Humble African
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 4,781
- 14,415
Mkuu Pasco tatizo ni kwamba hizi power ukiziweka kwenye real world hili kila mtu azione zinagoma...I am sure hakuna hata psychic mmoja atakejitokeza adharani na kusema ndege iko wapi...
Asije akawa ni huyu!.Ninazo video kadhaa nitazipandisha punde hapa jamvini kuna mzee mmoja fundi anazionyesha dhairi ila mwishoni alikiri nguvu hizo kupotea baada ya yeye kudemonstrate hili watafiti wazungu wazione.
Vuta subira!! Nitapandisha mziho huo hapa punde.
Mkuu Mzizi Mkavu, hebu zama kwenye ile link ya pili kwenye thread ya mwanzo!.
Hujanipa Hatuwa ya pili kuhusu Aura mbona?
Mkuu Mzizi Mkavu, hebu zama kwenye ile link ya pili kwenye thread ya mwanzo!.
Pasco
Mkuu John Kachembeho, hiyo 1994, ulikuwa na umri gani?!.Nina Bilocation/Multilocation;
Mwezi January 1994 nilihama kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine na baadhi ya ndugu zangu, nina kumbukumbu mbili juu ya safari hiyo.
Kumbukumbu ya kwanza ni kwamba katika safari hiyo tulitembea kwa miguu na ndugu zangu mwanzo wa safari hadi mwisho, tulivuka mto pia kwa kutembea katika maji kidogo yaliyokuwa kwenye mwendo. Safari ilikuwa ndefu kwani tulianza kutembea kama saamoja asubuhi hadi mida ya saa saba mchana. Katika safari hiyo mara kwa mara nilikuwa nachoka na hivyo kupelekea ndugu zangu kunibeba mgongoni kwa kupokezana, tulifika salama siku hiyo.
kumbukumbu ya pili juu ya safari hiyo ni hii;
Ndugu zangu walitembea kwa miguu isipokuwa mimi ambaye nilibebwa kwa baiskeli na mjomba wangu hadi kule mwisho wa safari kisha yeye akarudi. Nilikaa pale kuwasubiri wenzangu waliokuwa wanasafiri kwa miguu hadi walipowasili mchana. Kwa kifupi mimi sikutembea kwa miguu wala kuvuka maji mtoni katika safari hiyo.
Kwa bahati nzuri au mbaya nilihama tena wilaya hiyo na kwenda kuishi mkoa mwingine kabisa kwa miaka mingi nikiwaacha ndugu zangu, hizo kumbukumbu mbili za safari moja zikawa zinasumbua akili yangu kadiri miaka ilivyokuwa inasonga, kwa muda mrefu sikupata mtu sahihi wa kumweleza au kumwuliza ili anipe clarification.
Miaka kama mitano baadae nilikutana na mmoja wa ndugu zangu tuliotembea pamoja ile safari, tuliongea na kukumbushia ile safari ya mwaka 1994 na nika-prove kwamba tulitembea kwa miguu. sikumweleza kwamba nakumbuka pia namna tofauti ya safari ile.
Miaka kumi badae, mwaka 2004 ulitokea msiba kule nilikohama mwaka 1994 na nikaenda kuhudhuria msiba ule (Sikuwahi kurudi kule kabla ya msiba huo), basi mara moja nikakutana na mjomba aliyenibeba kwa baiskeli katika safari ya mwaka 1994 na palepale akaanza kunisimulia/kunikumbusha ile safari ya 1994 alivyonibeba kwa baiskeli safari nzima hadi kunifikisha na alivyorudi peke yake. Kwakweli nilipatwa mshituko fulani, kwa sababu hiyo ilikuwa ni proof nyingine kwamba ni kweli nilibebwa kwa baiskeli katika safari ile. Nilisafiri safari moja kwa namna mbili tofauti kwa wakati mmoja. The fact i don't believe even myself!
Kuna mengi pia yanayonitokea maishani hata sasa nabaki najishangaa tu na kukubali hivyo ndivyo nilivyo, ila kuna hili moja naombeni mnisaidie tafsiri yake; Mara nyingi ninapolala napata ndoto nikiwa napaa angani kama ndege, hii nini maana yake???
Mkuu Mzizi Mkavu, hebu zama kwenye ile link ya pili kwenye thread ya mwanzo!.
Pasco
Ukweli wa ndoto unategemea mambo mengi sana..
ila kubwa zaid ni muda ulioota ndoto yenyewe.
