Protectionism ni hatari kwa Maendeleo ya Viwanda

Protectionism ni hatari kwa Maendeleo ya Viwanda

Hakuna nchi duniani isiyolinda viwanda vyake. Wewe iite 'protectionism', lakini ukweli wenyewe ndio huo...
We hujaelewa, kasema wenye viwanda wajiongeze na wao kuzalisha bidhaa kwa ufanisi. Maana sukari hiyo ya Brazil inalipiwa kodi kibao na gharama za usafiri lakini inakuwa bei rahisi kuliko ya hapa.

Kipindi cha Nyerere hiyo protectionism ilisaidia nini zaidi ya kuharibu zaidi uchumi wa nchi?
 
Ila importation inaumiza uchumi wetu zaidi! Mie nafikiri encouragement ndio approach nzuri zaidi
Una export Chadema au una export CCM.

Au unaexport Kipigo cha mbwa koko

Hakuna mnachozalisha zaidi ya kufukuzana na Chadema

Hivi kwa wabunge hawa wanaobishana kuhusu nguo kuna Maendeleo ya viwanda?


Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Elezea vizuri mkuu. Ongeza ongeza nyama
Yeah tunatakiwa kuwekeza efforts kwenye uzalishaji tu masoko yapo sehemu mbali mbali ulimwenguni ni kuwa na right product of the right quality at the right time!

Uwekezaji wa Kilimo ndio utatuokoa tu! Ishu ya maparachichi ni moja tu ila tungejikita katika mazao kama yale 20 tu tukawa best producers swala la ajira lingekuwa sio tatizo tena! Graduates wangeajiriwa kwenye estates kila mkoa!

Exporting ingeleta faida kwa uchumi wetu sana
 
Yeah tunatakiwa kuwekeza efforts kwenye uzalishaji tu masoko yapo sehemu mbali mbali ulimwenguni ni kuwa na right product of the right quality at the right time!...
Hii ni hoja inasimama peke yake kabisa mkuu.

Nlitaka useme kidogo kuhusu protectionism. Maana jamaa anasema protectionism inaviangamiza viwanda vyetu na wewe ukaja na hoja tofauti kana kwamba unampinga, kwa madai ya kwamba importation inauwa viwanda vyetu (which I agree with you) lakini kwenye mantiki ya mtoa mada sikubaliani nawe.

Sijui unanielewa Bob????
 
Hii ni hoja inasimama peke yake kabisa mkuu.

Nlitaka useme kidogo kuhusu protectionism. Maana jamaa anasema protectionism inaviangamiza viwanda vyetu na wewe ukaja na hoja tofauti kana kwamba unampinga, kwa madai ya kwamba importation inauwa viwanda vyetu (which I agree with you) lakini kwenye mantiki ya mtoa mada sikubaliani nawe.

Sijui unanielewa Bob????
Protectionism kibongo bongo ni kukumbatia wenye uwezo wa kuzalisha kwa viwango hafifu na kuwanyima fursa watu wenye uwezo toka nje kuja kuwekeza!

Importation inauwa viwanda ofcourse sababu unapoleta bidhaa ambazo zingeweza kuzalishwa hapa nchini ni kuumiza uchumi tu! Tuna ma miti kibao ila mashine ya kufyatulia toothsticks tu zinatushinda tunaagiza mzigo uchina! Hivi kuna teknolojia gani ya ajabu inayohitajika kwenye kuzalisha vile vidude? Kwa mantiki hii kuna mambo ambayo tunaweza kuyafanya wenyewe kabisa ila hatufanyi sielewi sababu ni nini? Kwa ukuaji wa teknolojia ulipofikia kwa sasa tulitakiwa tuwe na capacity ya kuunda magari yetu wenyewe kabisa.

Hata fundi wa muembeni aliyetengeneza corrolla kwa miaka 20 anajua functions za kila part ya gari kiasi ukimpa parts kwenye box anaweza aka assemble na kukufyatulia corrolla kabisa ukapanda na kuendesha!

Tunahitaji foundry plant kwa ajili ya kuchonga parts za vyuma hizo piston na blocks,gearboxes, bolts and nuts! Tunahitaji watu ambao wataenda kujifunza process nzima ya ku assemble parts and we will be a step away from having our first car plant!
 
Lakini pia mkifanya protectionism na kuishia kuuziana vitu vibovu wenyewe kwa wenyewe mnakuwa mnapiga marktime. Na hakuna nchi inaweza kuendelea kwa kuuziana vitu wao kwa wao.
Ni kweli kabisa, angalia mafuta ya Alizeti sasa yanaviwango gani hivyo hata label hayana ni mtu akijua kuchuja anapaki kwenye kidumu anauza imagine hata ingredients huoni na bidhaa nyingi ndo zinatengenezwa hivyo na tena hivyo tunavyoita viwanda vya ndani wala hata havipo, siku hizi mtu anajifungia ndani anasaga karanga au kutengeza mkate anapeleka dukani anauza hata watu wa TFDA hawafiki kutoa kibali baada ya kujihakikishia mazingira salama ya chakula sasa hivyo wiwanda tunavyolinda ni vipi? Na ndo maana ajira hazionekani.
 
Tafakari kidogo sekta ya mawasiliano bila competition ,TTCL only service provider : matokeo non perfomance,poor service, huduma kufikia wachache, teknolgia duni..........
Competition is good for the consumer.
Hata kwa maendeleo pia. Leo tungesema TTCl wabaki peke yao ili kulinda makampuni yetu sijui hali ingekuwaje? sitaki kuwaza.
 
