Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Badala ya kuwekeza kwenye jeshi na teknolojia nyie mnawekeza kwa machawa, Sifa anazopewa Rwanda ni za kweli....Maisha ni kitu cha wazi sana kila mtu anaona.
Rwanda haina chochote cha kweli.

Msumbiji kaenda kulinda makampuni ya Mfaransa na Ufaransa ndiyo imetoa hiyo tenda kwa Rwanda.

Congo anapigana na wanamgambo, Congo haina jeshi.

Vikosi ya Malawi, Afrika ya Kusini na Tanzania vimeenda kule kwa mission ya amani na wala si ya vita. Aliyekuwepo kwenye vita ni Rwanda.

Hata hivyo vikosi vya Sadc vinaingozwa na South Africa ambao nao wanapokea maelekezo kutoka UN na mfano wake ni juzi waliambiwa wasiendelee na mapambano.

Rwanda ni mwepesi hana nguvu ya namna yoyote. Nguvu pekee aliyokuwa nayo ni ya propaganda anayotumia kuwajaza watu hofu na kuwajaza wa-Rwanda ujinga kuwa nchi yao ni kubwa na ina uwezo wa kukabiliana na taifa lolote hapa Afrika. Huu ni ujinga! Na hii ni dunia, ni vizuri ukaifahamu nafasi yako.

Jwtz lipo Mtwara! Limefanya kazi kubwa sana kuleta amani na kuwafukuza magaidi wa Msumbiji.

Pauline wakazi wa Mtwara hali ya usalama awali ilikuwaje na sasa ipoje! Magaidi walikuwa wanataka kumege Mtwara na kisha kuelekea Lindi.

Nyinyi wa mikoa mengine huko isiyokuwa na kambi au hampo mipakani hamjui mambo yanayoendelea huko! Hivyo mnaandika chochote matakachojisikia.

Waulize wakazi wa Mtwara au lipia nauli nenda kajionee mwenyewe!
 

Hakuna future kwa nchi inayoshindwa uwezo wa kuprovide maji kwa wananchi.

Kama nchi ina migao ya maji wakati imezunguukwa na ziwa victoria, Tanganyika, Nyasa, Bahari ya hindi jua hiyo nchi ikipambana na Rwanda ya Kiongozi Smart itachakazwa vibaya sana.

Sisi tunaweza kudeal na mzee Kibao, Soka, Mawazo, Abdu Nondo lakini vitu vya maana hatuwezi.
 
Jeshini wapo wanaulinda Taasisi, wapo wanaolinda rais na wapo wanaolinda nchi na nafikiri umenielewa.

Huyo mama yupo kukamilisha taratibu za kisiasa kulingana na kanuni na mwongozo wa kisheria unavyotaka.

Ila mengineyo wapo ambao wanaoyasimamia.

Hakuna ambaye anayemuonea wivu Kagame. Suala ni usalama wa nchi, kama mambo huyafahamu omba ufahamishwe.
 

Mkuu uliwahi kushika Binacular ya aina yoyote?
Mimi ninayo Moja ambayo matumizi yake inategemea unataka kuangalia wapi na kuna sehemu mbili za adjustments, Moja ya umbali au ukaribu, ya pili ukiigeuza unaweza kubadili lenzi za Binacular kwa kuadjust tuu. Yaani mbele kukawa nyuma nyuma kukawa mbele.

Hakuna anayemuonea Wivu Kagame Wala Warwanda Mkuu.

Wewe upo na Mkeo alafu kutwa Mkeo anamsifu Taikon Master huku akikudharau wewe unayemlinda. Hiyo kwako inamaanisha kitu gani?
 
Jeshi limesaliti wananchi wake wanaopotezwa na halitoi tamko lolote jeshi limesaliti wananchi wake kuendelea kulinda chama tawala kushinda chaguzi hivyo Hilo sio jeshi la nchi ni la chama tawala hizi sio zama za mazuzu kudanganyana
Majukumu muhimu ya Jwtz ni yapi?
 
Duh .. kwahiyo mtu alisema bajeti ya jeshi la Rwanda ni Dola z kimarekani 5.3 milioni analidunisha jeshi la Bongo?
 
Uwezo wa nchi unapimwa kwa mambo ya msingi.

Nchi ambayo bado inapewa misaada ya matundu ya vyoo na ambayo inapoteza watoto wadogo wenye damu ya kisiasa inayochemka kama akina Soka nakuhakikishia, nchi hiyo ni failure ktk anga zote.

Akili isiyoweza kusolve matatizo ya msingi kama vile maji, matundu ya vyoo, madawati usitegemee inaweza kuwa nzuri kwenye mambo complex kama ya ulinzi ktk geopolitics.
 
