Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Mkuu Pasco, hebu rudi kwenye huu uzi wako, kuna ufafanuzi wahitajika tafadhali
 

Ushawahi kujiuliza kama MUNGU wa waislamu na wakristo ni mmoja mbona tunatumia vitabu tofauti na vyenye maagizo tofauti?!..Je,MUNGU huyu awaagize hawa waoe wake wanne na wengine waoe mke mmoja,hawa wasali kwa Jina la YESU na wengine wamwamini Muhamad?!Awaambie wengine kuna majini mabaya na mazuri na wengine majini ni viumbe vilivyoasi na vinasubiri hukumu?!Awaambie hawa ukienda peponi utapata wanawake walionona 72 na wengine awaambie mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa?!Awaambie hawa kisasi ni juu yake na wengine awaambie kisasi kinaruhusiwa?!..
Tafsiri ya neno MUNGU ni chenye kuabudiwa so mtu akisema namwamini MUNGU ni lazima umuulize MUNGU yupi?maana wengine wanaabudu Jua,mwezi,nyota,ng'ombe,kijiko,marehemu(mizimu) na wao wanadai wanamwamini MUNGU..
Ukweli ni kwamba wanachoabudu waislam sio sawa wanachoabudu wakristo na ushahidi ni maagizo(vitabu vyao) jinsi vinavyokinzana vinaonyesha wazi maagizo hayo yanatoka kwa waabudiwa tofauti.
Kusema tunamwamini MUNGU mmoja ni kujitia moyo tu lakini ukweli ni kuwa huku duniani kuna miungu mingi na la kusikitisha watu wengi wanaabudu wasivyovijua wakidhani wapo sahihi kumbe wanapotea dah.
BWANA YESU na afungue macho ya nyoyo zenu mpate kujua ukweli.
 

Daaaah haya maelezo yamereflect kitu kinachokuwa kinanitokea... sometimes naweza kufika mahali nahisi kama nishawahi kupaona au kufika... na mwisho huwa na conclude kuwa May be nilishaota nipo mahali hapo kabla na kupotezea tu.. thanks Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pasco, hebu nikuulize, hizi Pyschic power huja kwa kumaditate. Kuna watu walikua siku za nyuma pale CBE wakifanya hii kitu ila wao hawali samaki na nyama, vile vile hawataki mambo ya kugonga mara kwa mara au kujichua kwa aina yeyote kwa madai, vitu hivyo hupunguza nguvu za hiyo meditation, hii imekaaje maana sijaona uizungumzie.

Vilevile hizi nguvu mnadai zinatoka kwenye au mnaziita universe na huku mkidai wengine wanziita Mungu na wengine Allah, kwa hiyo hamuamini kama kuna Mungu na hivyo nguvu hizi ziko naturally?

Na ipi njia rahisi ya kujenga nguvu hizi kwa muda mfupi?
 

Ni kuamini "IMANI"ndo mambo yote
 
there is no such thing as " psychic powers " hiyo unatakiwa ulale nayo leo. Those guys manipulate others by observation. The weaker you are the easier it become for them to catch you. Lose your faith ( which is not easy for you following maelezo yako meengi ila jaribu kuacha kuamini )and then kutana na psychic mmoja halafu muangalie katika jicho la kawaida utaona walivo tapeli. Only weak people are manipulated and I believe you are not one of them.
 
Mkuu, na wenye nyota ya Simba tukoje?

NYOTA YAKO YA SIMBA MAISHA YAKO YOTE YAPO HAPO:


NYOTA YA SIMBA (LEO)


  • Hii ni nyota ya tano katika mlolongo wa nyota kumi na mbili.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21Julai na 21 Agosti.
  • Sayari yao ni Jua (Sun).
  • Siku yao ya bahati ni Jumapili.
  • Namba yao ya bahati ni 1 na 4.
  • Rangi yao ya bahati ni Njano au rangi ya Dhahabu.
  • Asili ya nyota yao ni moto.


KIPAJI CHA SIMBA (INSPIRED):
Wenye nyota hii wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.
Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi.

TABIA ZA SIMBA:
Watu wenye nyota hii ya Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Ni watu wanaopenda kutumia na wanataka waonekane na wanuwezo wa kuvumbua mambo amabyo watu wengine hawajui na wanapenda sana heshima.
ni wakarimu lakini ni wajeuri na wanapenda kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.

TABIA YA SIMBA KATIKA MAPENZI:
Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.
Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

MATATIZO YA KIAFYA:
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.
Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.
Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.
Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.
Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.
{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.
Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.
Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.
Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

FAMILIA ZA SIMBA:

Kwa asili Simba ni Mfalme na mamlaka yake yamezungukwa na hisia za kifalme. Wazazi wa simba huwa wana mila ya kuwapangia watoto wao namna watakavyoishi kwa sababu wanajivunia sana familia zao.

Wazazi wa Simba wanajiona kwamba wana nafasi kubwa katika dunia ambayo inawataka wajionyeshe kwa watu ubora. Pamoja na kwamba wenye nyota hii hupenda kuzunguka na watoto wao (na wao wenyewe wakati mwingine wana tabia ya utoto) hawakubali kupoteza heshima zao wakati wanafanya hivyo.

Wenye nyota hii ni wachangamfu, wenye moyo wa kupenda na wanapenda raha, pamoja na ukali wao wanaweza kuwa wepesi kwa watoto wao.

