Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Halafu mi nauliza! Vipi huyu Pasco ajiite mkristo hali ya kuwa anamlinganisha yesu na mchawi??

Hii si laana hii?? Anasema yeye ni mkatoliki!
Hivi ndivyo wanavyofunzwa na papa!?

Kumfanya nabii wa Mungu kama shemeji yako??

Ama.mtoto wewe huna adabu!

Laiti ningemjua baba Pasco ! Ningeenda mchapa kofi kwa kutokufundisha nidhamu!
Yaani mi nilidhani Nicholas na Matola ndio hawana adabu lkn wewe mwisho!

Mfnssssssssssss!
Mkuu hao wawili Nicholas na Matola ni majuhalaa wanachukisana na uislamu lakini mimi nawaambia wame:frusty:
 
Una tatizo la kusoma na ukaelewa

Mkuu Nyenyere anakuambia kuwa kitendo chako cha kumtaja Kisto na kulinganisha nguvu zake na za wachawi pia kuitaja biblia moja kwa moja

Hapo ndipo tatizo lilipoanzia na ni hapo sisi tukaja kukukosoa na kuonesha nma ulivyokosea

Unadai kuwa unafundisha kuhusiana na power ambazo hata husemi zinatoka wapi,lakini ulishindwa nini kufundisha hizo power zako bila kuwataja Roho mtakatifu,Yesu na biblia?
Ulishindwa nini kujenga hoja kivyako?
Au ulikuwa unatafuta tention kutoka kwa wasomaji?

Hizo meditationa unazodai zipo miaka mingi na sijui kitu gani,sisi hatuna tatizo na hilo, tatizo linakuja pale ulipotamka Roho mtakatifu na Yesu pamoja na biblia.Ungekuwa umesema tu Mungu kusingekuwa na tatizo maana kuna wengi wanaabudu mawe na wanayaita Mungu,hata Hsetani nae anaitwa hivyo na wafuasi wake na tusingekuwa na tatizo

Tatizo linakuja kwenye mambo mawili,Biblia na Roho mtakatifu
Hao huwezi kuwapata kwenye imani yoyote ile tofauti na biblia,kwenye Yesu wapo watu wengine wana yesu wao lakini ulipoitaja biblia hiyo inamaana kuwa unamtaja Yesu wa kwenye biblia na ndipo tulipata jukumu la kukukosoa na mafundisho yako ya kishetani[samahani kwa kutumia lugha kali] na tumekuonesha ni namna gani ni ya kishetani

Mtu unasema shetani hakuumbwa na Mungu na hana mwanzo wala mwisho.unadhani hayo sio mafundisho ya kishetani na ni kwanini usiitwe mpinga Kristo?

Halafu hao wengine unaodai tunawaingilia sijui ni wakina nani,ni nani anamwabudu Roho mtakatifu tofauti na wakristo?Ni nani anamwabudu Yesu Kristo wa Biblia tofauti na wakristo?
Hao wengine unaodai ni wakina nani?

Suala hili la hizi power tunakushauri u edit mada yako iwe huru ili wote wanaochangia wasichangie wa mitazamo ya kidini
Kama ni kosa limefanywa kwa watu kuchangia kwa mtazamo wa kidini kosa hilo umelianzisha wewe mwenyewe kwenye post yako

Tafadhali sana Invisible hebu fanyeni haki kwetu yunaemwabudu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu!

Mkuu Eiyer, umemueleza vitu va msingi ingawa lengo lake ni kupingana na Ukristo na kuingiza hayo mafundisho machafu!

Nimekua nasoma huu Uzi bila kuchangia lolote. Lakini na Mimi ningependa kusisitiza kua kwenye Mada hii atoe bible na Roho mtakatifu then aendelee na mambo yake!
 
Last edited by a moderator:
Watu wasiokuwa na adabu hilo pia haliwatoshi.
Hao wamelaaniwa kabisa! Tena haifai kuwa hata jirani yako
Laana inaweza kukuangukia na wewe!

Sijui kama hili ni fundisho kwenye imani yenu,lakini usichokijua ni kwamba hata kama mtu hana adabu bado anastahili heshima
Na sijui atakuwa amelaaniwa na nani,maana kama haamini kwenye imani yako huna mamlaka ya kumuita hivyo
Nani amekuambia laana inawaangukia watu kirahisi hivyo?
 
huna haja ya kuw na imani Fulani Ili laana ikupate! we hujaskia mpagani pia analaanika??

