Wewe hulijui kanisa Katoliki, Takatifu la Mitume, hujui taratibu za kumchagua Papa, unafikiri namna anavyopatikana ni kama WASIRA alivyochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM?? 🤔🤔🤔
Nakusikitikia sana, mambo ya wakatoliki tuachie wakatoliki wenyewe.
Kifupi Makadrinali kutoka pande zote za dunia ambao wana umri chini ya miaka 80 ndiyo wenye haki ya kupiga kura kuchagua au kuchaguliwa kuwa pope, ambapo uliyemtaja yupo ndani ya sifa hizo.
Makadrinali Huwa wanachagua Papa kwa kuongozwa na roho matakatifu baada ya kusali na kujifungia katika faragha ndani ya kusanyiko Congregation ya Makadrinali kwenye kanisa linaloitwa SISTINE CHAPEL.
hakuna mawasiliano ya Internet wala simu, kwenye hiyo kusanyiko liitwalo Conclave,wanalala humo, na kusali humo na kula humo bila kutoka nje ya hiyo conclave wakati wa kuchagua Pope mpaka anapopatikana.
Uchaguzi unapaswa kuitishwa ndani ya siku 14 au 20, yaani wiki 2 mpaka wiki tatu Toka papa kufariki au kujiuzuru, lengo kuwezeaesha Makadrinali kusafiri Toka pande mbalimbali za dunia.
Katika vikao vya awali hata Makadrinali waliozidi miaka 80 wana haki ya kushiriki, isipokuwa inapofikia hatua ya kuanza mchakato rasmi wa kuchagua kupiga kura ,hawaingii kwenye conclave kuchagua papa, Bali wale tu ambao wana umri chini ya miaka 80.
Toka kuingia conclave na kuanza kupiga kura,haijawahi kuzidi siku nne au Tano kumpata papa!!
Ni mwaka 1831 tu ambapo mchakato wa kumpata papa ulikwenda mpaka siku 53 karibu miezi miwili ndio Papa akapatikana.
Ishara kuwa papa amepatikana ni Moshi mweupe unaotokana na karatasi za kupigia kura zilizochomwa, kupitia kwenye dohani.
Ikiwa papa hajapatikana ni Moshi mweusi unaotokana na karatasi zilizopigiwa kura, zinazopakwa madini flani ili utokee Moshi mweusi.
Mara papa anapopatikana ataenda kuvaaa nguo za kipapa nyeupe, na viatu vyekundu, ambapo papa mavazi hayo yanakuwa yameshonwa mapema na familia ambayo ya washonaji wa mapapa kwa miaka na miaka.
Zinashonwa pair angalau zisizopungua tatu mpaka nne, Papa Ikitokea mrefu mwembamba, au mrefu mnene, mfupi mnene, mfupi mwembamba, ili mradi papa anapochaguliwa akapatikana, lazima avae na atoke kwenye verandah ghorofani saint Peter square ambapo wakristu wanakuwa wamekusanyika.
Moshi mweupe unatokea, pope anatokea anatotoa baraka yake ya kwanza kwa Lugha ya kilatini.
Kabla Pope hajatokea ni Moshi mweupe na maneno ya kilatini HABEMUS PAPAM" we have already Pope , Tunaye Papa tayari.
Haya mengine ni nyongeza, Nia yangu kukuonya mtoa uzi uache kupotosha NA KULINGANISHA UCHAGUZI WA POPE SAWA NA UMAKAMU MWENYEKITI WA WASIRA, au mchakato bwa KUMPATA ASKOFU WA K.K.K.T Tanzania katika mambo yetu ya imani sisi wakatoliki
Ni maongozi ya roho matakatifu, baada ya kusali sana, sio hizo ramri zako unazopiga.
Acha kuwapotosha watu wasiojua kuhusu uchaguzi wa Pope,kama hujui naomba ukae kimyaa kuliko kufanya upotoshaji wako au betting.
🙏🙏🙏