Tu encourage uwekezaji watu walete tech kama ilivyo kwa wachina
Tatizo sisi wenyewe huo uwekezaji hatutaki, tunataka watu wa nje ndo waje kuwekeza na kuingia gharama za kutulipa mishahara na tipu kibao, imagine watu wameanza kwenda Dubai na China kuleta hivyo vitu kuuza ndani lakini kwenda kununua mashine na ujuzi hawakuta kabisa sasa hao watu ukiwa Kama Raisi utaletea nini zaidi ya kuwaletea vitu vya kuuza na kununua.
 
Tatizo sisi wenyewe huo uwekezaji hatutaki, tunataka watu wa nje ndo waje kuwekeza na kuingia gharama za kutulipa mishahara na tipu kibao, imagine watu wameanza kwenda Dubai na China kuleta hivyo vitu kuuza ndani lakini kwenda kununua mashine na ujuzi hawakuta kabisa sasa hao watu ukiwa Kama Raisi utaletea nini zaidi ya kuwaletea vitu vya kuuza na kununua.
Na hii ndio inatumaliza, watu wanatakiwa kununua viwanda na kuvileta tuzalishe na kuwauzia majirani zetu kwa kuanzia. Sababu bidhaa ikiwa nzuri tutauza tu no matter what! Bidhaa complex sio lazima utengeneze yote mwenyewe from scratch tunaweza tuka outsource inputs zingine tukawa tunapewa na viwanda vingine!

Ntakupa mfano wa Toyota sio kwamba anatengeneza gari zima mwenyewe! Kuna electronic parts anachukua Denso au Aisin, Zingine Yamaha, Tyre anachukua Bridgestone au Yokohama. Vioo kuna kiwanda maalum kina supply vioo kwake!

Haya mambo yanawezekana kama tukiwa na akili ya kuchangamka kidogo ila tukifikiria kwa matumbo na kuvizia matobo ya upigaji basi Tanzania itaendelea kuwa dampo na shamba la bibi vizaz na vizazi
 
Pathetic.
Wakati Ujerumani imegawanyika magharibi na mashariki, Ujerumani Mashariki ilishikilia sana hii sera ya protectionism(kulinda viwanda vya ndani). Bidhaa nyingi hazikuruhusiwa kuagizwa toka nje ya nchi hivyo watu wakalazimika kununua kutoka ndani na viwanda vikaweza kuendelea...
 
Wakati Ujerumani imegawanyika magharibi na mashariki, Ujerumani Mashariki ilishikilia sana hii sera ya protectionism(kulinda viwanda vya ndani). Bidhaa nyingi hazikuruhusiwa kuagizwa toka nje ya nchi hivyo watu wakalazimika kununua kutoka ndani na viwanda vikaweza kuendelea...

Haya matatizo yote ni kwakuwa tuna misingi ya kijamaa, kwenye ujamaa ndio mifumo hulazimisha watu waifuate, na sio soko kuamua.

Ukiangalia bidhaa za Kenya nyingi zina ubora mkubwa kuliko za hapa nchini, ila tunajikuta tunatumia bidhaa zenye ubora duni kwani hatuna ushindani wa kweli.
 
Ila importation inaumiza uchumi wetu zaidi! Mie nafikiri encouragement ndio approach nzuri zaidi
Tusikariri Extrovet. Dunia ya leo si ya 1960 wakati tunapata uhuru.

Tunaelekea kwenye technology ambayo daktari wa marekani atamfanyia operation mgonjwa wa TZ akiwa huko huko marekani huku mchango wetu kwenye hiyo technology ukiwa sifuri. Tupo nyuma sana sababu tunajilinda sijui na kitu gani.

Dunia inaenda kuwa kijiji kidogo sana. Tusijifungie, turuhusu ushindani nchini kwa kuruhusu bidhaa mbalimbali za wenzetu na kujenga mahusiano ya kibiashara huku tukiwawezesha wajasiriamali wetu kutengeneza bora zaidi kwa gharama nafuu.

Huwezi kuwa bora kwa kushindana wewe vs wewe mwenyewe ndani. Tutaishia kupaki mahindi kwenye mifuko ya plastic iliyochomwa na mishumaa kuifunga

Mm naona TZ ikiwa nchi ya Uchukuzi Biashara na Kilimo cha kisasa huku tukiboresha utalii tutafanikiwa kuliko kuhangaika na nyimbo za kulinda viwanda. Viwanda vijengwe na matajiri tutakaowatengeneza baada ya kuona fursa na si kulazimisha kwa kujifungia ndani kwamba tunalinda viwanda.
 
Mnakuja na mifano ya kijinga hapa kutetea uamuzi mbovu wa SSH, mpaka saivi mataifa makubwa yana sera za kulinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa, si USA , Europe wala China hawa wote wanalinda bidhaa zao dhidi ya ushindani usio sawa...
Mtu akitazama hoja yako anaweza kuamini una hoja za msingi, ni ujinga kuzuia bidhaa za Kenya, huku za China zimejaa madukani, tena nyingi zikiwa na ubora duni. Hatukatai kulinda viwanda vya ndani, lakini isiwe sehemu ya kutupatia bidhaa duni.
 
Unakuta Mchina ana kiwanda cha kupaki magunia 10000 kwa saa, sisi tunajifungia tulinde viwanda vyetu ambavyo ni vya mikono au gunia 50 kwa siku. Dunia haitasimama kuisubiri TZ, wakati tunazalisha magunia 10000 kwa siku wao wanaviwanda mwezini huko. Tutumie akili ili twende na kasi ya dunia.
 
Hamna cha kupoteza ikiwa mali zitazalishwa hapa hapa na mitaji kutoka nje ya nchi! As long as wazawa watafaidika na kodi zitakusanywa kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla! Bidhaa ziuzwe ndani na nje ya nchi kwa address ya Tanzania
 
Back
Top Bottom