Tetesi: Protase Kardinali Rugambwa atajwa kumrithi Papa Francis

Tetesi: Protase Kardinali Rugambwa atajwa kumrithi Papa Francis

Protase Kardinali Rugambwa tayari ametua Vatican kwa ajili ya mchakato wa Papa Mpya. Anatajwa kumrithi Papa Francis. Tunamuombea apeperushe Bendera ya Tanzania Kimataifa.

**Huu ni mwaka wetu Watanganyika [Janabi na punde Rugambwa]

**** Kagera tujipange kwa kuunda kamati ya Maandalizi iliyojaa Wasomi na wafanyabiashara wakubwa tuwe na mapokezi makubwa dunia itutambue.
Umesahau kwamba ni mweusi. Toka Papa Petro hadi hadi anayesimamia Vatican kwa sasa umeshawahi kuona ngozi nyeusi?
 
Ila Rugambwa yupo kwenye Conclave tayari na ameenda
Concrave anaingia kufanya nini???🤣🤣🤣 Hata mazishi bado!!
Gentleman acha kulinganisha siasa za mia mbili mia mbili na mambo bya kanisa Katoliki,hapa tuachie wenyewe, wewe endelea na habari za MAMA ANAYEUPIGA MWINGI 🤔🤔🤔

Hopefully you do understand my friend Gentleman 😀😀😀
 
Wewe hulijui kanisa Katoliki, Takatifu la Mitume, hujui taratibu za kumchagua Papa, unafikiri namna anavyopatikana ni kama WASIRA alivyochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM?? 🤔🤔🤔

Nakusikitikia sana, mambo ya wakatoliki tuachie wakatoliki wenyewe.

Kifupi Makadrinali kutoka pande zote za dunia ambao wana umri chini ya miaka 80 ndiyo wenye haki ya kupiga kura kuchagua au kuchaguliwa kuwa pope, ambapo uliyemtaja yupo ndani ya sifa hizo.

Makadrinali Huwa wanachagua Papa kwa kuongozwa na roho matakatifu baada ya kusali na kujifungia katika faragha ndani ya kusanyiko Congregation ya Makadrinali kwenye kanisa linaloitwa SISTINE CHAPEL.
hakuna mawasiliano ya Internet wala simu, kwenye hiyo kusanyiko liitwalo Conclave,wanalala humo, na kusali humo na kula humo bila kutoka nje ya hiyo conclave wakati wa kuchagua Pope mpaka anapopatikana.

Uchaguzi unapaswa kuitishwa ndani ya siku 14 au 20, yaani wiki 2 mpaka wiki tatu Toka papa kufariki au kujiuzuru, lengo kuwezeaesha Makadrinali kusafiri Toka pande mbalimbali za dunia.

Katika vikao vya awali hata Makadrinali waliozidi miaka 80 wana haki ya kushiriki, isipokuwa inapofikia hatua ya kuanza mchakato rasmi wa kuchagua kupiga kura ,hawaingii kwenye conclave kuchagua papa, Bali wale tu ambao wana umri chini ya miaka 80.

Toka kuingia conclave na kuanza kupiga kura,haijawahi kuzidi siku nne au Tano kumpata papa!!

Ni mwaka 1831 tu ambapo mchakato wa kumpata papa ulikwenda mpaka siku 53 karibu miezi miwili ndio Papa akapatikana.

Ishara kuwa papa amepatikana ni Moshi mweupe unaotokana na karatasi za kupigia kura zilizochomwa, kupitia kwenye dohani.

Ikiwa papa hajapatikana ni Moshi mweusi unaotokana na karatasi zilizopigiwa kura, zinazopakwa madini flani ili utokee Moshi mweusi.

Mara papa anapopatikana ataenda kuvaaa nguo za kipapa nyeupe, na viatu vyekundu, ambapo papa mavazi hayo yanakuwa yameshonwa mapema na familia ambayo ya washonaji wa mapapa kwa miaka na miaka.

