Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Pasco kuna kitabu niliwahi kukisoma zamani na kujaribu kupractise nikawa naona kama inakuwa kweli.ni vitu vya kawaida ila ni rahisi kutokuvifanya kwa kujisahau
Inahitajika kuupa ubongo chakula chake kikuu ambacho ni oxygen then utaongeza thinking capacity against mambo yanayokuzunguka.
Namna ya kulala,Kujenga imani,kupata utulivu wa rangi na fresh flowers vyote hufungua milango ya nguvu hizi
Pia kutoa kiasi ya ulichonacho kws wahitaji hukuongezea,hii niliijaribu nikiwa chuo na ika-work out siku hiyo hiyo.kwa kifupi huwezi kupata zaidi kama hutumii(refer Bill Gates)
Mtu anayepractise njia hizi ile kumtazama tumgonjwa anaweza kujua kama atapona au la..bila kujali muonekano wake wa nje
Hakika nilifikia mahali nikasema ukiacha bible that was my second favourite book...
 
Last edited by a moderator:
Jina la Yesu ndilo lenye nguvu siyo the powers from within acheni kupotosha umma
huyu'nae katokea wapi?acha wenzio tufaudu Pasco unikumbusha enzi za marehemu munga tehenan wa gazeti la jitambue,tupeni ujuzi jamani nyinyi ni walimu na sisi ni wanafunzi wenu,elimu tenu itatusaidia sana,keep it up.
 
Last edited by a moderator:
Wana Jf wenzangu, Chonde, chonde, chonde. naomba naomba sana, sana, sana, mtu ye yote asijaribu kufanya meditation ya aina yo yote ile bila chini ya uangalizi wa mwalimu, ama mtu aliebobea kwenye elimu hiyo. Mimi kwa mara ya kwanza nilifahamu kuhusu meditation mwaka wa 1973, kupitia vitabu vya Tibetan Lama mmoja aitwae Tuesday Lobsang Rampa ambaye nae alikuwa na mwalimu wake aliyeitwa Lama Mingya Dondap. Huyu bwana alikuwa akisisitiza kuwa na mwalimu katika njia hii, kama vile unapokuwa na mwalimu katika masomo ya kawaida darasani. Nilijaribu kufanya meditation bila ya kuwa na mwalimu, lakini nikaacha baada ya kuona kuwa energy ilikuwa ikinizidi na sikujua jinsi ya kui-channel katika mwili wangu. Kwa kuwa nilikuwa na ari kubwa ya kutaka kuijua elimu hii, nilijisomea vitabu mbalimbali vya kuhusu astrology, palmistry, ambapo naweza kusema nime-master sana elimu hii, vile vile kuhusu mambo mengi sana ambayo siwezi kuyaandika yote hapa. Ni sheria ya maumbile kuwa, " when the student is ready, the teacher will come " Mwaka wa 1981, nilipata mwalimu na hadi hii leo naendelea kufanya meditation katika kiwango cha juu kabisa. Ninao watoto wanne, na watatu ni ' Initiates ' na wanafanya meditation ya juu, ambapo walianza tangu wakiwa na umri wa miaka mitano. Meditation ni way of life ili kuweza kutimiza lengo la kuwepo hapa duniani. Meditation siyo dini wala imani yo yote, kwa kuwa ni practical. Meditation ziko za aina nyingi sana, lakini ipo inayoweza kukupeleka katika ngazi ya juu sana na ukafahamu mambo ya ajabu kabisa, kwa wewe kuingia ndani yako kupitia katika jicho lako la tatu. Siwezi kueleza zaidi maana sipendi kuwakwaza kwani sheria zinasema ' know and be humble '. Kwa anaependa kwa dhati, naweza kumuunganisha na " The Path " ama Sant Mat " ambazo zote zipo hapa Tzania na ninaweza kuzi-recommend kabisa. Haya kazi kwenu! 0786-961-542.
 
Pasco
...mathalan
unagundua baadhi ya
watu waliokuzunguka
wako kinyume na
wewe!, au kuna hiyo siku
wife alitoka party ya
kazini, sixth sense
imekuambia mwenzako
"tayari" ili kukuzuga,
ajajifanya yuko "high!"
akihitaji huduma!. "Mzee"
aligoma! lakini
aliamshwa!, na kwenye
"game" ilibidi ajitahidi
sana na ku fake "kufika"
mapema kuliko
kawaida!. Kupitia
mazoezi hayo, unaweza
kudistinguish "kufika"
kweli na "kufika" fake ili
kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust,
love na happyness
inayeyuka kwa kujua you
are cheated!...

