Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Mkuu Pasco tatizo ni kwamba hizi power ukiziweka kwenye real world hili kila mtu azione zinagoma...I am sure hakuna hata psychic mmoja atakejitokeza adharani na kusema ndege iko wapi...

Ninazo video kadhaa nitazipandisha punde hapa jamvini kuna mzee mmoja fundi anaonyesha nguvu hizo dhairi ila mwishoni alikiri nguvu hizo kupotea baada ya yeye kudemonstrate hili watafiti wazungu wazione.

Vuta subira!! Nitapandisha mzigo huo hapa punde.
 
Niliota ndoto siku chache zilizopita, nilikuwa na kipochi changu kiunoni eneo lililokuwa na umati wa watu mara nikaona watu wananiangalia huku wakiongea ni vijana wa kiume. Nilipowatazama vizuri nikahisi ni vibaka na hisia zikanipa kuwa wanataka kuniibia. Ndani ya kile kipochi kulikuwa na simu mbili, kitabu kidogo cha mambo ya habari miwani body spray, usb cable mbili na pesa kiasi.

Akili ikaniamuru mara moja kutoka eneo lile kwamba naweza ibiwa, kiukweli nilijibanza sehemu ghafula nikawa ninawaona wale vijana wenye mionekano ya vibaka. Mara wakaja kasi nilipokuwa awali wakanikosa wakaonekana kushangaa na kuogopa imekuwaje ndani ya sekunde kadhaa sipo eneoni. Nikamsikia mmoja akisema anabahati leo tungemkwangua kila kitu, wakaondoka na mimi gari ikafika ile natoka ili niingie kwa gari nikaamka.

Hii ni nini, yaani kwamba ina maana gani, nimeshindwa kupata tafsri. Na je nifanyeje ili hali kama hii niwe napata tafsiri yake kihalisia?

Nakumbuka kuna wakati niliwahi ota kuwa nimefungwa pingu hazikupita siku nyingi polisi walikuja wakanikamata na nilifungwa pingu ila nilitoka baada ya muda mfupi. Siku hiyohiyo baada ya kuota ndoto ya kufungwa pingu niliota tena kuwa nipo na Wahasibu wanahesabu hela na mimi nimekaa nawasubiri na hizo hela zilikuwa zangu. Ila hizo hela sijazipata mpaka leo. Majuzi ndio nikaota hiyooo ndoto ya vibaka.

Mtu mmoja nilipomueleza akaniambia kuna hela nitapata nyingi tu hivyo ninapaswa kuwa makini na kila nitakaye kutana naye. Nisaidie kwa ufafanuzi mdau wangu wa nguvu.
 
1514429_600015050083801_1706213807_n.jpg

Hujanipa Hatuwa ya pili kuhusu Aura mbona?
Mkuu Mzizi Mkavu, hebu zama kwenye ile link ya pili kwenye thread ya mwanzo!.
Pasco
 
Mkuu Mzizi Mkavu, hebu zama kwenye ile link ya pili kwenye thread ya mwanzo!.
Pasco

Mkuu Pasco..
Kwanini somo haliendelei tumestuck hapa hapa...wanafunzi tupo tayari mwalimu jitokeza basi...
 
Nina Bilocation/Multilocation;

Mwezi January 1994 nilihama kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine na baadhi ya ndugu zangu, nina kumbukumbu mbili juu ya safari hiyo.
Kumbukumbu ya kwanza ni kwamba katika safari hiyo tulitembea kwa miguu na ndugu zangu mwanzo wa safari hadi mwisho, tulivuka mto pia kwa kutembea katika maji kidogo yaliyokuwa kwenye mwendo. Safari ilikuwa ndefu kwani tulianza kutembea kama saamoja asubuhi hadi mida ya saa saba mchana. Katika safari hiyo mara kwa mara nilikuwa nachoka na hivyo kupelekea ndugu zangu kunibeba mgongoni kwa kupokezana, tulifika salama siku hiyo.

kumbukumbu ya pili juu ya safari hiyo ni hii;
Ndugu zangu walitembea kwa miguu isipokuwa mimi ambaye nilibebwa kwa baiskeli na mjomba wangu hadi kule mwisho wa safari kisha yeye akarudi. Nilikaa pale kuwasubiri wenzangu waliokuwa wanasafiri kwa miguu hadi walipowasili mchana. Kwa kifupi mimi sikutembea kwa miguu wala kuvuka maji mtoni katika safari hiyo.

