Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.

MShana hiki kitabu wirelessly ni expensive sana ,, nimecheck Kindle kinaenda kwa USD 178. Duuuh nikastaajabu..
 
More disjointed bullshit!
Hiyo itakuwa ni maji maji, tunaitumia sana kwenye utumbo!. Utumbo wa mbuzi hatuuoshi kabisa!, tunaukamua tuu na kuusokota ile ile harufu isipotee!. Hata utumbo wa ngombe ile sehemu ya kitabu, tunakunguta tuu! na moja kwa moja kwenye sufuria, ile harufu ya utumbo ndio mpango mzima!, jee unajua ni harufu ya nini?!, disjoited bullshit!.

Kwa vile nyani haoni ...sishangai, nikiendwa mtwara ambako wewe ni chakula yao, nitafutilia kama kwenye utumbo pia wanaacha ili ni taste ...shit nilinganishe na ile ya bull!.
Pasco.
 
Hiyo itakuwa ni maji maji, tunaitumia sana kwenye utumbo!. Utumbo wa mbuzi hatuuoshi kabisa!, tunaukamua tuu na kuusokota ile ile harufu isipotee!. Hata utumbo wa ngombe ile sehemu ya kitabu, tunakunguta tuu! na moja kwa moja kwenye sufuria, ile harufu ya utumbo ndio mpango mzima!, jee unajua ni harufu ya nini?!, disjoited bullshit!.

Kwa vile nyani haoni ...sishangai, nikiendwa mtwara ambako wewe ni chakula yao, nitafutilia kama kwenye utumbo pia wanaacha ili ni taste ...shit nilinganishe na ile ya bull!.
Pasco.

Jibber jabber.
 
Pasco,
Thanks! I wonder how do you know these things! Umesomea? Nitajaribu ku-exercise kama ulivyonishauri. In-fact mara nyingi nimekuwa na wazo la kuwa mimi ni mtu wa kipekee ingawa bado sijawa na uhakika wa upekee huo, labda sasa umeanza kunipa mwanga! Sasa nitaanza kujifunza na ku-practice ili nione exactly what I have inside me!

NB:
Nashukuru kwa kunipa jina la ile nguvu ya pili (second sight) kwa kongezea tu ni kuwa ninapowaona watu hao walio uchi ni kweli kuwa wenyewe hawaoni wala kusikia lakini ukifanya jambo (kwa vitendo au maneno) kuwahusu wao wanashtuka na ku-take action! Hilo nimelishuhudia mara kadhaa. Mfano kuna mmoja nilimwagia maji akashtuka, akageuka na kutokomea.
Mwingine aliingia chumbani kwetu (tukiwa watoto) kupitia kwenye ceiling board, nikapiga kelele kuwaambia wazazi kuwa kuna mtu hapa ameingia chumba chetu wakawa hawamuoni, nilipokomaa kumchunguza akanipiga ngumi ya mdomoni nikapiga kelele wazazi wangu wakawa hawaamini baada ya dakika chache mdomo ukaumuka (vimba) wakaanza kuogopa na kupiga kelele kuomba msaada toka kwa majirani na tangu siku hiyo wakaanza kuniamini!
Mkuu Mpigania Uhuru, fanya with moderations kwa sababu powers zako ni higher powers, ukizifanya unguided, tunaweza kujistukia tumekupoteza into the unknown.

Huyo aliyekuja chumbani kwako usiku ni mchawi, sio mwanga!. Kuna tofauti kati ya wanga na wachawi!. Wote wanaruka usiku na wote wanatembea uchi, ila wanga wanatumia astra bodies, wachawi wanatumia real bodies!.
Wanga wanawachezea tuu watu na kuwachosha bila kuwadhuru, wachawi wanawadhuru!. Wanga wanachukua astra body kuiwangia, by that time real body inakuwepo kitandani, wachawi wanahukua real bodies hivyo unaweza kurudishwa na matope!. Wanga hawawezi kushika kupiga kwa sababu wao ni astra, wachawi ndio wanaweza kupiga!, huyo aliyekupiga ni mchawi, na baaa ya kujua umemuona, alikwenda kuwaita wenzange ili wakushughulikie ikibidi wakupotezee!, walishindwa baada ya kukuta powers zako ni over and above!. Kwa lugha ya kawaida wanaita malaika wako ni imara!. Ukiongea na wazazi prefarbly mababu, watakuambia kwenye ukoo wenu you hadi a great man, hivyo vile vipawa vimekuibukia wewe!.

