Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Moja ya kosa linalofanywa na wapinzani ni kufikiri wao wakipewa nchi wataongoza watu tofauti na Watanzania waliopo sasa. Ni muhimu kwenye mambo serious yanayogusa future ya nchi yetu hasa mambo ya ulinzi wa nchi, wote tuwe na sauti moja bila kujali wewe ni upinzani au chama tawala. Jeshi ndiyo chombo pekee cha ulinzi wa mipaka ya nchi yetu. Halistahili kubezwa hata kidogo. Kwa hapa East and Central Africa tuna jeshi Imara na bora sana.
Acha ujinga, mbona Trump alipinga ushiriki wa USA vita ya Ukraine na Gaza na bado akapewa kura za kumwaga. Hata DA Ilikataa ziara ya Putin Afrika kusini licha ya kwamba ni jambo la kitaifa.

Unafiki ndio umetufikisha hapa, yaani muungane hata kama kitu ni kiovu?

Kingine sijasikia Lissu wala Mnyika wakisema lolote kuhusu vita hiyo in fact hata zitto anaunga mkono JWTZ kupiga waasi sasa unaposema wapinzani wanaipinga serikali kwenye issue ya vita ni kina nani?
 
👉💥💥

Wacha niache uniache niwaachie.

💥💥👈
 
Sujui kwa nini umeanza na neno “acha ujinga” Hii nayo ni changamoto nyingine kubwa tuliyonayo hapa kwetu ya kujaribu kufikiri matusi ni hoja. Nadhani unatakiwa kuniomba radhi, tunaweza kujadili bila kuvunjiana heshima na hiyo ndiyo inatufanya tujenge hadhi yetu mbele ya wengine.

Tukirudi, kwenye mada ya mtoa hoja na hoja yangu; hatuwezi kufikiri jeshi letu ni dhaifu na tukafanikiwa kama nchi wheather wewe ni CCM au mpinzani. Jeshi halilindi vyama bali linalinda Raia. Jeshi letu limekuwa tested kwa namna mbalimbali na limeprove kuwa jeshi imara na lenye nidhamu kubwa. Imagine baada y akifo cha JPM tungekuwa na jeshi la hovyo nini kingetokea??

Vijana wengi wenye haiba za upinzani wamezodoa jeshi letu sana, ushahidi angalia kwenye uzi huu, twitter nk na ndiyo maana mtoa hoja akaja na uzi huu. Na mimi ninasema, lazima tuliunge mkono jeshi letu. Kuhusu kukataa vit fulani hilo ni jambo la kawaida lakini kudharau jeshi letu sio sawa na haipaswi kuunga mkono.
 
Jeshi halilindi vyama bali linalinda Raia.
Sio kweli, jeshi linailinda CCM mara kibao tu wapinzani wanatekwa, chaguzi zinaibiwa na serikali kuingia mikataba mibovu ya kuuza rasilimali zetu ila jeshi lipo kimya tu. Hata upinzani ukipanga maandamano unasikia jeshi linataka kufanya usafi!! Hii ni nidhamu gani?
Nadhani unatakiwa kuniomba radhi,
Kumradhi sana mkuu it won't happen again.
Vijana wengi wenye haiba za upinzani
Unawajuaje? Hao ni mashabiki tu hata kadi hawana. Ni muhimu misimamo ya chama uichukue kutoka official sources za chama sio post za sisi washabiki wa vyama. Maadam Lissu, Zitto n.k hawajasema lolote basi ni fair ukisema upinzani haujaonyesha hiki unachodai.
Kuhusu kukataa vit fulani hilo ni jambo la kawaida lakini kudharau jeshi letu sio sawa na haipaswi kuunga mkono
Umemsikia malema? Kakosoa uwezo wa jeshi la South Africa licha.
Na mimi ninasema, lazima tuliunge mkono jeshi letu
Sio lazima, nimekupa mfano wa Trump amekua akikosoa majeshi ya US yanayolinda na mpaka na hata aliposhinda kafanya teuzi mpya nyingi ili kubadili jeshi hilo. Tuache unafiki ndio unaotumaliza, sasa M23 imetupiga majeshi zaidi ya 7 na kuteka Goma na sasa wanaelekea Bukavu bado tusifiane tu!! Si tutakua delusional.
 
Sio kweli, jeshi linailinda CCM mara kibao tu wapinzani wanatekwa, chaguzi zinaibiwa na serikali kuingia mikataba mibovu ya kuuza rasilimali zetu ila jeshi lipo kimya tu. Hata upinzani ukipanga maandamano unasikia jeshi linataka kufanya usafi!! Hii ni nidhamu gani?
Mkuu Zitto Junior; hayo uliyoyataja siyo majukumu ya JWTZ; hayo ni majukumu ya vyombo vingune vya ulinzi na usalama. Ni muhimu sana kuchora mstari huo ili kuavoid distortion. Unaweza kupitia majukumu ya JWTZ hapa; Mwanzo-Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
Kumradhi sana mkuu it won't happen again.
Appology noted. Huu ni uungwana.
Unawajuaje? Hao ni mashabiki tu hata kadi hawana. Ni muhimu misimamo ya chama uichukue kutoka official sources za chama sio post za sisi washabiki wa vyama. Maadam Lissu, Zitto n.k hawajasema lolote basi ni fair ukisema upinzani haujaonyesha hiki unachodai.
Hili kwangu lilikuwa ni angalizo kwa wapinzani wenye fikra hizo. Kama kwako haina mashiko haina shida tuishi.
Umemsikia malema? Kakosoa uwezo wa jeshi la South Africa licha.
Malema pia ni aina ya wapinzani very conservative, mimi sio muumini wa siasa za aina hiyo. Kwangu mimi kiongozi anayekosoa uwezo wa jeshi la Nchi yake siwezi kumuunga mkono.
Sio lazima, nimekupa mfano wa Trump amekua akikosoa majeshi ya US yanayolinda na mpaka na hata aliposhinda kafanya teuzi mpya nyingi ili kubadili jeshi hilo. Tuache unafiki ndio unaotumaliza, sasa M23 imetupiga majeshi zaidi ya 7 na kuteka Goma na sasa wanaelekea Bukavu bado tusifiane tu!! Si tutakua delusional.
Conclusion kuwa M23 imepiga majeshi zaidi y saba ni misleading kwani sisi hatuko kwenye uwanja wa vita. Tunachojua pale kuna mission mbili moja ya MONUSCO na nyingine ya SAMIDRC. Na zote tumechangia wanajeshi. Mission ya MONUSCO haipigani kabisa na hatujui scope ya SAMIDRC inaishia wapi, sidhani kama ni all out offensive. Nadhani ni logical error kuconclude kuwa majeshi ya nchi saba yamepigwa.
 
