SOURCE YA POWERS ZA MUNGU NA SHETANI:
Mwenyezi Mungu Kabla Ya Kuumba Aliumba MBINGU Na Ardhi Sikuwepo Lakini Ndio Ukweli Ulivyo Kisha Akaumba Viumbe Ambao Ni Malaika Kwa Kuamuru Nuru Yani Mwenyezi Mungu Akisema "Kuwa Jambo Linakuwa" baada ya hapo akaumba mazingira yaani mimea,wanyama,wadudu n.k except binaadamu na majini....
baada ya mazingira ndipo akaumba majini na kuwakabidhi ulimwengu na kuwawekea vipower vya kuwasaidia kuishi duniani hapa... katika kuumba mwenyezi mungu aliwapa malaika akili tu... lakini wanyama akawapa matamanio...
baada ya kuumba majini akawapa vitu viwili matamanio na akili nao aliwaumba kwa moto... baada ya kuwepo kwa wingi wa miaka majini walianza kumuasi mwenyezi mungu...
wakuu siongelei dini ya mtu hapa naongelea kuzitafuta tofauti ya power za mwenyezi na shetani...
Walimuasi Sana Ikafikia SEHEMU mwenyezi mungu akatoa kauli kwamba wakauliwe wote...
majeshi ya malaika wakashuka duniani na kuuwa kila jini waliemuona mbele yao waliwauwa wengi sana lakini kwa kuwa mwenyezi mungu ni mjuaji zaidi katika kuwapa kipower majini aliwapa kipower cha kuingia popote kama moshi bila kupaharibu ndipo hapa walipokimbia wengine kwenye miamba matumbo ya wanyama na baharini ambapo malaika hawana amri ya mungu kufika maeneo hayo...
walipoona wameenda mule walikaa sana majini ndani ya maeneo hayo kwa kuwa majini ni survivals wa miaka mingi waliweza kujificha kwa muda mrefu hadi pale ilipotoka amri ya mwenyezi mungu kwamba waachwe.. wakati vita inaendelea malaika walikikuta kitoto jini(JINI) Hakihusiani kabisa na Malaika NI KITOTO JINI...
Ambacho walikibeba na kumuomba mwenyezi mungu atoe hukumu kuhusu kitoto kile mwenyezi mungu akaamuru kuwa katika majini chenyewe kakiumbia kwa ulimi wa moto sio moto kama majini wengine hivyo alijua mwenyezi mungu kwa nini kakiumba kwa ulimi wa moto akawaamuru wakilee...
baada ya kupita muda mwenyezi mungu aliwakusanya malaika wake na kitoto jini ambacho ndio unaemskia leo shetani au jini wakati bado yupo mtoto mambo haya yanaendelea... mwenyezi mungu akawaambia malaika wake nitamleta kiumbe atakaeishi humo duniani na watazaliana hadi siku ya mwisho....
malaika wakajibu "ewe mola wetu unataka kumleta kiumbe atakae fanya maasi ya kumwaga damu na machafuko katika dunia yako"?
mwenyezi mungu akawaijibu "hakika mimi ninayajua msioyajua yaliopo mpaka ndani ya nyoyo zenu nayajua"
malaika wakamwambia umetakasika ewe mjuzi wa wajuzi...
mwenyezi mungu akamuumba adamu kwa neno kipindi adamu yupo dongo kitoto jini kilikuwa kinachezea mwili wa adamu kwa kuingia mapuani kutokea kwenye kila tundu la mwili....
vile kililelewa kimalaika na kujua historia yake na kukua kikawa kichamungu sana nikisema "abasajda" waislamu wanamjua sana alikuwa ni mwingi wa kusujudu na kumuomba mungu yeye ndo yeye hadi baadhi ya malaika akawashinda..
ilipofika wakati adamu alivyokamilika likalia la mgambo mbinguni na wakaitwa malaika woote na kuambiwa leo ni siku ya kumtambulisha kwenu kiumbe mpya adam niliemuumba kwa udongo nikampa vitu viwili akili na matamanio...
kisha akawaita wanyama wote wa duniani na viumbe wengine na kuwaamuru malaika wawataje ni kina nani??
"malaika wakajibu umetakasika wewe mjuzi wa wajuzi sisi hatujui lolote ewe mola wetu"
ndipo mwenyezi mungu akamuamuru adamu awataje viumbe wale adamu kama tape recorded akaanza kuwaolodhesha kwa majina... lugha aliotumia kuwataja ni moja ambayo tutaizungumza sote siku ya mwisho... wanaijua wachache miongoni mwenu lugha hiyo ambayo haileti maana ukitoa yake herufi hata moja....
baada ya kuwaorodhesha ndipo mwenyezi mungu akawaambia malaika wote wamsujudie ikiwemo abasajda ambae alishasali duniani kila sehemu unayokanyaga wewe yeye alishasali... malaika wote wakaenda chini kumsujudia adamu sasa hapa ndipo jina la shaitwan au shetani ibilis likaanzia hapa kwamba aliehasi... ni vibaya sana na ni machukizo kumuita binaadamu mwenzio shetani maana yeye bado ananafasi ya kutubu kurudi kwa muumba wake ndio maana wewe uliemuita pasco wakala wa shetani ulinikwaza sana kuhukumu nyama hai...
mwenyezi mungu akamwambia ewe ibilis yani ulieasi mbona humsujudii adamu?
kwa majigambo ya umbo ibilisi akasema ewe mola wangu mtukufu siwezi kumsujudia huyo japo tunafanana sifa za matamanio na akili ila umbo yeye ni udongo na mimi ni moto tena ulimi wa moto.....
ndipo hapa mwenyezi mungu akamwambia imelaaniwa na adhabu yako ni moto wa ajabu uwakao
"ibliis akasema nakuomba ewe mola wangu unipe uwezo wa kuniweka hadi mwisho wa dunia na nitawapotosha wote wa kama huyu....
"Ndipo Mwenyezi Mungu Akamwambia Utawapotosha lakini sio wa kwangu na nimekupa nafasi ulioomba lakini laana yangu ipo juu yako na moto uwakao unakusubiri"
kwa mwenye kupenda kisa hiki nitakiendeleza lakini Jibu Lako Mkuu PASCO liko hapa kwamba power ya shetani kapewa kipawa kidogo cha kupumbaza na kuwepo hadi kiama akili na matamanio na inguvu kidogo ya kichawi na aliempa ni mungu...
makazi yako ya shetani utakaa nae motoni na nyote mtakula adhabu ya milele
na
makazi yako na mwenyezi mungu atakuwepo akikuangalia kwa karibu sana peponi na kule hakuna kutubu wala kusali tena ni starehe mtindo mmoja lakini hutamuona mola wako kwa macho daima na hii imani uwe nayo ili siku shetani akikwambia mimi mungu mwambie ametakasika mola wangu asiyeonekana milele...
N.B
Mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu jichungeni.....
#Rakims