Watu wa simba kwa uhakika wanaona raha kuwa wazazi lakini wanatakiwa wawe makini kutowaharibu watoto wao kwa zawadi nyingi na maisha ya raha.
Simba wana uhakika na nafasi yao katika jamii kwamba wao ni viongozi hivyo watoto wao huwa wanapenda kujionyesha na wanategemea wawe wanaonekana kwa watu muda wote.

MADINI YA SIMBA:
(AMBER); Jiwe hili lenye rangi ya njano iliyochanganyika na kahawia linasemekana lina uwezo wa kumpa ukakamavu na ari ya uongozi kwa anayelivaa, vilevile linamwepusha mvaaji na maradhi ya kichwa.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(SIMBA NA NDOO):
Tabia ya Simba ya kutopenda kudhibitiwa au kudhibiti watu inakuwa ni faraja kubwa kwa wenye nyota ya ndoo ambao wanapenda uhuru na kufanya mambo yao bila kuingiliwa.

VYAKULA VYA SIMBA:
Wenye nyota ya simba wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao.
Vyakula hivyo ni machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo.

NCHI ZA SIMBA:
Watu wa nyota ya simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.
Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)

RANGI ZA SIMBA:
Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri


Kuota wewe una paa inaonyesha unaye Spiirit mwilini mwako.
 
Mkuu mbona hujajibu kitu umefanya kiujumlajumla tu!

Kwa uelewe mdogo nilivyowaelew Pasco na Rakim...usemacho kweli ni nguvu za MUNGU,isipokua nyakati Muumba anatuumba alitupa uwezo wa kutenda kila kitu bcoz we hve the power aliyoiweka yeye mwenyewe,sasa linapokuja swala la kuchaji hizo nguvu kwa maelezo ya mtoa mada ni kwamba inahitaji kuamini kua you hve the power na hakuna kinachoweza shindikana kwako,ukielewa hilo utagundua kwamba wako ambao wameweza kuchaji nguvu zilizo ndani yao na kujikuta hata wakichezea akili za wale ambao hawajajua kua wanazo nguvu hizo hizo pia,kwa mfano waganga wa kienyeji,wasoma nyota,na wale wanaotiisha mapepo yakatii.lakini wanafanya haya kwa muhimili mkubwa wa IMANI,wanajiamini kua wanaweza na kweli wanaweza.sasa swala la hao ndugu waliokua wanafanya meditation yakua hawakua hawali baadhi ya vyakula na hawafanyi mapenzi ovyo I think ni katika ile hali ya kutokutaka kuchafua mwili na roho kwa matendo ya maudhi kama uzinzi,yamkini medi yao waliielekeza kwa kumtegemea MUNGU ambae kimsingi hachangamani na uchafu kama uzinzi,japo katika kusherehesha hili ntamuomba RAKIM aje akupe soma zaidi.lakini all in all katika kutenda kila jambo yapaswa kua na Imani,hapo ndipo Pasco alipokazia.
 
this is outrageous, I can't believe am actually reading this in JF...Anyway you can choose to believe anything you want to believe but hakuna ukweli juu ya ndoto, utabiri wala nyota. Haya ni masuala madogo madogo ambayo wachache wanatumia uwezo wetu wa kuamini bila kuhoji kupata umaarufu. Mara ngapi vitu ambavo vilitakiwa vikutokee following maelezo ya nyota yako havijakutokea? fanya research ya nguvu uone kama hauji na majibu tofauti { Maneneo yako ya research yawe yenye valid infoz na ni trusted }
 
Ukiamaini au usipo amini hilo silo swala langu kwanza sijakuwekea wewe kwanini una Comment kitu ambacho hakikuhusu? ignore achilia mbali ipite wewe fanya kama hujaiona Mkuu BestOfMyKind Jambo halikuhusu wewe kwanini unaliingilia? umetumwa nini na wakuu wako wa kazi? Achana na Comment zangu kabisa take care you self. Tafadhali usini Tag jiheshimu utaheshimiwa.
 
Doh!! Sikua na maana ya kukuudhi ndugu yangu, wala hakuna alienituma kuja kujibu post yako...nilipokua napitia huu uzi moja kati ya sehemu zilizonivuta kuziongelea ilikua post yako..Mi nafikiri ingekua vizuri ukanishika kwa facts kuliko kunituhumu kua nimetumwa na kua nimevamia post isionihusu...Post yako ni debatable, mimi kutoa maoni yangu ( ambayo in some ways yameonekana kama ni conclusion na yana-infuriate ) hakukuzuii wewe kutoa hoja zako ambazo zitakinzana na zangu. Kama hutopenda kuendelea kujadiliana namimi I'll understand. Ni hayo tu mkuu.
 
Bwana pasco kujuwa kwingi mbele ni giza acha kuongea usichokijuwa...jifunze au tafuta watu wakufundishe maandiko matakatifu na siyo kuyapotoa namna hii...neema ya Mungu ikushukie umjue yeye aliyewapekee...
 

Kaka mbona umekuwa mkali ghafla? Hupendi changamoto?
 

mkuu umenifungua upo kama mimi naweza kumbka mambo ya zamani sana nikiwa mtoto lakini nikasahau kitu cha jana tu hi inakuwa imekaaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…