Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

 
Mkuu Mshana,
Nakubaliana na wewe, hata mimi kuna wakati niliishi India, nikasoma sana buthiism, na ku practice ayuverda na pranayaana hivo nika turn vegetarian, pia nimemsoma sana krishna, niliporudi bongo, nikajikuta nashindwa ku mix na watu wangu!, kwanza nilianza kuirudia wine, kisha kuendelea kupiga kinywaji na hatimaye kurudia nyama!.

Wakati wa practive ni kweli nilikuwa poweful, nikajikuta badala ya kuishi kwa raha kufuation high state of alert, unajikuta unaishi kwa mateso, mathalan unagundua baadhi ya watu waliokuzunguka wako kinyume na wewe!, au kuna hiyo siku wife alitoka party ya kazini, sixth sense imekuambia mwenzako "tayari" ili kukuzuga, ajajifanya yuko "high!" akihitaji huduma!. "Mzee" aligoma! lakini aliamshwa!, na kwenye "game" ilibidi ajitahidi sana na ku fake "kufika" mapema kuliko kawaida!. Kupitia mazoezi hayo, unaweza kudistinguish "kufika" kweli na "kufika" fake ili kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust, love na happyness inayeyuka kwa kujua you are cheated!.

Hivyo info nyingine unaachana nazo for love peace of mind and tranquility ya mahusiano!.

Ndio maana ukiwachunguza matajiri wengi, utagundua they are not real happy!. Unaweza kuwajua kwa kuwatazama machoni!. Nimejiamulia bora kubaki masikini happy kuliko tajiri huzuni!. Na sometime ukifuatilia life stily za hao matajiri, licha kula dinner Kempinsky, hawa enjoy kama sisi tunakula chips vumbi!.
Wee acha tuu!.
Pasco.
 
Uzi huu umenivuta kutaka kujua zaidi,hasa hapo kwenye ndoto,mara nyingi kila niliotalo hutokea ni nini hii?msaada zaidi,hrf sijui vizuri kingereza sa pale ulipomwaga ngeli umeniacha.nahitaji msaada zaidi,na swali je!hapo hakuna uhusiano wa kiimani za kidini kama vile maono au kuongozwa na roho mtakatifu?na nini imani yako khs imani za dini?hapa niko njiapanda huwa sijui huku ni kuongozwa kwa nguvu za mizimu au nguvu za mungu?leo nikutana na nguvu zilizo ndani yetu?
 
Asante sana Pasco kwa mada hii.Hili ni jambo ambalo limenitatiza kwa muda mrefu na nimekua nikitamani nifungulie nguvu hizi lakini bado sijafika huko.Nimesoma sana kuhusu haya mambo na ninashukuru kupata kitabu cha The Master Key hiki ndicho kilichonitambulisha kwenye ulimwengu huu.

Ninaendelea kujisomea kila siku na sasa nimejikita kwenye maandiko ya Tibet hssa hasa mafundisho ya Atisha.Ninatumaini nitagika huko ninakokutazamia kwa maana yote haya ni nguvu ya Mind.
 
Pasco hebu nijibu hili swali

watu huwa 'wanaibiwa ' huu uwezo?

manake mimi zamani nilikuwa na uwezo wa ajabu wa mambo meengi mno

now naona kama kuna mtu ameniibia hayo mambo,
je nifanyaje?

The Boss kama nimesoma kwa usahihi kwenye The Book of Wisdom ya Osho,Inasemwa ya kwamba nguvu hizi ni vigumu sana kuzitambua kama uko nazo lakini ni rahisi sana kuzipoteza.Mara nyingi kinachofanya nguvu hizi zikimbie ni Ego..yaani mtu akishaacha kuwa Aware (awareness ni
jambo la muhimu kulifahamu) na kuanza kutumia Ego basi ngivu hizi zinapotea kama zimechukuliwa na upepo wa kisulisuli.Ni sawa tu na wale ambao wanaifungua ile Lotus ya Kundalini vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Pasco hebu nijibu hili swali

watu huwa 'wanaibiwa ' huu uwezo?

manake mimi zamani nilikuwa na uwezo wa ajabu wa mambo meengi mno

now naona kama kuna mtu ameniibia hayo mambo,
je nifanyaje?
Mkuu The Boss, hakuna aliyekuibia, hizo powers bado zipo na unazo, ila zimekuwa dormant kwa sababu hazikutumika!.