Na hio sharia au kauli ya kusema asiye na adabu pia aheshimiwe umeitoa wapi??

manake nyie kwa kuzua vitu ni watu wabaya sana kwa hilo,

kama ni hivyo! kwa nini BIBLE IMLAANI NA KUMUHUKUMU ASIE NA ADABU?? AU wewe na biblia nani anaejua zaidi!!
 
Halafu mi nauliza! Vipi huyu Pasco ajiite mkristo hali ya kuwa anamlinganisha yesu na mchawi??

Hii si laana hii?? Anasema yeye ni mkatoliki!
Hivi ndivyo wanavyofunzwa na papa!?

Kumfanya nabii wa Mungu kama shemeji yako??

Ama.mtoto wewe huna adabu!

Laiti ningemjua baba Pasco ! Ningeenda mchapa kofi kwa kutokufundisha nidhamu!
Yaani mi nilidhani Nicholas na Matola ndio hawana adabu lkn wewe mwisho!

Mfnssssssssssss!

umenichekesha sana kwa kweli.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Pasco anasema hizi ni power from within pasipo kusema what are the source of this power, kwa uelewa wangu kama ni nguvu kutoka ndani haziwezi ni nguvu zilizojiweka zenyewe lazima zimewekwa for the purpose, na nani kaziweka kama si creator? the one who created the man is the one who put those power inside human being, kwa hiyo vyovyote utakavyo amini lakini ujue aliyemuumba mwanadamu ndiye aliyeweka Nguvu ndani yake.
mniwie radhi nnachangia nikiwa nimeweka kilaji.
 
Last edited by a moderator:
shetani ni nani?
Mkuu Bona, hili ni swali la msingi sana, kuna wanaojua sana dini humu, lakini hawajibu!. Ukijibu wanakuja juu!.

Sambamba na swali hili, dini zote hawaruhusiwi kuuliza Mungu ni Nani?, wala kuuliza mwanzo wake!, wala hawaulizi Roho Mtakatifu ni nani, wala hawaulizi mwanzo wake!.

Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulikuwepo na Powers, hizo powers ndizo Mungu. Hana mwanzo, hana mwisho, yeye ni Alfa na Omega!.

Huyu Mungu alikuwa na wasaidizi, waitwao Malaika, kati ya malaika hawa, malaika Mkuu kabisa kuliko wote, mwenye madaraka makubwa karibu kabisa na Mungu, aliitwa Luciferi. Huyu alikuwa na karibu nguvu zote sawa na Mungu, ila alikosa nguvu mbili tuu, Uumbaji, na Utoaji Roho!. Yaani Lucifer kama malaika Mkuu, alikuwa na uwezo wa kufanya kila Mungu anachofanya, isipokuwa hakuwa na uwezo wa kuumba, wala kutoa roho!. Malaika wa tatu kwa ukuu aliitwa Gabriel!, wa nne Mikaeli, malaika wote waliobakia hawakutajwa kwa majina!.

Hakuna mahali popote palipoelezwa Mungu aliwaumba hawa malaika akiwemo Luciferi!. Hivyo mwanza wa Mungu ndio mwanzo wa Malaika!.

Malaika huyu Mkuu, Lusiferi, akaendesha uasi mbinguni kwa kuandaa jeshi la malaika kutaka kuyatwaa madaraka ya Mungu, baadhi ya malaika ambao ni watiifu kwa Mungu wakiongozwa na Gabrieli, hawakukubali kuasi!. Vikapiganwa vita kati ya jeshi la Mungu na jeshi la Luciferi, jeshi la Lusiferi likashindwa, hivyo ndivyo Lusiferi akapewa jina la shetani!, akatupwa duniani kuja kutafuta wafuasi!. Haikuelezwa popote kama alinyanganywa hizo nguvu!.

Shetani aliumbwa kama malaika mtakatifu (haikusema aliumbwa na nani), Isaya 14:12 inampa Shetani jina kabla aanguke kuwa nyota ya alfajiri. Ezekieli 28:12-14 inamwelezea Shetani kuwa, aliumbwa awe kerubi, kawaida malaika mkuu. Aligeuka na kuwa mkali kwa ajili ya urembo wake na cheo chake na akaamua kuwa aketi kwenye kiti kilicho juu ya Mungu (Isaya 14:13-14; Ezekieli 28:15; 1 Timotheo 3:6). Kiburi cha Shetani kilimfanya aanguke. Kumbuka usemi wa wengi “nita” katika Isaya 14:12-15. Kwa sababu ya dhambi zake, Mungu alimfukuza Shetani kutoka mbinguni na kumtupa duniani!.