Sidhani kama ni Jambo la kizalendo kusifia Jeshi la Rwanda na kubeza Jeshi letu. ni kweli tumevurugwa sana na TISS na PDF lakini sio JWTZ yenye historia ya kufanya kazi iliyo tukuka. Cha mhimu ni kuwaasa CCM kuto liingiza jeshi kwenye Siasa zao za kutawala milele. Acha watawale milele kwa kutumia POLICCM na TISS ila waliache jeshi liendelee ku maintain nidhamu tusije kuaibika huko mbeleni
 
Imagine baada y akifo cha JPM tungekuwa na jeshi la hovyo nini kingetokea??
Mkuu wewe ndio umeleta hii hoja, wakiepusha vurugu baada ya kifo cha JPM unaona ni majukumu yao ila vurugu za kwenye chaguzi 2020 mpaka watu wanauawa zanzibar unaona sio majukumu yao? Kuzuia maandamano yaliyo kikatiba eti kwa kigezo cha "kufanya usafi" ni majukumu yao?
 
Mkuu,

Kwa maoni yangu, Rais anavyokuwa amefariki akiwa madarakani, Jeshi linakuwa vigillant kwa kuwa ni kipindi hatari kwa Nchi. Na kumbuka Amir Jeshi Mkuu anakuwa hayupo at that point mpaka aapishwe mwingine kwa mujibu wa katiba. Nadhani walifanya kazi yao vizuri ukirejea pia press ya CDF mstaafu. Na ninadhani hoja yangu ilikuwa hiyo na kwa contecxt hiyo wanakuwa wakitimiza jukumu lao.

Nje ya hapo, kwa hayo mengine ni majukumu ya watu wengine, walaumiwe hao badala ya kutupa mpira kwa JWTZ kwa maoni yangu.
 
Kwahiyo nchi kuongozwa na mafisadi ambao wanauza rasilimali za nchi yetu sio risk ya usalama wetu? Au mtu kuvuruga uchaguzi na kupelekea vifo na machafuko sio risk ya kiusalama?

JWTZ hawawezi kwepa lawama, wangekua serious huu uchafu wa CCM usingefanyika. Mfano walipewa tender ya kulinda Mererani ila bado Mama samia alisema dhahabu ilitoroshwa kama kawaida, hao JWTZ walikua wapi?

Mie naamini jeshi likitoa onyo kwa wizi wa kura tutaona chaguzi huru na haki na hivyo kuepusha machafuko
 
Kwahiyo nchi kuongozwa na mafisadi ambao wanauza rasilimali za nchi yetu sio risk ya usalama wetu? Au mtu kuvuruga uchaguzi na kupelekea vifo na machafuko sio risk ya kiusalama?
With due respect Mkuu, hii sio kazi ya JWTZ. Ni muhimu kujikita kwenye majukumu yao. Na wakifanya hicho unachokitaka ni risk zaidi, God forbid.
JWTZ hawawezi kwepa lawama, wangekua serious huu uchafu wa CCM usingefanyika. Mfano walipewa tender ya kulinda Mererani ila bado Mama samia alisema dhahabu ilitoroshwa kama kawaida, hao JWTZ walikua wapi?

Mie naamini jeshi likitoa onyo kwa wizi wa kura tutaona chaguzi huru na haki na hivyo kuepusha machafuko
Hii si kazi yao; haiko kwenye majukumu yo, wakifanya unachokitaka maana yake wapindue nchi. Is this what you want??
 
Nenda shule ukadai ada yako,
hata mtoto mdogo anajua Rwanda ikigusa tz siku haitaisha kitakuwa kijiji kimojawapo cha vijiji vya tz na wao wenyewe wanajua

Silaha zao zinapita bandarini Africa mashariki wahusika wanaziona wanazijua , silaha za bongo unazijua wewe? Acha kusifia ujinga, yaani kijiji kishinde nchi ya watu 60m?
Punguza ujinga
Kwa teknolojia gani tuliyonayo mkuu? Jeshi limesheheni MAKADA wa CCM watashindia vita wapi? Acha mzaha basi.
 
Hizo sio sababu, angalia waisrael wanavyohamia kwenye nchi za watu lakini likija swala la vita hawakamatiki kiurahisi.
Na hilo suala linazua mtafaruku hata US kipindi cha Biden au hufuatilii mambo?
 
Back
Top Bottom