamo wa Mwanajeshi husika au jeshi husika katika upambanaji.

Kwa Sisi Wasomi wa Bibilia, Moja ya mambo makubwa ambayo yanajitokeza tokeza katika visa vya Biblia ni Propaganda ya kuwapa Waisrael Ujasiri, Imani, na mtazamo Chanya kuwa wao ni Bora kuliko watu wote Duniani.
Kisha ndipo Sheria za Torati zinawekwa ili kuwafanya wawe na Nidhamu.

Zipo Makumi ya aya zinazoeleza kuwa Muisrael Mmoja atakimbiza watu Mia WA mataifa mengine. Hiyo ni propaganda

Kuna kisa kingine ambacho Musa aliagiza Wapelelezi Kumi na mbili Kwenda kuipeleleza Nchi ya Kanaani. Wapelelezi wale Kumi na mbili waliporudisha ripoti. Wapelelezi Kumi wakatoa ripoti Yao kuelezea Jinsi nchi Ile ilivyo na watu wake walivyo Wakubwa na wenye nguvu na hodari. Kwa jinsi walivyokuwa wanaoelezea ni Kwa namna ya kuwakatisha tamaa na kuwatisha waisrael Jambo ambalo ni Kweli Waisrael waliingiwa na Hofu.

Lakini kwa Bahati, wapelelezi Wawili ambao ni Joshua na Kalebu wao wakatoa ripoti Yao inayokinzana na ripoti ya wale wapelelezi kumi. Wao wakasema in a positive ways.
Kusifia nchi wanayoiendea(Lengo Lao), kusifia Jeshi lao na Waisrael kwa ujumla, na mwisho kueleza sifa za maumbile ya adui Zao in a negative ways.
Wakasema, ni kweli wale watu ni Wakubwa Sana, wanamiili Mikubwa Mno na nguvu za Kimwili, lakini mioyoni mwao wanahofu juu yetu. Mambo makubwa tuliyoyafanya kuanzia kwa Farao, bahari ya shamu na kupiga mataifa yote tuliyokutana nayo imewanyong'onyesha Sana.
Hivyo waisrael na Jeshi la Israel Halina Sababu ya kuogopa watu hao kwani ni ukubwa wa Pua tuu ambao haulingani na wingi wa makamasi.

Ari, ujasiri, imani kwa Waisrael na Jeshi lao ikarejea lakini Musa kama kiongozi wa kijeshi na mwenye hiyo Movement akatoa maamuzi wale wapelelezi kumi wauawe ili wasije waletea Hofu na kuambukiza Hofu hiyo watu wengine.

Muhtasari huo tunajifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi linaloendana na Mada hii ni nguvu ya propaganda na maneno katika Ulinzi na usalama na wanajeshi wetu.

Jeshi imara linatokana na wananchi imara.

Hawa watu wanaendesha propaganda za kuishusha nchi yetu na kuidunisha hasa kijeshi(kiulinzi na KIUSALAMA), sio tuu wanatukosea Bali wanahatarisha usalama wa nchi kwa wakati ujao.

Kama ikiendelea hivi itajengeka dhana kwenye jamii yetu kuwa Warwanda ni watu hodari kuliko Sisi. Sisi ni Duni mbele ya Warwanda Jambo ambalo ni Uongo lakini likiendelea litafanya mitazamo ya Watanzania kuligeuza Jambo hilo ni KWELI.

Hawahawa wananchi ndio baadaye watajiunga na Jeshi. Yaani watu wenye kujiona Duni na hofu dhidi ya Warwanda ndio watakuwa wanajeshi hata ikitokea vita watakuwa waoga na kushindwa mbele za adui Zao Warwanda.

Nini chakufanya?

