Tetesi: Protase Kardinali Rugambwa atajwa kumrithi Papa Francis

Machawa wa Mama wanasemaje kwenye hili?
 
By virtue of being Cardinal ni lazima awepo kwenye huo mchakato. Kwahiyo kitendo cha yeye kuhudhuria sio jambo la kustaajabisha na kuja la jibu la moja kwa moja kuwa yeye ndiye, bali yeye ni sehemu ya washiriki halali wa huo mchakato.
Exactly, wewe umenielewa ila kuna Kibwengu hapo naona anarukaruka haelewi kitu ila kujifanya kujua kwingi sana
 
Papa hapatikan kama mgombea binafsi mzee
 
Hahahaha Wahaya bana! Hizo ni akili za kitoto ya kwamba nikikua nitakuwa Rais, it's just a childish behavior.
 
Basi kwa lugha rahisi mchakato wa kumpata rais wa baraza la Maaskofu ni kwa kupiga kura ama ni kwa zamu ?
Ndio hapo umenyoosha maelezo kwa zamu kivipi? Eleza vizuri
 
Hamna prediction hapo unapotosha, ni maongozi ya Mungu roho matakatifu sio vinginevyo!!!


Acha kupotosha
Wewe ndiye unaposha kwa sababu hujui kusoma kwa ufahamu. Mimi nimeweka orodha inayosemwa semwa na vyombo vya habari na nikasema kabisa ''kwa mujibu wa......'' Yaani ni hivi: siyo orodha yangu. Kwa hiyo kama hukupendezwa hiyo siyo issue yangu. Huu ni uchaguzi wako wa kwanza wa papa? Mimi siyo wa kwanza. Na muda wote wanapokuwa wanachagua, huwa kuna majina yanajitokeza zaidi.
 
Mswahili ateuliwe Papa?
Subutu….!
Kwanza wahaya ni watu wanapenda sana sifa na kujiona!
Hilo tu ni sababu ya kukosa sifa ya kuwa papa!.
Lakini ikatokea , mweh!mweh! mweh! mweh !
Majivuno ya wahaya tutashindwa hata kunywa maji na Bukoba watajisifu kwa miaka 100.
 
Cardinali Rugambwa alishafariki kitambo Sana, kaburi lake liko kanisa catholic bukoba, na amehifafadhiwa kama wale mummy WA Egypt
 
Ni nani atakayekuwa Papa ajaye? Uamuzi huo unaweza kuwa na athari kubwa kwa Kanisa Katoliki na kwa Wakatoliki wa Roma wapatao bilioni 1.4 waliobatizwa duniani kote.

Pia, ahadi ya mchakato huu ni kwamba utakuwa wa kushangaza na usiotabirika kwa sababu nyingi.

Chuo cha Makardinali kitakutana katika mkutano wa siri ndani ya Kanisa la Sistine ili kujadili na kisha kupiga kura kwa wagombea wanaowapendelea hadi jina moja litakaposhinda.

Kwa kuwa asilimia 80 ya makardinali waliteuliwa na Papa Francis mwenyewe, hawatakuwa tu wanamchagua Papa kwa mara ya kwanza, bali pia wataleta mtazamo mpana wa kimataifa.

Kwa mara ya kwanza katika historia, chini ya nusu ya wale waliopatiwa haki ya kupiga kura watatoka Ulaya.

Na ingawa chuo hicho kinaweza kutawaliwa na walioteuliwa na Papa Francis, uteuzi wake haukuwa wa watu wa mtazamo mmoja wa “kimaendeleo” au “kihafidhina” pekee.

Kwa sababu hizo, ni vigumu kuliko wakati mwingine wowote kutabiri nani atakayechaguliwa kuwa Papa ajaye.

Je, makardinali wanaweza kumchagua Papa kutoka Afrika au Asia, au wataamua kumpa nafasi mmoja wa watendaji wakongwe wa utawala wa Vatican?

Hapa kuna baadhi ya majina yanayotajwa kuwa waweza kuwa warithi wa Papa Francis — na tunatarajia majina mengine zaidi kujitokeza katika siku chache zijazo.

Pietro Parolin

Nationality: Italian

Age: 70


Luis Antonio Gokim Tagle

Nationality: Filipino

Age: 67



Peter Kodwo Appiah Turkson

Nationality: Ghanaian

Age: 76


Fridolin Ambongo Besungu

Nationality: Congolese

Age: 65



Chanzo: bbc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…