Shetani akawa kiongozi wa ulimwengu na mfalme wa anga (Yohana 12:31; 1 Wathesalonike 3:5), na mwongo (Mwanzo 3; 2 Wakorintho 4:4; Ufunuo Wa Yohana 20:3). Jina lake linamaanisha Mwenye “majanga” au “mpingamizi.” Majina yake mengine ni, Ibilisi kumaanisha “mdanganyaji.”

Hata kama alifukuzwa kutoka mbinguni, bado anazidi kujinua kiti chake juu ya Mungu. Anayageuza yale Mungu anayafanya, akitumaini kuabudiwa na ulimwengu na anatia tumaini kwa pingamizi zote za ufalme wa Mungu. Shetani ndiye ako nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia akijipretend ni Mungu!. Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).

Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimeweka sheria zote na jinsi ya kuabudu!. Kuna dini nyingi duniani zinamwabidu shetani bila masikini waumini kujua!. Ukijisomea Bibilia Takatifu, huku umetulia, utafunuliwa tuu na kuijua kweli, hivyo kama uu miongoni mwa waabudu shetani bila kujijua, utafunguka na unaweza kuamua kubadilika, au kuendelea kuabudia nyumba za Ibada zile zile, huku moyoni mwako unamwabudu Mungu wa Kweli!.

Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano wake, akatupulizia pumzi ya uzima ambayo ndio source ya hizi nguvu tulizo nazo za kutenda mema, na miujiza na kutenda kila kitu!. Kwa vile shetani naye yuko duniani, naye ananguvu na kufanya kila kitu, ila kwa lengo la kupoteza wana wa Mungu!. Kuna wakati huwa anazungumza hata na Mungu kabla ua kuleta majanga na huwa anapata kibali cha kufanya hayo majanga mfano ni kwa Ayubu!.

Hata Yesu alipokuja duniani, kuna wakati Shetani alimjaribu.
Katika nguvu tulizopewa na Mungu, pia tumepewa uwezo wa kujitambua na kuzitambua hilo zote za shetani. Bila kuwa na uwezo huu, unaweza kabisa kujidhania unamwabudu Mungu wa kweli, kumbe sivyo, bali unamwabudu shetani, ibilisi na mwisho wa siku, utateketezwa nae kwenye jehanum ya milele!.

Kwa vile Mungu ni onmipresence, vivyo hivyo shetani naye ni omni present!, binadamu wote ambao hutenda mema, hutumia nguvu za Mungu, na wote watendao maovu hutumia nguvu za shetani!. The dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za shetani is very thin!, the only diference ni Nguvu za Mungu ni freely na unconditional, hazina masheri yoyote zaidi ya kuamini tuu!. Nguvu za shetani ni conditional, kwamba uli zipate lazima ufanye hiki, na kile!.

Mafunzo ninayoyatoa humu ni free, freely na unconditional, na nguvu hizo wote tunazo ila tuu hatujaziamsha!. Usikute hata hizi juhudi zinazoendelea humu watu kuogopa zisifunuliwe, inaweza kabisa kuwa ni kazi ya shetani, nawahakikishia zitashindwa!, watu watafunuliwa na watatenda miujiza!.
Pasco.
 
mkuu Pasco anasema hizi ni power from within pasipo kusema what are the source of this power, kwa uelewa wangu kama ni nguvu kutoka ndani haziwezi ni nguvu zilizojiweka zenyewe lazima zimewekwa for the purpose, na nani kaziweka kama si creator? the one who created the man is the one who put those power inside human being, kwa hiyo vyovyote utakavyo amini lakini ujue aliyemuumba mwanadamu ndiye aliyeweka Nguvu ndani yake.
mniwie radhi nnachangia nikiwa nimeweka kilaji.
Mkuu Naibili, nimerudia time and times again, its 100 times now!, Sote Tumeumbwa na Mungu!, God!, The Creator!, alipotuumba ndipo alipotupatia nguvu hizi! aliposema "na tuumbe mtu kwa mfano wetu!". Hata Yesu alipokuja kila alipofanya miujiza, alisema "ni imani yako ndio imekuponya!".