Kwa bahati nzuri au mbaya nilihama tena wilaya hiyo na kwenda kuishi mkoa mwingine kabisa kwa miaka mingi nikiwaacha ndugu zangu, hizo kumbukumbu mbili za safari moja zikawa zinasumbua akili yangu kadiri miaka ilivyokuwa inasonga, kwa muda mrefu sikupata mtu sahihi wa kumweleza au kumwuliza ili anipe clarification.
Miaka kama mitano baadae nilikutana na mmoja wa ndugu zangu tuliotembea pamoja ile safari, tuliongea na kukumbushia ile safari ya mwaka 1994 na nika-prove kwamba tulitembea kwa miguu. sikumweleza kwamba nakumbuka pia namna tofauti ya safari ile.
Miaka kumi badae, mwaka 2004 ulitokea msiba kule nilikohama mwaka 1994 na nikaenda kuhudhuria msiba ule (Sikuwahi kurudi kule kabla ya msiba huo), basi mara moja nikakutana na mjomba aliyenibeba kwa baiskeli katika safari ya mwaka 1994 na palepale akaanza kunisimulia/kunikumbusha ile safari ya 1994 alivyonibeba kwa baiskeli safari nzima hadi kunifikisha na alivyorudi peke yake. Kwakweli nilipatwa mshituko fulani, kwa sababu hiyo ilikuwa ni proof nyingine kwamba ni kweli nilibebwa kwa baiskeli katika safari ile. Nilisafiri safari moja kwa namna mbili tofauti kwa wakati mmoja. The fact i don't believe even myself!

Kuna mengi pia yanayonitokea maishani hata sasa nabaki najishangaa tu na kukubali hivyo ndivyo nilivyo, ila kuna hili moja naombeni mnisaidie tafsiri yake; Mara nyingi ninapolala napata ndoto nikiwa napaa angani kama ndege, hii nini maana yake???
 
Mkuu John Kachembeho, hiyo 1994, ulikuwa na umri gani?!.

Hizo ndoto za kuota unapaa ni ndoto za kawaida tuu, ila pia unaweza kuwa unapaa kweli!.
Kipimo cha kuzipima kama ni za kawaida au unapaa kweli ni kimoja tuu.

Ukiona unapaa, kisha ukashtuka, akajiona kama una hema fulani, kumbuka uliona nini ulipopaa, eg, sherehe, msiba, tukio, etc, kesho yake ukipata habari hicho ulichoota ni kweli kimetokea, then ni kweli ulipaa!.

Ukiota unapaa, then ukiamka uko ok, nothing happened, then ni ndoto tuu!.
Pasco
 
Pasco embu tupe na hatua ya pili basi, hili somo lako nalipenda sana na ile issue ya maditation nilijaribu kufanya lakini nimeambulia patupu na nimeacha!
...
Nakumbuka niliweza kukiangalia kitu hadi nikawa nakiona kinabadilika rangi!
...
Muda wa kujiunga na vyuo vya meditation sina kabisa!
Embu anzisha thired na uweke hatua moja kwenda nyengine pamoja na masharti yake!
...
Napenda sana siku moja niuhame mwili wangu na kutembea kiroho tu!
 
Ukweli wa ndoto unategemea mambo mengi sana..
ila kubwa zaid ni muda ulioota ndoto yenyewe.

Ndoto ni vague memories ya mambo yote yaliyokutokea maishani mwako kwa kuwaza kunena au kutenda
Kuna ndoto zinatokana na yaliyotokea leo lakini nyingine ni za juzi au hata mwezi uliopita .inategemea tu zilihifadhiwa kwenye sense ya ngapi na kulikuwa na nguvu gani
 
Pasco embu tupe na hatua ya pili basi, hili somo lako nalipenda sana na ile issue ya maditation nilijaribu kufanya lakini nimeambulia patupu na nimeacha!
...
Nakumbuka niliweza kukiangalia kitu hadi nikawa nakiona kinabadilika rangi!
...
Muda wa kujiunga na vyuo vya meditation sina kabisa!
Embu anzisha thired na uweke hatua moja kwenda nyengine pamoja na masharti yake!
...
Napenda sana siku moja niuhame mwili wangu na kutembea kiroho tu!

ulikuwa umefikia mahali pazuri sana ulikata tamaa bure ,ile hali ya kuangalia kitu mpaka kinabadilika rangi ilikuwa ni mind transformation hukutakiwa kuacha
Nina uhakika zilikuja picha nyingi sana mwanzoni kama mkanda wa video kuhusu jana juzi au changamoto za maisha mapenzi nk ulitakiwa kuendelea na concentration yako
 
nahisi mimi nina divination powers.lakini nashindwa namna ya kuzidelop.

