Protectionism ni hatari kwa Maendeleo ya Viwanda

Protectionism ni hatari kwa Maendeleo ya Viwanda

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakati Ujerumani imegawanyika magharibi na mashariki, Ujerumani Mashariki ilishikilia sana hii sera ya protectionism(kulinda viwanda vya ndani). Bidhaa nyingi hazikuruhusiwa kuagizwa toka nje ya nchi hivyo watu wakalazimika kununua kutoka ndani na viwanda vikaweza kuendelea.

Siku ukuta wa Berlin ulivyovunjwa Ujerumani Mashariki ikakuta bidhaa imazozalisha ni kama takataka ukilinganisha na zile za Ujerumani magharibi. Walijikuta wana magari ya teknolojia ya miaka zaidi ya 30 nyuma. Viwanda vyao vingi vikajifia.

Inasemwa kuwa sukari inaweza kutoka Brazil na ikawa bei rahisi hapa kwetu kuliko tunayotengeneza. Chanzo ni kuwa Wabrazili wamewekeza kwenye mitambo, kuanzia shambani nk. Hata cement inaweza kutoka Pakistani ikawa bei rahisi kuliko inayotengenezwa hapa. Lakini protectionism inafanya viwanda vya ndani viendelee kuzembea na kutojiupgrade na wananchi waendelee kupata bidhaa mbovu

Kwa maoni yangu ptrotectionism haina faida ya maana sana. Sanasana inafaidisha wenye viwanda wachache sana huku ikiumiza wananchi na kudumaza maendeleo. Mi nafurahi san kuona mama Samia akiua hiyo kitu, ni adui wa maendeleo na tumekuwa naye kwa miaka 60 bila faida yoyote ya maana.
 
Nadhani tulishatoka kwenye uchumi hodhi. Serikali iliyopita ilijaribu kuturejesha huko lakini madhara yake tukaanza kudhoofisha hata hivyo viwanda vichache tulivyokua navyo kwa kukosa ushindani

Nadhani kuweka standards za juu kwa bidhaa na huduma zinaingizwa nchini ni bora zaidi kwa kutoa changamoto ya ubora ya wazalishaji wa ndani kuliko ku impose protectionism kwa kutumia kodi
 
Hakuna nchi duniani isiyolinda viwanda vyake. Wewe iite 'protectionism', lakini ukweli wenyewe ndio huo.

Hiyo cement inayotoka Pakistan unajuwa kwa nini ni rahisi zaidi kuliko inayozalishwa hapa? Tafuta jibu lake kwanza ndipo ujue kwamba siyo swala tu la 'protectionism'.

Na unapozungumzia sukari ya Brazil, kwa nini usikazie nasi tujitahidi kuzalisha kwa gharama ndogo kama wao, badala tu ya kuhimiza tufungue soko ili viwanda vyetu vife.

Kwa hiyo hapa na mada yako hii unasemaje; tufungulie tuuu kila kitu huku sisi hatujitahidi kuimarisha hivyo viwanda na vyenyewe viweze kuzalisha kwa gharama nafuu na bidha zenye viwango? Tusipovilinda sasa na kuviwezesha kufanya hivyo, tutapata ushindani lini?

Hebu eleza, unataka tulime tumbaku hapa, lakini tusiweze kuzalisha sigara, bali tuuze tumbaku yetu ili tuuziwe sigari hizo zilizotengenezwa kwa tumbaku yetu huko nchi za nje?
Hivyo hivyo, unahimiza tuzalishe pamba kwa wingi, nanasi na matunda mengine kwa wingi, lakini tusiweze kuvisindika vitu hivyo tupate vitu vilivyoongezwa thamani, bali tutegemee tunaowauzia mali ghafi hizo kutuletea vitu hivyo?

Fikra potofu hizi zinatoka wapi?
 
Mnakuja na mifano ya kijinga hapa kutetea uamuzi mbovu wa SSH, mpaka saivi mataifa makubwa yana sera za kulinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa, si USA , Europe wala China hawa wote wanalinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa. Yaani saivi badala ya kutafuta njia ya kuongeza uzalishaji ndani, ushindani uwe wa ndani mnataka tuanze ku import cement na sukari yote nje ? Hizo ndio akili za SSH?

Mwambieni aruhusu pia ardhi ya Zenji pia watanzania wengine waimiliki tuone kama after 10yrs wazenji hawatakuwa shamba boys kwenye ardhi yao. Kuilinda jamii yako dhidi ya ushindani usio sawa ni wajibu wa serikali, ni serikali isiyo na maono tu itakayoruhusu huu ujinga unaoenda kutokea.
 
Protectionism inaleta uzembe, ubwana na umwinyi. Lazima turuhusu ushindani! Viwanda vyetu viwe flexible kuwekeza katika teknolojia. Tuweke sera nzuri za uwekezaji ili wenye mitaji wapate hamasa ya kuja kuwekeza kwa kuweka viwanda nchini. Hamuwezi kuendelea kwa kujifungia ndani na kuumiza wananchi huku wachache wakinufaika, ni upuuzi.

Wawekezaji wa ndani wanaotaka ku upgrade teknolojia ya viwanda vyao, sera iwe rafiki kwao, mitambo na vipuli vya viwanda visitozwe kodi ili kuruhusu uwekezaji zaidi, kodi tutapata kutokana ajira viwandani, mauzo ya bidhaa n.k . Kikubwa ni kuwa wenye viwanda wengi hapa tz wanataka kupata faida tu, they don't invest in technological advancements
 
Kuna kitu kinaitwa dumping kwenye uchumi ungeweza kukizungumzia alongside protectionism hapo ungebalance mzani wa huu uzi
 
Hebu mkuu rudia kusoma bandiko halafu comment tena. Labda this time around utakuja na fikra tofauti
 
Mnakuja na mifano ya kijinga hapa kutetea uamuzi mbovu wa SSH, mpaka saivi mataifa makubwa yana sera za kulinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa, si USA , Europe wala China hawa wote wanalinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa...
Tafakari kidogo sekta ya mawasiliano bila competition ,TTCL only service provider : matokeo non perfomance,poor service, huduma kufikia wachache, teknolgia duni.

Competition is good for the consumer.
 
Back
Top Bottom