Ukweli wa ndoto unategemea mambo mengi sana..
ila kubwa zaid ni muda ulioota ndoto yenyewe.
Pasco embu tupe na hatua ya pili basi, hili somo lako nalipenda sana na ile issue ya maditation nilijaribu kufanya lakini nimeambulia patupu na nimeacha!
...
Nakumbuka niliweza kukiangalia kitu hadi nikawa nakiona kinabadilika rangi!
...
Muda wa kujiunga na vyuo vya meditation sina kabisa!
Embu anzisha thired na uweke hatua moja kwenda nyengine pamoja na masharti yake!
...
Napenda sana siku moja niuhame mwili wangu na kutembea kiroho tu!
nahisi mimi nina divination powers.lakini nashindwa namna ya kuzidelop.
ulikuwa umefikia mahali pazuri sana ulikata tamaa bure ,ile hali ya kuangalia kitu mpaka kinabadilika rangi ilikuwa ni mind transformation hukutakiwa kuacha
Nina uhakika zilikuja picha nyingi sana mwanzoni kama mkanda wa video kuhusu jana juzi au changamoto za maisha mapenzi nk ulitakiwa kuendelea na concentration yako
Khaa! Kumbe ilikuwa ni stage mzuri tu?!!!
Nilidharau bure kumbe!
Nakumbuka nilifanya maditation kwa wiki moja tu na nilifikia hivyo!
Embu mkuu nipe hatua baada ya kufikia hali kama hiyo (ya kuona rangi zinabadilika) nilitakiwa kuingia hatua gani? Or nilitakiwa kufanya nini?
...
Kumbuka, mimi ni mtumizi mzuri tu wa pombe!!!!!
Mkuu mayenga, mimi nina
Telepathy - Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.
Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.
Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!.
Matumizi ya nguvu hizi yalikuwa ni kwa "kata funua tuu!, mpaka nilipokutana na dada mmoja aliyekuakisoma Jangwani, ndipo akanieleza kuhusu uwezo huo, na ninachokifanya ni abuse of power! akanionya nikiendelea hivyo matokeo yake yatakuwa nini, ndipo nikabadilika!.
Ila mpaka leo, kuna mtu nikimfikiria tuu, anatoke, au nafika mahali na kuambiwa, una maisha marefu, sasa hivi tulikuwa tunakuzungumza!. Au uko mahali unatembea, njia nyembamba, unataka kupishana na mtu, ukienda upende ule naye anakuja huko, ukirudi huku naye anarudi huku hadi mnataka kugongana unaamua kusimama mpishane!.
Pia nina Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen. kidogo. Kuna mambo huwa naota yanakuja kutokea!. Nina kitu kinaitwa "intuition!" yaani kabla sijafanya jambo, unapata hisia this is not gona work!, au unakutana na mtu anakuzimikia sana for real, wewe unaona its not for real!. Au ndani ya ndoa, ikitokea wife ame cheat, utajua!, huwezi kuuliza kwa sababu huna ushahidi, ili mtu akicheat, ujue atacheat tena!, nilianza kufanya kazi ya kukusanya ushahidi nikathibitisha!, na nilisamehe kwa kujifikiria ni mara ngapi nilipitia wake za watu!, wengine wakiwa ni wake wa marafiki zangu kabisa!.
Pia naweza kufanya Aura reading - Perception of the energy fields surrounding people, places, and things kwa kiwango kidogo!, nikikutana na mtu for the first time, I can tell huyu ni mtu mwema au ni mtu mbaya!. Hii nimeiwea kwa practice kutoka kwenye net.
Retrocognition - Perception of past events imeishanitokea mara kadhaa, naweza kufika mahali for the first time, na kujiona I have seen this place before ila sikumbuki ni wapi!, au nimekutana na mtu for the first time, na kujiona I've seen him before sijui ni wapi!, hii inaitwa De-ja-vu kwa Kifaransa!.
Nimesoma sana vitabu vingi vya mambo haya, hivyo naangalia uwezekano wa kufungua more evenues kwa meditation ila kwa njia ya natural sio kupitia secret societies kama Freemasons, Illuminati au Rosecrusians. Hawa jamaa ndio ma master wa haya mambo ila wanafanya siri!. Matajiri wengi wanatumia powers hizi kupata utajiri iwe ni kwa njia za sala kupitia makanisa ya wokovu, waganga wa kienyeji, kujiunga na vikundi kama freemasons etc, all and all its works of powers!.
Pasco.