Tafuta muda wa kama wiki moja nenda retreat mbali na nyumbani kwako mfano kwenye mbuga za wanyama ambako kuko natural na hakuna kelele
Kakae huko ukiwa huna mawasiliano na dunia nyingine zima simu zako epuka kukutana na watu kunywa maji muda mwingi vaa nguo zisizo bana mwili ukiweza vaa pyjama tuu kula vyakula vya kuchemsha hasa mbogamboga kula usishibe kila mlo
kuwa na ratiba ya kula muda ule ule na kipimo kile kile asubuhi mchana na jioni
Fanya kitu kilekile kwa muda uleule kwa siku zote utakazokaa huko
Rekodi matukio yote yatakayotokea kipindi chote hicho kama kuumwa mwili kupata hasira za ghafla kuharisha kuota vipele nk nk nk
 
ulikuwa umefikia mahali pazuri sana ulikata tamaa bure ,ile hali ya kuangalia kitu mpaka kinabadilika rangi ilikuwa ni mind transformation hukutakiwa kuacha
Nina uhakika zilikuja picha nyingi sana mwanzoni kama mkanda wa video kuhusu jana juzi au changamoto za maisha mapenzi nk ulitakiwa kuendelea na concentration yako

Khaa! Kumbe ilikuwa ni stage mzuri tu?!!!
Nilidharau bure kumbe!
Nakumbuka nilifanya maditation kwa wiki moja tu na nilifikia hivyo!
Embu mkuu nipe hatua baada ya kufikia hali kama hiyo (ya kuona rangi zinabadilika) nilitakiwa kuingia hatua gani? Or nilitakiwa kufanya nini?
...
Kumbuka, mimi ni mtumizi mzuri tu wa pombe!!!!!
 
Acha pombe zinaharibu usikivu wa mwili !!!hatua inayofuata inategemea na background yako lakini kwa kifupi endelea kupractice
 
Mkuu mayenga, mimi nina
Telepathy
- Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.

Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.

Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!.

Matumizi ya nguvu hizi yalikuwa ni kwa "kata funua tuu!, mpaka nilipokutana na dada mmoja aliyekuakisoma Jangwani, ndipo akanieleza kuhusu uwezo huo, na ninachokifanya ni abuse of power! akanionya nikiendelea hivyo matokeo yake yatakuwa nini, ndipo nikabadilika!.

Ila mpaka leo, kuna mtu nikimfikiria tuu, anatoke, au nafika mahali na kuambiwa, una maisha marefu, sasa hivi tulikuwa tunakuzungumza!. Au uko mahali unatembea, njia nyembamba, unataka kupishana na mtu, ukienda upende ule naye anakuja huko, ukirudi huku naye anarudi huku hadi mnataka kugongana unaamua kusimama mpishane!.

Pia nina Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen. kidogo. Kuna mambo huwa naota yanakuja kutokea!. Nina kitu kinaitwa "intuition!" yaani kabla sijafanya jambo, unapata hisia this is not gona work!, au unakutana na mtu anakuzimikia sana for real, wewe unaona its not for real!. Au ndani ya ndoa, ikitokea wife ame cheat, utajua!, huwezi kuuliza kwa sababu huna ushahidi, ili mtu akicheat, ujue atacheat tena!, nilianza kufanya kazi ya kukusanya ushahidi nikathibitisha!, na nilisamehe kwa kujifikiria ni mara ngapi nilipitia wake za watu!, wengine wakiwa ni wake wa marafiki zangu kabisa!.

Pia naweza kufanya Aura reading - Perception of the energy fields surrounding people, places, and things kwa kiwango kidogo!, nikikutana na mtu for the first time, I can tell huyu ni mtu mwema au ni mtu mbaya!. Hii nimeiwea kwa practice kutoka kwenye net.
Retrocognition - Perception of past events imeishanitokea mara kadhaa, naweza kufika mahali for the first time, na kujiona I have seen this place before ila sikumbuki ni wapi!, au nimekutana na mtu for the first time, na kujiona I've seen him before sijui ni wapi!, hii inaitwa De-ja-vu kwa Kifaransa!.

Nimesoma sana vitabu vingi vya mambo haya, hivyo naangalia uwezekano wa kufungua more evenues kwa meditation ila kwa njia ya natural sio kupitia secret societies kama Freemasons, Illuminati au Rosecrusians. Hawa jamaa ndio ma master wa haya mambo ila wanafanya siri!. Matajiri wengi wanatumia powers hizi kupata utajiri iwe ni kwa njia za sala kupitia makanisa ya wokovu, waganga wa kienyeji, kujiunga na vikundi kama freemasons etc, all and all its works of powers!.
Pasco.

kiukweli nimeogopa maana hayo yote umetaja mimi ninayo kwa kiasi kikubwa najua mpnz wangu aki cheat naota tukio kabla halijatokea nisha fika sehemu nyingi ambazo niliziona kwenye ndoto au kuhisi nilishafika before sijatongozwa nimeshajua unataka kusema nini kama ume cheat kwenye the same bed nikilala hapo matukio yote yanajirudia nikitaka kujua mpnz wangu jana alikua nanani navuta hisia alipo picha nzima inakuja lkn mwanamke anafichwa sura najiogopa nimejaribu kwenda kanisani kunywa pombe na kula kitimoto ili niwe normal imepungua kidogo ila now inarudi kwa speed yaani kabla hujanifanyia lolote napata hisia kua utakachofanya sio kizuri au ni kizuri
 
Back
Top Bottom