Zinashonwa pair angalau zisizopungua tatu mpaka nne, Papa Ikitokea mrefu mwembamba, au mrefu mnene, mfupi mnene, mfupi mwembamba, ili mradi papa anapochaguliwa akapatikana, lazima avae na atoke kwenye verandah ghorofani saint Peter square ambapo wakristu wanakuwa wamekusanyika.

Moshi mweupe unatokea, pope anatokea anatotoa baraka yake ya kwanza kwa Lugha ya kilatini.

Kabla Pope hajatokea ni Moshi mweupe na maneno ya kilatini HABEMUS PAPAM" we have already Pope , Tunaye Papa tayari.

Haya mengine ni nyongeza, Nia yangu kukuonya mtoa uzi uache kupotosha NA KULINGANISHA UCHAGUZI WA POPE SAWA NA UMAKAMU MWENYEKITI WA WASIRA, au mchakato bwa KUMPATA ASKOFU WA K.K.K.T Tanzania katika mambo yetu ya imani sisi wakatoliki

Ni maongozi ya roho matakatifu, baada ya kusali sana, sio hizo ramri zako unazopiga.

Acha kuwapotosha watu wasiojua kuhusu uchaguzi wa Pope,kama hujui naomba ukae kimyaa kuliko kufanya upotoshaji wako au betting.

🙏🙏🙏
Asante sana kwa maelezo mazuri.

Naomba kuuliza kama unaweza kufahamu uchaguzi wa rais wa baraza la Maaskofu, huwa ni zamu labda la jimbo hili au kuna kuwa na kupiga kura?
 
Asante sana kwa maelezo mazuri.

Naomba kuuliza kama unaweza kufahamu uchaguzi wa rais wa baraza la Maaskofu, huwa ni zamu labda la jimbo hili au kuna kuwa na kupiga kura?
Swali lako limeenda kushoto nyoosha maelezo upewe jibu
 
Protase Kardinali Rugambwa tayari ametua Vatican kwa ajili ya mchakato wa Papa Mpya. Anatajwa kumrithi Papa Francis. Tunamuombea apeperushe Bendera ya Tanzania Kimataifa.

**Huu ni mwaka wetu Watanganyika [Janabi na punde Rugambwa]

**** Kagera tujipange kwa kuunda kamati ya Maandalizi iliyojaa Wasomi na wafanyabiashara wakubwa tuwe na mapokezi makubwa dunia itutambue.
Hakuna papa mweusi. Hapo ndio mtawajua wazungu roho zao ndaaani kabisa.
 
Wewe Kibwengu acha ubishi yupo tayari huko kashaenda.
By virtue of being Cardinal ni lazima awepo kwenye huo mchakato. Kwahiyo kitendo cha yeye kuhudhuria sio jambo la kustaajabisha na kuja la jibu la moja kwa moja kuwa yeye ndiye, bali yeye ni sehemu ya washiriki halali wa huo mchakato.
 
Hawa hapa, kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya Vatican na BBC

1. Pietro Parolin
Nationality: Italian
Age: 70,

2. Luis Antonio Gokim Tagle
Nationality: Filipino
Age: 67

3. Fridolin Ambongo Besungu
Nationality: Congolese
Age: 65


4. Peter Kodwo Appiah Turkson
Nationality: Ghanaian
Age: 76
Hamna prediction hapo unapotosha, ni maongozi ya Mungu roho matakatifu sio vinginevyo!!!


Acha kupotosha
 
Concrave anaingia kufanya nini???🤣🤣🤣 Hata mazishi bado!!
Gentleman acha kulinganisha siasa za mia mbili mia mbili na mambo bya kanisa Katoliki,hapa tuachie wenyewe, wewe endelea na habari za MAMA ANAYEUPIGA MWINGI 🤔🤔🤔

Hopefully you do understand my friend Gentleman 😀😀😀
Subiria muda utaongea Kibwengu
 
Back
Top Bottom