...dah!...hapa kwa 'wife' nikama umeunitonesha kidonda,ilishawai kuntokea na kila nikiikumbuka hiyo siku nakuwa sina hamu kabisa na mwenzangu...
 
Last edited by a moderator:
Pasco kuna kitabu niliwahi kukisoma zamani na kujaribu kupractise nikawa naona kama inakuwa kweli.ni vitu vya kawaida ila ni rahisi kutokuvifanya kwa kujisahau
Inahitajika kuupa ubongo chakula chake kikuu ambacho ni oxygen then utaongeza thinking capacity against mambo yanayokuzunguka.
Namna ya kulala,Kujenga imani,kupata utulivu wa rangi na fresh flowers vyote hufungua milango ya nguvu hizi
Pia kutoa kiasi ya ulichonacho kws wahitaji hukuongezea,hii niliijaribu nikiwa chuo na ika-work out siku hiyo hiyo.kwa kifupi huwezi kupata zaidi kama hutumii(refer Bill Gates)
Mtu anayepractise njia hizi ile kumtazama tumgonjwa anaweza kujua kama atapona au la..bila kujali muonekano wake wa nje
Hakika nilifikia mahali nikasema ukiacha bible that was my second favourite book...

jina la kitabu na muandishi tafadhali!
 
jina la kitabu tafadhali
 
Mkuu pasco, unanifanya naconcentrate kupita kiasi.

Mimi kuna wakati naamini kuwa sisi (binadamu) ni miungu pia, kwa sababu katika kitabu cha Mwanzo kinaelezea kuwa tumeumbwa kwa mfano wa mungu (from this point we ar just a copy) then if yo go to Luke chapter 17 smthing like 21st vers anasema "and thy kingdom of God is within you"

Na ukifuatilia mazungumzo ya Yesu as u ve be tryn to show us alikuwa anademand "Imani" ilifika mahali akasema kama ukiwa na imani hata kama chembe ya haradani unaweza kuambia huu mlima ung'oke ukajitose katika kilindi cha bahari.

Huwa nataka nijue ni vitu gani hasa vinaweza kukufanya imani yako ikakua??
Mkuu Six, sisi tumeumbwa kwa mfano wake na tumepewa uwezo wake, tatizo ni jinsi tuu ya kuutumia!.

Mungu alipoweka lile " tunda" la mti wa "katikati", alilita "mti wa Mema na Mabaya", shetani alipomrubini Eva, alimwambia "ukila" utafunguliwa kujua "mema na mabaya" na utakuwa na uwezo kama wa Mungu!, ikiwemo "uumbaji!".
Mungu ni omnipresent, yuko popote ikiwemo yumo ndani mwetu, ila na sherani pia ni vivyo hivyo!. Nguvu zote tunazo, na Mungu na za shetani pia, zote zimo ndani yetu!, its up to you, ufungue milango ya nguvu zipi na uzitumieje kwa manufaa gani!?.
Niliwahi kuzungumza na Askofu Mkuu, Zakaria Kakobe, nikakuta "the man has powers!, nilichoshindwa ku establish by thenm ni jee hizo "powers ni za Mungu au?" by that time nilikuwa bado sipata insight nzuri. Pia nilizungumza na Mchungaji Getrude Rwakatare pia na Mchungaji Antony Lusekelo, by then tayari niliishaanza kupata insight. naomba maeneo mengine nisiweke opinion zangu nisije nikahukumu na kuja kuhumiwa!, but all amd all, its all "work of powers" be it evil or Divine, it is "powers", na matokea ndio determinant ya powers hizo ni za nani!.
Pasco.
 
Mkuu Slow, Mungu alipomuumba Adam, alimpa uwezo!. Yesu alipokuja alifanya miujiza, na kila muujiza alisema "imani yako ndiyo imekuponya!", kasome Marko 10 : 52 - Yesu akamwambia, \"Nenda, imani yako imekuponya, na Mathayo 9:22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu;imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile, au [h=3]Luka 17:19 "[/h]Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya..hiyo imani yako ndio "powers from within!". Akasema laiti watu wangekuwa na imani kama punje ya haradali, wangeiambia milima ondoka!, na milima ikahama!", ina maana hizi imani tunazotumia ni ndogo tuu kama mbegu ya mchicha!.

