Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimeona maandiko mengi huku mitandaoni yakijaribu kuonyesha kuna uadui au kambi mbili kubwa zinazokinzana kati ya Mbowe na Lissu. Hizi propaganda zimefika mbali kiasi kwamba sasa hata chaguzi za ndani za CHADEMA zinahusishwa katika kihoja hiki cha propagandai! Kila mara ninapokutana na nyuzi hizi za kuonyesha Lissu na Mbowe wametifuana huwa napatwa na kichefuchefu kwa sababu ni propaganda za kibwege sana.
Sijajua chanzo cha propaganda hizi dhaifu ni nini ila itoshe kusema nchi ina watu wenye uwezo mdogo mno hata katika kufanya propaganda za kisiasa. Mtu yeyote mwenye akili hata ndogo za kuvukia barabara anaweza kusoma mazingira ya kisiasa ya ya CHADEMA akafahamu sio Mbowe au Lissu anayeweza kutaka kumuondoa mwenzake katika nafasi yake ya sasa kwa wakati huu kwa sababu hakuna mbadala wao sahihi katika kipindi hiki kifupi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Mbowe akimundoa au akimuhujumu Lissu katika nafasi yake nani mwingine anayeweza kushika nafasi ya Lissu na kuijaza ikamtosha hata kumkaribia Lissu ambaye kwa sasa unaweza kusema hawezi kukosekana katika listi ya wanasiasa watatu maarufu zaidi nchi hii? Kwa upande mwingine Mbowe ndiye msuka mipango yote ya CHADEMA kupata fedha za kujiendesha na oparesheni zake mbalimbali za kuwafikia wananchi, sasa Lissu atakuwa mpuuzi namna gani kutaka mtu aina hii aondoke katika nafasi yake katika kipindi hiki muhumu hivyo?
Jambo lingine ni kwamba hawa wawili hawana platforms nyingine wanayoweza kufanya siasa zao nje ya CHADEMA kwa sasa na wakaeleweka. Mbowe au Lissu hawewezi kukanyaga CCM au ACT kwa namna yoyote, hawawezi kuanzisha chama kipya cha siasa kwa sasa kwa hiyo hata kama hawapendani inawalazimu tu kukaa pamoja na ku-compromise hadi hapo watakapomaliza uchaguzi wa 2025.