Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.
Chief naomba unisaidie . Mimi usiku huwa naota napaa Kama Nina mbawa na huwa ni muda mrefu hutokea hicho kitu ebu naomba unisaidie nini Maana yake
 
Je kuna uwezekano wa mtu kuukopi mwili wa mtu mwingine na kufanana naye kwa 100%? Mfano wa lile roboti kwenye movie terminator 2.
Utakesha ndugu..kaa ktk uhalisia wako na tumia meditation kupambanua mambo au kutengeneza akili iliyotulia kuliko kujaribu kuvaa mwili usio wako naamini utafeli tu.
 
Uli practice kivipi mkuu kila siku au na kwa njia gani
Nili practice kila siku, asubuh nikiamka au jioni wakat nimetoka job kukiwa na utulivu au muda mfupi kabla sijalala...hii kitu ukianza kuifanya inakuwa nzuri sana ..kama ndio unaanza unaweza kufanya guided meditation, download app
 
Mkuu mayenga, mimi nina
Telepathy
- Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.

Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.

Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!.

Matumizi ya nguvu hizi yalikuwa ni kwa "kata funua tuu!, mpaka nilipokutana na dada mmoja aliyekuakisoma Jangwani, ndipo akanieleza kuhusu uwezo huo, na ninachokifanya ni abuse of power! akanionya nikiendelea hivyo matokeo yake yatakuwa nini, ndipo nikabadilika!.

Ila mpaka leo, kuna mtu nikimfikiria tuu, anatoke, au nafika mahali na kuambiwa, una maisha marefu, sasa hivi tulikuwa tunakuzungumza!. Au uko mahali unatembea, njia nyembamba, unataka kupishana na mtu, ukienda upende ule naye anakuja huko, ukirudi huku naye anarudi huku hadi mnataka kugongana unaamua kusimama mpishane!.

Pia nina Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen. kidogo. Kuna mambo huwa naota yanakuja kutokea!. Nina kitu kinaitwa "intuition!" yaani kabla sijafanya jambo, unapata hisia this is not gona work!, au unakutana na mtu anakuzimikia sana for real, wewe unaona its not for real!. Au ndani ya ndoa, ikitokea wife ame cheat, utajua!, huwezi kuuliza kwa sababu huna ushahidi, ili mtu akicheat, ujue atacheat tena!, nilianza kufanya kazi ya kukusanya ushahidi nikathibitisha!, na nilisamehe kwa kujifikiria ni mara ngapi nilipitia wake za watu!, wengine wakiwa ni wake wa marafiki zangu kabisa!.

Pia naweza kufanya Aura reading - Perception of the energy fields surrounding people, places, and things kwa kiwango kidogo!, nikikutana na mtu for the first time, I can tell huyu ni mtu mwema au ni mtu mbaya!. Hii nimeiwea kwa practice kutoka kwenye net.
Retrocognition - Perception of past events imeishanitokea mara kadhaa, naweza kufika mahali for the first time, na kujiona I have seen this place before ila sikumbuki ni wapi!, au nimekutana na mtu for the first time, na kujiona I've seen him before sijui ni wapi!, hii inaitwa De-ja-vu kwa Kifaransa!.

Nimesoma sana vitabu vingi vya mambo haya, hivyo naangalia uwezekano wa kufungua more evenues kwa meditation ila kwa njia ya natural sio kupitia secret societies kama Freemasons, Illuminati au Rosecrusians. Hawa jamaa ndio ma master wa haya mambo ila wanafanya siri!. Matajiri wengi wanatumia powers hizi kupata utajiri iwe ni kwa njia za sala kupitia makanisa ya wokovu, waganga wa kienyeji, kujiunga na vikundi kama freemasons etc, all and all its works of powers!.
Pasco.
kaka pasco naomba hizo power ulizoziolozesha hapo ambazo huwa unatumia tuelezee kiswhili ili tupate kujua kiundani zaid
 
Somo la kwanza kuhusu namna ya kusoma Aura ni picha ya kwanza.
Concentarate kuangalia hizo picha mbili, utaziona kama zinataka kuungana na kuwa picha tatu, ya katikati inakuwa na umbo la msalaba. Kwa pembeni unaona kama mwanga wa blue una glow!, hiyo ndio aura!

Somo la pili. ni picha ya pili.

Concetrate kwenye kuangalia hicho kidoti cheusi hapo katikati kwa muda mrefu. Utaona hizo picha mbili zinatoa mwanga wa light blea green kwa nyuma, huo mwanga ndio aura!.

Ukiweza hii hatua ya kwanza, nakupeleka ya pili!.

Pasco.

Mkuu Pasco, nimejaribu kuangalia picha ya pili yenye kidoti. mwanga wa light blue unatokea kwenye picha nyekundu lakini picha ya blue ina potea kwa semi cirle ya kwanza then inafuata ya pili. Panakuwa peupe kabisa nabaki na circle ya red pekee. je nakosea mahali?
 
Back
Top Bottom