Shetani pia ana powers, ikumbuke hapo mwanzo shetani ndiye aliyekuwa malaika mkuu, alipoasi, alifukuzwa ila hakunyang'anwa zile powers, ndiye aliyemrubuni Eva kule lile "tunda!". Nguvu za shetani hufanya maovu, nazo pia zimo ndani yetu kama hizo nguvu za Mungu!.

Kitendo cha kuamini, ni kufungua tuu milango. Mimi ni Mkristu Mkatoliki, kwa sababu nimezaliwa huku. Wengi hufuata imani fulani kwa kujikuta ndiko walikozaliwa na wanaendelea kujifungia humo humo kwa kuto look beyond!. Nilipokuwa India, nikasoma kidogo imani za Hindu ndipo nikagundua kumbe Christianity ni dini ya juzu juzi tuu, kwa taarifa tuu, dini za kale zaidi ni shamanism na animism, ambazo zilikuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu ila baadae zilifutika!. Kwa sasa dini ya kale zaidi iliyopo ni Hinduism ikifuatiwa na Buddhism zote za India ndipo ikaja Judaism ya Mashariki ya Kati, Israel, ikaja Taoism ya China na Shitoism ya Japan ndipo ikaja Christianity!. Hapo dini zetu za asili, hazitajiwi kabisa kwa sababu hazikuandikwa!.

Uki take time kutoka nje ya box la Ukristu au Uislamu ambamo ndiomo wengi wetu tumejifungia humo, ukachungulia ndani ya Hinduism au Buddhism, ndiko utakutana na real powers za "enlightenment!", kwa sababu dini hizi zinaamini kwenye "higher powers" bila kumtaja Mungu, Ukristu na Uislamu umezifungia milango, ili ukifuatilia uthabiti wa imani, discpline, na nguvu za kusali, utagundua sisi Wakristu na Waislamu tunatania tuu!.

Kiukweli ukizama sana kwenye hizi powers, unaweza kuingia kanisani na kujikuta unashutukia jinsi watu wanavyofungwa kamba, unaweza ukaacha kwenda!. Mimi bado ni Mkatoliki Die hard japo kuna mambo tunafanya ndivyo sivyo, ukishayangundua, unaachana nayo, bali unaendelea kuenenda kanisani kwa kufuata mafundisho ya Biblia na sio lazima yale yote ya kanisa ambayo umeisha yastukia kuwa sio!.

Wengi wakistuka, huamia makanisa ya wakovu, huko pia huwa nina hudhuria Mama yangu ni Esemblies og God, huko nako ndiko sio tuu unakuta kamba nene, bali watu wanapurushwa na kukamuliwa mpaka wanabaki mifupa!. Wale Wachungaji wameishajistukia jinsi ya kutumia hizi powers kucontrol waumini wao!. Wale wanaopataga mwanga hustuka na kujihamia kimya kimya, wengine wenye imani upofu, ni watumwa wa Wachungaji wao na wachungaji hao huwafanya lolote ikiwemo kuwa nani hii wake zao!, wao wakijua ndio baraka zenyewe kumhudumia mtumishi wa Mungu!.

Bwana wetu Yesu Krisu alisema wazi, watakuja watu, watahubiri kwa jina langu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!. Ukifuatilia sana the working of powers, unaweza kuogopa kuendelea ku practice, ila ukiisoma vizuri Bibilia, utagundua mahali mengi pameandikwa "nguvu imo ndani yako"!. Mungu alituumba kwa mfano wake, na katupa nguvu ambazo ndizo hizo powers from "within".
Pasco.