Kama nilivyosema mwanzo, kila mtu anazaliwa nazo!, infact zinaanza ku exist since the time of conception!. Ndio maana mtoto akiwa tumboni, unashauriwa zungumza nae, mwambie unampenda!, mkeo akiwa mja mzito, sometimes shika shika tuu tumbo la wife ongea na mtoto kuwa nnamsubiri kwa hamu!.

Baadhi ya watoto ambao mimba zao zilitaka kutolewa zikagoma, wanajua!, hivyo wanakuwa wamezaliwa huku subconcious ikiwaambia "they were rejected!". Letter in life, wanakuja kuwa ma psychopath kwa kufanya mambo ya ajabu, ikiwemo hata kuwa serial killer!, by the time wanayafanya hayo matendo, wanakuwa sio wao, ni sub concious mind yao inakuwa imetake charge, normal concious ikirudi, wanajuta!.

Mtoto akishazaliwa powers zinakuwa very distinct!, mara kibao anaweza kuanguka toka kitandani, akalia tuu ila kiukweli anakua hajaumia kabisa, kihivyo!. Mtoto mchanga akikuangalia anakusoma your mind, kama unampenda anaona, kama unamchukia anajua, anasikia japo hawezi kusema!, ndio maana wakija wachawi anawaona, au akija mtu mbaya, mtoto anastuka analia.

Kadri unavyokuwa, ndivyo powers hizi zinakwenda zikipungua mwisha zinapotea kutokana na kutotumika!.

Mfano mimi nayakumbuka baadhi ya majina ya baadhi ya wanafunzi niliosoma nao nursery school. Nilisoma shule ya St. Petrers Kindagarten Tanga nikiwa just 4 years!, Mpaka leo nayakumbuka baadhi ya majina-Robert Kilala na Ana Kilala, walikuwa wanaletwa shule na baba yao kwenye pikipiki. Kuna David Naburi, Alex Shaba, Jane Mutayoba, Cecilia Minja, na kuna drama nilicheza shule mimi nilikuwa King!. Bado nakumbuka nyimbo za Baba Black sheep etc!.

Lakini cha ajabu, siwakumbuki wanafuanzi niliosoma nao darasa la kwanza na la pili pale Nyanza Mwanza zaidi ya Leonard Mpupua n.a. wimbo wa "sasa sasa saa ya kwenda kwetu!". Na huwezi kuamini, kuna watu nimemaliza nao chuo pale UDSM, wao ndio wananikumbuka kuwa tumesoma darasa moja!.

Ili kwa mujibu wa michango yako humu jf, Mkuu the Boss, unajulisha wazi, "you have the powers!", issue ni kuzifuatilia tuu na kuzifufua!. Ila kama hizo powers ni strange powers, bora ziache tuu ili uishi normal life!.
Pasco.
 
Mh hapa sasa ndio penyewe nimekua nikifanya kitu nahisi kama kuna siku nilishakifanya lakin tatizo sikumbuki ni wapi na lini kwa mfano naweza kukutana na mtu popote pale iwe njiani au kwenye gari na tukianza kupiga piga stori nakuwa kama napata picha ya hayo tunayozungumzia yalishapita lakini kiuhalisia haijawahi kutokea, hapa nitakua katika kundi gani mkuu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pasco huo uwezo wa 'kata funua' bila kusema neno sipati picha
hizo pm za watu uwafundishe utakazopata lol

kikazi je uwezo ako ulikusaidia kupata kazi? kazi ipi kwa mfano?

Na wabongo tunavyopenda habari kama hizi na kwa uwezo wa Pasco kujieleza, akiamua anaweza kuwa milionea kwa muda mfupi sana though anachoeleza kina make sense.
pasco dunia ni yako chaguo ni lako, amua kuendesha Range Rover leo!
 
Last edited by a moderator:

Kama sijakuelewa hivi, ina maana matajiri wote lazima wawe na huu uwezo.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…