Ugomvi wangu na Wakritu humu ni pale tuu wanapodai copyright ya nguvu Mungu ni kwa Wakristu Pekee, wengine wote wasiomwamini Yesu, ni washetani!. Nikawaeleza nguvu hizi zimekuwa zikitumika miaka 300,000 kabla ya Kristu!. Yesu amekuja miaka 2013 tuu iliyopita!, ninachofundisha humu ni kuwa hata kama wewe sio Mkristo, nguvu hizi za Mungu unazo!, hata kama wewe huna dini kabisa, ila uunaamini kuna God, the Creator, in whataver the name utatumia!, nguvu hizi utakuwa nazo!. Mungu ni jina, God ni jina, Omukama ni jina, Omulugu ni jina, Allah ni jina, kwa vile Mungu ni onmipresence, kama wewe unaamini "upepo" ndio Mungu wako, amini hivyo, ndani ya huo huo upepo, Mungu wa kweli atakuwepo na milango ya powers from within itafunguka!. Akiamini Allaah, amini hivyo, na milango itafunguka!.
Just have faith kuwa you have the powers!, zitafunguka bila masharti yoyote!.
Pasco.
 
Mkuu mayenga, mimi nina Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.

Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.

Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!

Pasco.

Mkuu hii ya kumtazama tu binti unayemtaka inamhusu hata Wassira? Maana naona Kama akiwatazama Ndo watamkimbia.
 
Una tatizo la kusoma na ukaelewa

Mkuu Nyenyere anakuambia kuwa kitendo chako cha kumtaja Kisto na kulinganisha nguvu zake na za wachawi pia kuitaja biblia moja kwa moja

Hapo ndipo tatizo lilipoanzia na ni hapo sisi tukaja kukukosoa na kuonesha nma ulivyokosea

Unadai kuwa unafundisha kuhusiana na power ambazo hata husemi zinatoka wapi,lakini ulishindwa nini kufundisha hizo power zako bila kuwataja Roho mtakatifu,Yesu na biblia?
Ulishindwa nini kujenga hoja kivyako?
Au ulikuwa unatafuta tention kutoka kwa wasomaji?

Hizo meditationa unazodai zipo miaka mingi na sijui kitu gani,sisi hatuna tatizo na hilo, tatizo linakuja pale ulipotamka Roho mtakatifu na Yesu pamoja na biblia.Ungekuwa umesema tu Mungu kusingekuwa na tatizo maana kuna wengi wanaabudu mawe na wanayaita Mungu,hata Hsetani nae anaitwa hivyo na wafuasi wake na tusingekuwa na tatizo

Tatizo linakuja kwenye mambo mawili,Biblia na Roho mtakatifu
Hao huwezi kuwapata kwenye imani yoyote ile tofauti na biblia,kwenye Yesu wapo watu wengine wana yesu wao lakini ulipoitaja biblia hiyo inamaana kuwa unamtaja Yesu wa kwenye biblia na ndipo tulipata jukumu la kukukosoa na mafundisho yako ya kishetani[samahani kwa kutumia lugha kali] na tumekuonesha ni namna gani ni ya kishetani

Mtu unasema shetani hakuumbwa na Mungu na hana mwanzo wala mwisho.unadhani hayo sio mafundisho ya kishetani na ni kwanini usiitwe mpinga Kristo?

Halafu hao wengine unaodai tunawaingilia sijui ni wakina nani,ni nani anamwabudu Roho mtakatifu tofauti na wakristo?Ni nani anamwabudu Yesu Kristo wa Biblia tofauti na wakristo?
Hao wengine unaodai ni wakina nani?

Suala hili la hizi power tunakushauri u edit mada yako iwe huru ili wote wanaochangia wasichangie wa mitazamo ya kidini
Kama ni kosa limefanywa kwa watu kuchangia kwa mtazamo wa kidini kosa hilo umelianzisha wewe mwenyewe kwenye post yako

Tafadhali sana Invisible hebu fanyeni haki kwetu yunaemwabudu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu!
Mkuu Eiyer, nakuomba sana usilazimishe mambo!, hapa sio nyumba ya ibada!, naomba tufanye appontment kule jukwaa la dini, nikupige somo!, usijekujikuta na wewe ndio hao wamuabidia shetani aliyejidisguised kama Mungu, ndio maana unababaika sana!. Issue ya shetani aliumbwa na nani usiifanye a very big deal!, nilikuuliza huko nyuma, jee unaujua mwanzo wa Mungu?!, jee unaijua source of powers za Mungu?!, Jee unaujua mwanzo wa shetani?!, kama ulifundishwa kuwa shetani aliumbwa na Mungu, na ndiye aliyempa hizo nguvu za kushetani tufuindishi na sisi tujue!. Nilikuuliza baada ya shetani kuasi kule kwa Mbinguni, jee unajua ni kwa nini Mungu hakumuangamiza?!. Jee unajua Mungu alituumba sisi binadamu kwa mfano wake?!, jee huyo shetani baada ya kumdanganya mama Yetu Eva na kumshawishi kumuasi Mungu!, unajua alifanywa nini?!. Baada ya Kaini mtoto wa kwanza wa Eva, kumuua ndugu yake Abeli, unajua alifanywa nini?!.