1. Kitengo cha Propaganda hasa za kijeshi kisilale. Kijiimarishe na kuweka mipango na mikakati kufanya Watanzania waliamini Jeshi Lao.
Kwa sababu Jeshi likianza kutiliwa Mashaka hata ufanisi wake utapungua.
Kwa USA na mataifa mengine tunaona wo vitengo vya propaganda viko kila idea, huko Hollywood kwenye Filamu, kwenye Masuala ya kisayansi, na mambo ya Waandishi wa riwaya na tamthilia.
Kwamba ati Mwanajeshi Mmoja wa kimarekani anaweza kushughulikia maadui Mia moja wa mataifa mengine

2. Kutokana na baadhi ya watu kutokuwa na Akili au kuwa na chuki na nchi. Iundwe Sheria za kuzuia watu kuzungumzia mambo ya kijeshi na kiusalama kwa namna ya kudhalilisha, kumshusha heshima ya jeshi, kukejeli, kushusha morali au kudunisha.
Hii itaepusha na kuzuia wale wapiga propaganda zenye maudhui ya kudunisha Jeshi la nchi.

3. Watu wapewe uwezo wa kutoa maoni Yao lakini yawe maoni ya kujenga sio yenye lengo la kutukuza taifa jingine kuliko taifa kwa namna ya kukejeli taifa letu.

4. Mafunzo ya JKT yaendelee kutolewa kwa wanaomaliza kidato cha sita na kwa wale Wa kidato cha nne ambao wataendelea na vyuo vya Kati.

Ninawahakikishia, Maneno haya yakiendelea hivihivi watu na jamii itayaamini. Na matokeo ya kuyaamini Maneno ya aina hii hayatakuwa mazuri.

Lazima Sisi kama taifa tujitambulishe sio tuu kwa upendo wetu, umoja wetu Bali pia tujitambulishe kama watu wenye AKILI kubwa, na watu wenye kufanya mambo magumu.

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Poleni sana...
 
Hivi Rwanda ina ukubwa kama wilaya moja ya korogwe tu au imezidi? Yaani siku Rwanda au M23 wakijichanganya wakavamia bongo jina lao litabadilika
Congo kubwa mara tatu kuliko Rwanda ila inachapwa na Rwanda.

Wingi wa pua si ukubwa wa makamasi.
 
Mkuu, nchi kushindwa baadhi ya ishu ni mchanganyiko wa Sababu nyingi Sana.

Mojawapo ni watu kutokuwajibika, viongozi na wananchi kutokuwajibika.

Kwa uelewa wako, kuchimba shimo la Choo kwa Watu na kutengeneza Choo kunahitaji msaada WA serikali au mataifa mengine?

Kule Kwetu Makanya, Same na Mkoa wa Kilimanjaro
Ujenzi wa madarasa, matundu ya Choo kwa sehemu kubwa unafanywa na wanakijiji wenyewe au Wanafunzi.

Mfano, shuleni kwetu kulikuwa na utaratibu, mwanafunzi akipata F Moja anapiga matofali 20 siku za wikiendi.

Mimi nilifanya kosa la kwenda shule ya jirani kwenye michezo bila kufuata taratibu. Nikapewa adhabu ya kupiga tofali mia Tatu. Nikafyatua na inatakiwa uyakabidhi yakiwa mazima.

Matofali Yale yalitumika kujenga madarasa, na vyoo.

Ujenzi wa mitaro na barabarani au MiTo ya kumwagilia mashambani Kule kwetu hufanyika kwa misaragambo.
Serikali Kazi yake ni kutoa mchango kidogo tuu

Kufupisha, wananchi wanapaswa wawajibike.

Kule kwetu mwanamke na mwanaume lazima wote wafanye Kazi.

Sio unampa mtu Lawama mtu mwingine kwa Jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako.

Serikali ya Tanzania na nyingi za kiafrika zinafeli kwa sehemu kubwa kwa sababu wananchi wake hawataki kuwajibika na wanazalisha viongozi wasiowajibika.
Wanapenda mambo ya Burebure

Sasa Rwanda, Kagame kaweza kusolve vitu vidogovidogo hivyo hapa kwetu vinatushinda.

Hii maana yake Kagame ana upeo mkubwa kuliko viongozi wetu. Kama tukipigana nae, viongozi wetu hawana uwezo wa kiakili kumzidi ujanja.
 
Back
Top Bottom