Ki ukweli Pasco yote unayosema ni halisia kabisa. Mfano, mimi huwa kuna mambo ambayo nayatamani sana na nikiyawaza kwamba ni lazima ntayapata kwa kweli huwa nayapata. Huwa nashindwa kujua ntayapata vipi, wakati gani au kwa namna gani lakini huwa mwishowe nayapata. Hata hilo la wasichana kwa mfano, naweza muona msichana say tuko bar au mahali popote nikamfeel basi nikisema niconcentrate kumwangalia yanilazima atageuka tu na tukigongana nae macho basi kama yuko na jamaa yake utamwona hata utulivu unabadilika na kujifanya anaangalia huku na huko ili mradi tu apitishe macho na kuniangalia. Basi inafika wakati najisemea hebu niache kuendelea kumwangalia sana as naona kabisa hali imechange kwake.
Kiukweli hizi nguvu watu wengi tunazo tatizo ni how to realize if we have those powers.
Mimi huogopa kwa kweli kuingia deep katika haya mambo kwa sababu huwa yanaogopesha sana. Wakati mwingine yanakuwa kama yanakinzana na Imani tulizolelewa nazo.
Big up kwako Pasco na wadau wengine wenye nia na hii elimu ya ufahamu. Mimi naitumia selectively kwa mambo machache.
Huwa nasoma vitabu vya mind & psychology na kugundua mambo mengi sana.
 
Wana Jf wenzangu, Chonde, chonde, chonde. naomba naomba sana, sana, sana, mtu ye yote asijaribu kufanya meditation ya aina yo yote ile bila chini ya uangalizi wa mwalimu, ama mtu aliebobea kwenye elimu hiyo. Mimi kwa mara ya kwanza nilifahamu kuhusu meditation mwaka wa 1973, kupitia vitabu vya Tibetan Lama mmoja aitwae Tuesday Lobsang Rampa ambaye nae alikuwa na mwalimu wake aliyeitwa Lama Mingya Dondap. Huyu bwana alikuwa akisisitiza kuwa na mwalimu katika njia hii, kama vile unapokuwa na mwalimu katika masomo ya kawaida darasani. Nilijaribu kufanya meditation bila ya kuwa na mwalimu, lakini nikaacha baada ya kuona kuwa energy ilikuwa ikinizidi na sikujua jinsi ya kui-channel katika mwili wangu. Kwa kuwa nilikuwa na ari kubwa ya kutaka kuijua elimu hii, nilijisomea vitabu mbalimbali vya kuhusu astrology, palmistry, ambapo naweza kusema nime-master sana elimu hii, vile vile kuhusu mambo mengi sana ambayo siwezi kuyaandika yote hapa. Ni sheria ya maumbile kuwa, " when the student is ready, the teacher will come " Mwaka wa 1981, nilipata mwalimu na hadi hii leo naendelea kufanya meditation katika kiwango cha juu kabisa. Ninao watoto wanne, na watatu ni ' Initiates ' na wanafanya meditation ya juu, ambapo walianza tangu wakiwa na umri wa miaka mitano. Meditation ni way of life ili kuweza kutimiza lengo la kuwepo hapa duniani. Meditation siyo dini wala imani yo yote, kwa kuwa ni practical. Meditation ziko za aina nyingi sana, lakini ipo inayoweza kukupeleka katika ngazi ya juu sana na ukafahamu mambo ya ajabu kabisa, kwa wewe kuingia ndani yako kupitia katika jicho lako la tatu. Siwezi kueleza zaidi maana sipendi kuwakwaza kwani sheria zinasema ' know and be humble '. Kwa anaependa kwa dhati, naweza kumuunganisha na " The Path " ama Sant Mat " ambazo zote zipo hapa Tzania na ninaweza kuzi-recommend kabisa. Haya kazi kwenu! 0786-961-542.
Mkuu Quuen Matara, nakuunga mkono 100% kuwa usifanye haya mambo bila kuwa guided, mimi sijawahi kufundishwa wala kupata mwalimu yoyote, zaidi ya kusoma tuu vitabu na ku practice!, hiyo statement ya "when a student is ready the teacher will apper" niliisoma kwa Linda Goodmans "Star Signs". Nlijisomea kufikia stages za "Out of body" kuanza kufanya "astral travel" ila moyo ulisita!.

Mwaka jana niliwakaribisha watu humu kwenye chuo cha meditation kilichopo pale Upanga nyuma ya Boy Scout na nikaweka uzi humu, Mafunzo ya Meditation Bure. Ni Kupitia Brahima ... - JamiiForums
Pasco.
 
Pasco
...mathalan
unagundua baadhi ya
watu waliokuzunguka
wako kinyume na
wewe!, au kuna hiyo siku
wife alitoka party ya
kazini, sixth sense
imekuambia mwenzako
"tayari" ili kukuzuga,
ajajifanya yuko "high!"
akihitaji huduma!. "Mzee"
aligoma! lakini
aliamshwa!, na kwenye
"game" ilibidi ajitahidi
sana na ku fake "kufika"
mapema kuliko
kawaida!. Kupitia
mazoezi hayo, unaweza
kudistinguish "kufika"
kweli na "kufika" fake ili
kunizunga!.
Unakuja ile genuine trust,
love na happyness
inayeyuka kwa kujua you
are cheated!...

