kuna pastari mmoja kijana hapa dar alipenda sana kuvaa pensi huku anatembea mitaani watu wakahoji aliwajibu dar ni joto lazima avae vile. Akiwa anahubiri jumapili moja akamtetea mke wake mvaa vimini kuwa atavaaje magauni marefu, je yakimzongazonga na kuanguka, kero yote ya nini?. Kanisani kwake vijana walivaa na kunyoa mitindo yote kwa uhuru. Yupo mwingine naye ni kijana maarufu sana katika kazi yake ya sanaa ya uchekeshaji nadhani mnamjua huyu mwamba, yeye kaanzisha kanisa na linazidi kupata umaarufu, anaruhusu uende kuabudu kwake jinsi ulivyo. Ukitengwa na kufukuzwa kanisani kwako yeye anakupokea. Kanisani kwake wamejaa vijana na mabinti waliovaa ki ajabuajabu fresh tu. Yeye mwenyewe uvaaji wake ni utata mtupu japo ana suti za heshima ya uchungaji wake. Yule mwamba dhamiri haimchomi kupanda madhabahuni na nguo za kihuni, praise worship team yake sasa walivyovaa utashangaa unaweza kudhania upo amerika na ulaya, ni nguo za ajabu balaa