Mkuu Bona, hili ni swali la msingi sana, kuna wanaojua sana dini humu, lakini hawajibu!. Ukijibu wanakuja juu!.
Sambamba na swali hili, dini zote hawaruhusiwi kuuliza Mungu ni Nani?, wala kuuliza mwanzo wake!, wala hawaulizi Roho Mtakatifu ni nani, wala hawaulizi mwanzo wake!.
Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulikuwepo na Powers, hizo powers ndizo Mungu. Hana mwanzo, hana mwisho, yeye ni Alfa na Omega!.
Huyu Mungu alikuwa na wasaidizi, waitwao Malaika, kati ya malaika hawa, malaika Mkuu kabisa kuliko wote, mwenye madaraka makubwa karibu kabisa na Mungu, aliitwa Luciferi. Huyu alikuwa na karibu nguvu zote sawa na Mungu, ila alikosa nguvu mbili tuu, Uumbaji, na Utoaji Roho!. Yaani Lucifer kama malaika Mkuu, alikuwa na uwezo wa kufanya kila Mungu anachofanya, isipokuwa hakuwa na uwezo wa kuumba, wala kutoa roho!. Malaika wa tatu kwa ukuu aliitwa Gabriel!, wa nne Mikaeli, malaika wote waliobakia hawakutajwa kwa majina!.
Hakuna mahali popote palipoelezwa Mungu aliwaumba hawa malaika akiwemo Luciferi!. Hivyo mwanza wa Mungu ndio mwanzo wa Malaika!.
Malaika huyu Mkuu, Lusiferi, akaendesha uasi mbinguni kwa kuandaa jeshi la malaika kutaka kuyatwaa madaraka ya Mungu, baadhi ya malaika ambao ni watiifu kwa Mungu wakiongozwa na Gabrieli, hawakukubali kuasi!. Vikapiganwa vita kati ya jeshi la Mungu na jeshi la Luciferi, jeshi la Lusiferi likashindwa, hivyo ndivyo Lusiferi akapewa jina la shetani!, akatupwa duniani kuja kutafuta wafuasi!. Haikuelezwa popote kama alinyanganywa hizo nguvu!.
Shetani aliumbwa kama malaika mtakatifu (haikusema aliumbwa na nani), Isaya 14:12 inampa Shetani jina kabla aanguke kuwa nyota ya alfajiri. Ezekieli 28:12-14 inamwelezea Shetani kuwa, aliumbwa awe kerubi, kawaida malaika mkuu. Aligeuka na kuwa mkali kwa ajili ya urembo wake na cheo chake na akaamua kuwa aketi kwenye kiti kilicho juu ya Mungu (Isaya 14:13-14; Ezekieli 28:15; 1 Timotheo 3:6). Kiburi cha Shetani kilimfanya aanguke. Kumbuka usemi wa wengi nita katika Isaya 14:12-15. Kwa sababu ya dhambi zake, Mungu alimfukuza Shetani kutoka mbinguni na kumtupa duniani!.
Shetani akawa kiongozi wa ulimwengu na mfalme wa anga (Yohana 12:31; 1 Wathesalonike 3:5), na mwongo (Mwanzo 3; 2 Wakorintho 4:4; Ufunuo Wa Yohana 20:3). Jina lake linamaanisha Mwenye majanga au mpingamizi. Majina yake mengine ni, Ibilisi kumaanisha mdanganyaji.
Hata kama alifukuzwa kutoka mbinguni, bado anazidi kujinua kiti chake juu ya Mungu. Anayageuza yale Mungu anayafanya, akitumaini kuabudiwa na ulimwengu na anatia tumaini kwa pingamizi zote za ufalme wa Mungu. Shetani ndiye ako nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia akijipretend ni Mungu!. Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimeweka sheria zote na jinsi ya kuabudu!. Kuna dini nyingi duniani zinamwabidu shetani bila masikini waumini kujua!. Ukijisomea Bibilia Takatifu, huku umetulia, utafunuliwa tuu na kuijua kweli, hivyo kama uu miongoni mwa waabudu shetani bila kujijua, utafunguka na unaweza kuamua kubadilika, au kuendelea kuabudia nyumba za Ibada zile zile, huku moyoni mwako unamwabudu Mungu wa Kweli!.
Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano wake, akatupulizia pumzi ya uzima ambayo ndio source ya hizi nguvu tulizo nazo za kutenda mema, na miujiza na kutenda kila kitu!. Kwa vile shetani naye yuko duniani, naye ananguvu na kufanya kila kitu, ila kwa lengo la kupoteza wana wa Mungu!. Kuna wakati huwa anazungumza hata na Mungu kabla ua kuleta majanga na huwa anapata kibali cha kufanya hayo majanga mfano ni kwa Ayubu!.
Hata Yesu alipokuja duniani, kuna wakati Shetani alimjaribu.
Katika nguvu tulizopewa na Mungu, pia tumepewa uwezo wa kujitambua na kuzitambua hilo zote za shetani. Bila kuwa na uwezo huu, unaweza kabisa kujidhania unamwabudu Mungu wa kweli, kumbe sivyo, bali unamwabudu shetani, ibilisi na mwisho wa siku, utateketezwa nae kwenye jehanum ya milele!.
Kwa vile Mungu ni onmipresence, vivyo hivyo shetani naye ni omni present!, binadamu wote ambao hutenda mema, hutumia nguvu za Mungu, na wote watendao maovu hutumia nguvu za shetani!. The dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za shetani is very thin!, the only diference ni Nguvu za Mungu ni freely na unconditional, hazina masheri yoyote zaidi ya kuamini tuu!. Nguvu za shetani ni conditional, kwamba uli zipate lazima ufanye hiki, na kile!.
Mafunzo ninayoyatoa humu ni free, freely na unconditional, na nguvu hizo wote tunazo ila tuu hatujaziamsha!. Usikute hata hizi juhudi zinazoendelea humu watu kuogopa zisifunuliwe, inaweza kabisa kuwa ni kazi ya shetani, nawahakikishia zitashindwa!, watu watafunuliwa na watatenda miujiza!.
Pasco.