...dah!...hapa kwa 'wife' nikama umeunitonesha kidonda,ilishawai kuntokea na kila nikiikumbuka hiyo siku nakuwa sina hamu kabisa na mwenzangu...
Sabu, ndio maana unashauriwa kabla hujakabidhiwa powers zote lazima uwe guided with moderations namna ya kutumia hizo powers. Kuna wana wanazo powers za Remote viewing sio tuu unahisi bali unaona, na tena unaweza kabisa kuwa na Astral projection ukatoka kabisa out of body na kwenda kushuhudia jimsi wife wako anavyomegwa!, tena angalau ingekuwa anamegwa kawaida tuu, unaweza kukuta mwenzio anagaiwa "kule!". Sheria ya usiri "kiapo" kinakukataza kata kata usithubutu kuuliza, wala usijulishe unajua kitu!, unatakiwa akirudi, usimchenjie kwa lolote na kuendelea kuishi nae kikawaida!, utakachotakiwa kufanya ni kumtofuta tuu huyo mwizi wako na kumweleza kistaarabu, bila kumjulisha unajua na umeona, bali unamwambia tuu, "acha uhusiano usiofaa na mke wangu!", bila kupa chance kuuliza umejuaje!. Kama kawaida atajifanya kushutuka na kushangaa huku akikanusha!, mwanzo atadhania ni mkeo ameconfess, watakutana na kuulizana mke atakapothibisha hajaconfess na wewe hujamuuliza!, tabio hiyo itakoma!, na wakiendelea kwa kujifanya ni siri!, hapo ndipo works of power itakapowashukia, yatawakuta ya kuwakuta!.
Pasco.
 
Mkuu endeleza kusuhu aura...tayari tumeshapractice zile picha na matokeo yameonekana!
Ule kama unaouona mwanga mwanga ndio aura, kitendo tuu cha kuweza kuona, ni ushahidi tosha kuwa unazo hizo powers, kinachoona ule mwanga sio sense za sight bali sixth sense iliyo yuma ya jicho. Baada ya kuuona huo mwanga sasa unahitaji mafunzo ya concentration ili uweze kuona aura za watu na items mbalimbali na pia kupata mafunzo ya jinsi ya kuzitafsiri rangi mbalimbali unazoziona kwenye aura.

Mimi niliishia hapo, ili nikikutana na mtu mwenye nia mbaya, machale hunicheza, hata akija na zawadi ya kuzugia. Watoto wachanga wanaona vizuri kabisa aura, akija mtu mbaya, utaona mtoto analia sana na hataki kumshika!.
Ukishamiona mtu kuwa sio mzuri, iulize nafsi yako "is it true!: nafsi itakuambia na ukibisha, utakuja kuushuhudua ubaya wa mtu huyo sooner or letter!, kitu kibaya sometimes unaweza kukuta mbaya wako kwenye ndoa yako ni mama yako mzazi au mbaya wa maendeleo yako ni mkeo!.Mambo mengine yataka moyo!.

Pasco.
 
Pasco kuna kitabu niliwahi kukisoma zamani na kujaribu kupractise nikawa naona kama inakuwa kweli.ni vitu vya kawaida ila ni rahisi kutokuvifanya kwa kujisahau
Inahitajika kuupa ubongo chakula chake kikuu ambacho ni oxygen then utaongeza thinking capacity against mambo yanayokuzunguka.
Namna ya kulala,Kujenga imani,kupata utulivu wa rangi na fresh flowers vyote hufungua milango ya nguvu hizi
Pia kutoa kiasi ya ulichonacho kws wahitaji hukuongezea,hii niliijaribu nikiwa chuo na ika-work out siku hiyo hiyo.kwa kifupi huwezi kupata zaidi kama hutumii(refer Bill Gates)
Mtu anayepractise njia hizi ile kumtazama tumgonjwa anaweza kujua kama atapona au la..bila kujali muonekano wake wa nje
Hakika nilifikia mahali nikasema ukiacha bible that was my second favourite book...

Mkuu kinaitwaje hiko kitabu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom