Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #661
Mkuu Ntuzu, yanayofaa na yasiofaa ni relative, yanafuata principle za relativity, mfano mimi ni Mkatoliki, mafundisho yanayofaa kwangu ni pamoja na kuvaa rozari, misalaba makanisani kwetu, siku ya Ijumaa Kuu, tunapiga magoti, tunabisu Msalaba, kanisani tunafukiza ubani, na divai kidogo tunaipiga pale madhabahuni etc!.Jibu hoja za wadau sio utuambie tuhame Huku then tukuache Wewe unaendelea na mafundisho yako yasiofaa!
Kwa mlokole alie zama deep kwenye Biblia, kwake hizo ni ibada za masanamu na kwake ni sawa na kumtumikia shetani tukifikiri ni Mungu!, mtu asiye Mkatoliki hana right ya kumwambia Mkatoliki hayo ni mafundisho yasiofaa!. Wewe just shika lako!.
Mfano sisi Wakristu tunaamini Yesu ni Mungu!, Waislamu wanaamini Mungu wao ni Allah na Mtume wake ni Muhamed (SAW), kwao Yesu sii Mungu!. Wakristu wenye imani kali wanaamini Mungu sio Allah, etc, Mkristu hana haki kumwambia Muislamu kuwa Allah sio Mungu bali ni ... na Muislamu hana haki kumwambia Mkristu Yesu sii Mungu!.
Wewe shika lako unaloamini, after all hapa jf sio nyumba ya ibada, ndio maana wameweka jukwaa maalum la hayo na ukiingia huko hakuna msalie mtume!. Tukutanie kule tumalizane, hapa tuwapishe watu wa practice powers!.
Pascal.