Kwa maana hiyo jinsi Mungu aliupenda ulimwengu, hadi akamtoa mwanaye mpendwa wake anayependezwa naye kuja kuuokoa ulimwengu from what!, yaani huyu shetani ni nani haswa hadi Mungu kumtoa kafara mwanaye?!, kwa nini asingemuangamiza shetani na yote yakaisha!.

Nakushauri kwa mambo usiyoyajua ukidhani unajua, bora jikalie kimya, acha watu tufungulie watu milango ya kumtambua shetani na kumuepuka!, huku tukiwaacha watu mliojifungia katika box la shetani, akiwaaminisha yeye ndio Mungu, huku mkiamini!, bila kuwa elightened!, utajikuta unamtumikia shetani bila kujijua!.
Sio lazima kuchangia, fuatilia tuu uzi huu ukifunguka, utakuja kunishukuru nimekuokoa!.
Kipimo cha kwanza kwa wanaomwabudu shetani bila kujijua, Yesu wa ukweli akitajwa, watataka kukuzuia usimtaje!. Huyo Roho Mtakatifu mnaotaka kuzuia tusimtaje ndio hizo powers zenyewe na kufanya kila kitu!, neno Roho Mtakatifu likiwa ni jina tuu, the essence is powers!.
Nitamtaja Mungu!, Nitamtaja Yesu, Nitamtaja Roho Mtakatifu kwa ajili ya wale waaminio, na kwa kwa wasio waaminia, nitawaruhusu kuitumia imani yoyote wanayoiamini kuifungua milango ya "powers from within!".
Pasco!.
 
Mkuu hii ya kumtazama tu binti unayemtaka inamhusu hata Wassira? Maana naona Kama akiwatazama Ndo watamkimbia.
Mkuu Mdakuzi, amini nakuambia, huyu jamaa mabinti wanamgombania!. Ili pia kiukweli, Wasira is very humane!, nikiwa nchini India, alikuja kunitembelea mahali, he is a very good and very kind man!. Kwenye ulimwengu wa roho, hatuangalii mwili, tunaangalia roho tuu!. Njia ya motoni ni pama imepandwa maua!, njia ya mbinguni ni nyembamba, imejaa miiba!. Penye urembo ndipo penye ulimbo!.

Ila fanya experiment kidogo, wanawake wabaya kwa sura, kule ni balaa!, na wanawake wazuri sana, na warembo kama nanii... hakuna kitu!, ndio maana unashuhudia watu wanakuja, wanamega, wanapita!. The same applies kwa sura za kiume!, wale ma HB sana, utakuta ndio hivyo tena!!. wenye sura mbaya, warembo wanapigana vikumbo!.

Pasco.
 
huna haja ya kuw na imani Fulani Ili laana ikupate! we hujaskia mpagani pia analaanika??
Nani amesema hili?
Mimi nilikuuliza kama imani yenu inawafundisha hivyo,sikumaanisha kuwa ili upate laana inabidi uwe na imani fulani
Tafadhali soma uelewe kisha ujibu
Na hio sharia au kauli ya kusema asiye na adabu pia aheshimiwe umeitoa wapi??
Unaona tatizo lako/
Unawaza kisahria sharia tu,Hakuna kufikiri
Yaani wewe chochote kile kinaamuliwa na sheria hata kama sharia hiyo ni ya hovyo
Kisipokuwepo kwenye sharia unabaki mtupu

Halafu ni kwanini unafikiri kila nitakacho andika hapa natakiwa nikitoe mahali?
Hili ni tatizo la kuwa mfuasi wa kitu au mtu fulani bila kutumia akili yako kufikiri

Binadamu tuna maadili tunayotumia kuamua mambo,chochote kinachokwenda kinyume na maadili hayo hata kama kimeandikwa wapi tunakikataa,kama wewe unafuata mambo ki upofu upofu hilo ni tatizo lako
manake nyie kwa kuzua vitu ni watu wabaya sana kwa hilo,
Nyie akina nani?
Ni mambo gani yamezuliwa na hao "nyie"?
Na wana ubaya gani?
kama ni hivyo!
Ni hivyo nini?
kwa nini BIBLE IMLAANI NA KUMUHUKUMU ASIE NA ADABU?? AU wewe na biblia nani anaejua zaidi!!
Sitaki kuizungumzia biblia kwenye hili wala kitabu chochote kile cha kiimani,tulizungumze hili sisi kama binadamu tu
Tutumie maadili ya kibinadamu tu kuliamua hili halafu tuone kama utakuwa sahihi

Hakuna binadamu anaepoteza haki ya kuheshimiwa kwa kufanya chochote kile!
 