A very poor hypothesis, as the matter of fact it's rubbish.
Theories zako ni za kitoto mno, jeshi imara linajengwa kuanzia kwenye recruiting(si hawa wetu wanaoingia kwa vimemo, siku hizi hata TISS mpaka uwe UVCCM) na training.

Utawezaje ku-recruite watu ambao wanamitazamo hasi, mioyo ya hofu, wasio na Nidhamu, na wasio na Imani.
Au unafikiri Jeshini ni Jela la kufundisha watu Nidhamu?
Jeshini wanatakiwa watu ambao tayari Wana Nidhamu.

Kuhusu hayo ya UVCCM kuingizwa huko kwenye jeshi au TISS kimagumashi kama kuna Jambo hilo serikali iliangalie.
Vigezo vifuatwe

Back in the day things were different.
As long as things on the ground zinatuonyesha kuwa jeshi la PK liko vizuri haiwezekani watu
Embu toa hizo Takwimu zinazoonyesha kwa ground Jeshi la Rwanda liko vizuri kushinda Jeshi Letu.



Unaposema Comments za mitandaoni unamaanisha nini?
 
Soma vizuri uelewe Mkuu.
Naelewa mantiki yako but kiukweli lazima tujipange zaidi hasa tusisifie ubora wetu ardhini. Vita Leo imehamia hewani ndege bila rubani. Tusibweteke hata huko ardhini tuhakikidhe mifumo Bora ya ulinzi.
Nb.
Mfumo wa namna rec ruitment wapatikanavyo utizamwe . Waingie vijana wenye mori kweli kweli. Adui hatumjui vyema.
Lakini nikuulize boss Kuna chochote Cha ajabu kati yetu na wanyarwa?
 

Mkuu, nchi kushindwa baadhi ya ishu ni mchanganyiko wa Sababu nyingi Sana.

Mojawapo ni watu kutokuwajibika, viongozi na wananchi kutokuwajibika.

Kwa uelewa wako, kuchimba shimo la Choo kwa Watu na kutengeneza Choo kunahitaji msaada WA serikali au mataifa mengine?

Kule Kwetu Makanya, Same na Mkoa wa Kilimanjaro
Ujenzi wa madarasa, matundu ya Choo kwa sehemu kubwa unafanywa na wanakijiji wenyewe au Wanafunzi.

Mfano, shuleni kwetu kulikuwa na utaratibu, mwanafunzi akipata F Moja anapiga matofali 20 siku za wikiendi.

Mimi nilifanya kosa la kwenda shule ya jirani kwenye michezo bila kufuata taratibu. Nikapewa adhabu ya kupiga tofali mia Tatu. Nikafyatua na inatakiwa uyakabidhi yakiwa mazima.

Matofali Yale yalitumika kujenga madarasa, na vyoo.

Ujenzi wa mitaro na barabarani au MiTo ya kumwagilia mashambani Kule kwetu hufanyika kwa misaragambo.
Serikali Kazi yake ni kutoa mchango kidogo tuu

Kufupisha, wananchi wanapaswa wawajibike.

Kule kwetu mwanamke na mwanaume lazima wote wafanye Kazi.

Sio unampa mtu Lawama mtu mwingine kwa Jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako.

Serikali ya Tanzania na nyingi za kiafrika zinafeli kwa sehemu kubwa kwa sababu wananchi wake hawataki kuwajibika na wanazalisha viongozi wasiowajibika.
Wanapenda mambo ya Burebure
 

Sahihi Kabisa.
Kuna Sababu mbalimbali za vijana kuwa na morali.
Hizo propaganda zinafifisha Morali za Watanzania
 
Msichanganye siasa na usalama wa nchi, ukiona watu wamekaa kimya basi jua wamepima na wameona hakuna shida,

vyombo vya ulinzi vikiamua lake hata ujifiche wap na kikundi chako mtadakwa tu.

Siasa zisiwadanganye mkaona nchi ipo ipo tu ki-hasara hasara,

Kuna watu baadhi nawafahamu ambao nyumbani kwenye familia yake anaonekana kwa mwaka mara 1.

Ikitokea umesikia story za hawa jamaa ndio utajua haujui.
 
Poleni sana...
 
Hivi Rwanda ina ukubwa kama wilaya moja ya korogwe tu au imezidi? Yaani siku Rwanda au M23 wakijichanganya wakavamia bongo jina lao litabadilika
Congo kubwa mara tatu kuliko Rwanda ila inachapwa na Rwanda.

Wingi wa pua si ukubwa wa makamasi.
 

Sasa Rwanda, Kagame kaweza kusolve vitu vidogovidogo hivyo hapa kwetu vinatushinda.

Hii maana yake Kagame ana upeo mkubwa kuliko viongozi wetu. Kama tukipigana nae, viongozi wetu hawana uwezo wa kiakili kumzidi ujanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…