Mkuu Slow, Mungu alipomuumba Adam, alimpa uwezo!. Yesu alipokuja alifanya miujiza, na kila muujiza alisema "imani yako ndiyo imekuponya!", kasome
Marko 10 : 52 - Yesu akamwambia, \"Nenda, imani yako imekuponya, na Mathayo 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu;
imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile, au [h=3]
Luka 17:19 "[/h]
Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya..hiyo imani yako ndio "powers from within!". Akasema laiti watu wangekuwa na imani kama punje ya haradali, wangeiambia milima ondoka!, na milima ikahama!", ina maana hizi imani tunazotumia ni ndogo tuu kama mbegu ya mchicha!.
Shetani pia ana powers, ikumbuke hapo mwanzo shetani ndiye aliyekuwa malaika mkuu, alipoasi, alifukuzwa ila hakunyang'anwa zile powers, ndiye aliyemrubuni Eva kule lile "tunda!". Nguvu za shetani hufanya maovu, nazo pia zimo ndani yetu kama hizo nguvu za Mungu!.
Kitendo cha kuamini, ni kufungua tuu milango. Mimi ni Mkristu Mkatoliki, kwa sababu nimezaliwa huku. Wengi hufuata imani fulani kwa kujikuta ndiko walikozaliwa na wanaendelea kujifungia humo humo kwa kuto look beyond!. Nilipokuwa India, nikasoma kidogo imani za Hindu ndipo nikagundua kumbe Christianity ni dini ya juzu juzi tuu, kwa taarifa tuu, dini za kale zaidi ni shamanism na animism, ambazo zilikuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu ila baadae zilifutika!. Kwa sasa dini ya kale zaidi iliyopo ni Hinduism ikifuatiwa na Buddhism zote za India ndipo ikaja Judaism ya Mashariki ya Kati, Israel, ikaja Taoism ya China na Shitoism ya Japan ndipo ikaja Christianity!. Hapo dini zetu za asili, hazitajiwi kabisa kwa sababu hazikuandikwa!.
Uki take time kutoka nje ya box la Ukristu au Uislamu ambamo ndiomo wengi wetu tumejifungia humo, ukachungulia ndani ya Hinduism au Buddhism, ndiko utakutana na real powers za "enlightenment!", kwa sababu dini hizi zinaamini kwenye "higher powers" bila kumtaja Mungu, Ukristu na Uislamu umezifungia milango, ili ukifuatilia uthabiti wa imani, discpline, na nguvu za kusali, utagundua sisi Wakristu na Waislamu tunatania tuu!.
Kiukweli ukizama sana kwenye hizi powers, unaweza kuingia kanisani na kujikuta unashutukia jinsi watu wanavyofungwa kamba, unaweza ukaacha kwenda!. Mimi bado ni Mkatoliki Die hard japo kuna mambo tunafanya ndivyo sivyo, ukishayangundua, unaachana nayo, bali unaendelea kuenenda kanisani kwa kufuata mafundisho ya Biblia na sio lazima yale yote ya kanisa ambayo umeisha yastukia kuwa sio!.
Wengi wakistuka, huamia makanisa ya wakovu, huko pia huwa nina hudhuria Mama yangu ni Esemblies og God, huko nako ndiko sio tuu unakuta kamba nene, bali watu wanapurushwa na kukamuliwa mpaka wanabaki mifupa!. Wale Wachungaji wameishajistukia jinsi ya kutumia hizi powers kucontrol waumini wao!. Wale wanaopataga mwanga hustuka na kujihamia kimya kimya, wengine wenye imani upofu, ni watumwa wa Wachungaji wao na wachungaji hao huwafanya lolote ikiwemo kuwa nani hii wake zao!, wao wakijua ndio baraka zenyewe kumhudumia mtumishi wa Mungu!.
Bwana wetu Yesu Krisu alisema wazi, watakuja watu, watahubiri kwa jina langu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!. Ukifuatilia sana the working of powers, unaweza kuogopa kuendelea ku practice, ila ukiisoma vizuri Bibilia, utagundua mahali mengi pameandikwa "nguvu imo ndani yako"!. Mungu alituumba kwa mfano wake, na katupa nguvu ambazo ndizo hizo powers from "within".
Pasco.