Kwa maana hiyo jinsi Mungu aliupenda ulimwengu, hadi akamtoa mwanaye mpendwa wake anayependezwa naye kuja kuuokoa ulimwengu from what!, yaani huyu shetani ni nani haswa hadi Mungu kumtoa kafara mwanaye?!, kwa nini asingemuangamiza shetani na yote yakaisha!.

Pasco!.

mkuu Pasco hapo nnatumia simu ndo maana nimequote hicho kipande kidogo hapo lengo watu wasome between the line,
Ninachokiona mimi unahoji uhalali wa Nguvu za Mungu!!!
harakati unazozianzisha lengo lako unasema kama nimekuelewa vizuri ni kuonyesha kuwa kuna nguvu ya Tatu yaani badala ya ile inayotokana na shetani, na Mungu, yako unasema ni unconditional lakini kuna sehemu hapo juu unasema jina lolote utakalo amini na kutaja unazo nguvu, kama hizi nguvu ni unconditional kwa nini uamini upepo, au mlima, au nyumba au kitu chochote, kuna haja gani ya kunuia maneno, kwa mtazamo wangu hizi nguvu zina conditional
 
Mkuu Naibili, nimerudia time and times again, its 100 times now!, Sote Tumeumbwa na Mungu!, God!, The Creator!, alipotuumba ndipo alipotupatia nguvu hizi! aliposema "na tuumbe mtu kwa mfano wetu!". Hata Yesu alipokuja kila alipofanya miujiza, alisema "ni imani yako ndio imekuponya!".

Ugomvi wangu na Wakritu humu ni pale tuu wanapodai copyright ya nguvu Mungu ni kwa Wakristu Pekee, wengine wote wasiomwamini Yesu, ni washetani!. Nikawaeleza nguvu hizi zimekuwa zikitumika miaka 300,000 kabla ya Kristu!. Yesu amekuja miaka 2013 tuu iliyopita!, ninachofundisha humu ni kuwa hata kama wewe sio Mkristo, nguvu hizi za Mungu unazo!, hata kama wewe huna dini kabisa, ila uunaamini kuna God, the Creator, in whataver the name utatumia!, nguvu hizi utakuwa nazo!. Mungu ni jina, God ni jina, Omukama ni jina, Omulugu ni jina, Allah ni jina, kwa vile Mungu ni onmipresence, kama wewe unaamini "upepo" ndio Mungu wako, amini hivyo, ndani ya huo huo upepo, Mungu wa kweli atakuwepo na milango ya powers from within itafunguka!. Akiamini Allaah, amini hivyo, na milango itafunguka!.
Just have faith kuwa you have the powers!, zitafunguka bila masharti yoyote!.
Pasco.

Kwanza kabisa Yesu alikuwa akisema Imani yako imekuponya akimaanisha Imani yako kwa Mungu na sio Imani unayojiamini wewe. Wana wa_Israel wamelelewa ktk kumuamini Mungu mmoja yaani Mungu wa Isaka, Yakobo, Ibrahimu n.k hivyo wao Imani yao ilikuwa kwa Mungu aliehai ambae Yesu ametoka huko na yupo huko.
Sasa Pasco kama unavosema kuwa mwanadamu anapopuliziwa hewa yaani kuwa Nafsi hai huwa anapewa hizi. Kwanini Yesu hakutumia hizi Powers mfano kuhubir, miujiza ya kuponya na kufungua, kufufua n.k ambayo we unasema vinatokana na power anazozaliwa mtu nazo,lakini hakutenda Ishara zozote zile mpaka pale alipobatizwa kwa kupokea nguvu ya R/Mtakatifu???
 
Mkuu umeuliza maswali mazuri,
Niwaombe mods waruhusu chalenge kwa pasco na wafuasi wake tusijenge Taifa la ndio mzee
 
Back
Top Bottom