Just take time slowly slowly kuzicontrol at will, ukiamua kuzama kwenye dini, utafanya miujiza sana!.
Pasco.
 
Jibber jabber.
Duu, hii ni mpaka kesho nikatafute dikshenari!, hii ni shit ya nani?!, naikumbuka ile bullshit, na disjointed bullshit!,
sasa hii "Jibber jabber disjointed bullshit!" itakuwa kiboko!, kama ile bullshit ya mwanzo tunailia kwenye mchicha, ile disjointed bullshit tunailia kwenye utumbo, nadhani hii "Jibber jabber disjointed bullshit!" itakuwa ni ya kupakuliwa kabisa kwenye sahani!, tena nahisi zize yake itakuwa kama yale masoseji ma biggy! au misoseji mikubwa!.
Pasco.
 
Pasco i salute u, unaelewa haya mambo sana, binafsi i've read and tried some stuffs and i see some unusual changes, so much to explain.
Nina swali huwa lantatiza, nataka unsaidie, nmewasoma alchemists, and they relate the plant cannabis(weed) na masuala fulani kama ulioelezea ya subconscious mind meditation and stuffs like those, and i personally smoke sumtyms.
Whenever i meditate while am high inakuwa extraordinary meditation, yan nafika places ambazo sifiki nkiwa normal, pia ile kuwaza jambo kwa umakini zaidi while high. I need to know the relationship, kama upo aware na haya mambo na huu mmea, plz enlighten me.
 
Pasco kaka mzuri mie nimeusoma ahuu uzi toka jana mpaka leo nimejikuta nina maswali mengi sana kwako, hivi kwann mtu huwa anakuwa na uwezo wa ku foreseen mambo?? like mimi huwa naona kabaisaa jambo la mbele yangu lkn kama ni baya once i open my mouth and curse it halitatokea tena but if i keep silence basi latokea kwa kiwango kile kile nilichoonea.

pia ndoto zote ambazo kwangu ni successful ni zile ambazo nimeziota on negative bases, like nikiota nimefeli sana hadi nalia basi utakuta matokeo siku hivyo yatatoka na ninakuwa nimefaulu sana kupita maelezo. nikiota binti fulan ni mjamzito basi utakuta mimi ndiye mjamzito.

halafu kuna baadhi ya ndoto ambazo ni repetitive kwangu baada ya muda fulan let saya a day or two or even a week hujirudia tena lkn hizi sijaweza kuzifumbua zina maana gani.

ontop of that huwaga kama ninajifikiria kwamba nina pepo la utambuzi kwa hali hii na huwa namwomba Mungu sana aniondolee manake sidhan kama ni hali ya binadamu ya kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Hii imenisisimua kidogo..ila kaka hujawai fanyiwa matambiko utotoni labda na bibi hivi kama vile kuwekewa chale za kukulinda..!!
All in all we jasiri sana unawezaje kustahimili maono haya

mkuu hii haina cha matambiko wala nini..mimi nilikua nina uwezo wa kuona watu kama hao ila niliteseka sana na sijui hiyo ability ilipotelea wapi..
 
All in all, ushauri wangu msijaribu kwenda kufungua jicho la tatu, wengine huona raha wakidhania watakua spiderman au superman wanayemuona kwenye movie... Hii sio movie, wala si science, hakuna kitu kama science unavoona kwenye science fiction ati ubongo una initiate a certain energy inayokufanya unaona future, huu ni uchawi tu sema wajanja wameu-modernize uonekane kama science, ndio maana wakaanza kwa kuwapa movie kwanza ziwachanganye akili. There's no science in these stuffs, vyote ni uchawi tu. Don;t open the third eye maana wengi ambao wakifungua hua wana-vibrate katika frequency ndogo sasa hujikuta huona mizimu na maviumbe ya kutisha (yote majini hayo) hadi ujue kuvibrate kwa frequency ya kutosha utakua ushateseka sana... Just a warning, kama hutaki unadhani its fun basi fungua hilo jicho la tatu ukidhani utakua spiderman, utajionea madhara yake mwishoni.. n its an addiction kuliko hata madawa ya kulevya. Huu ujuzi wote subiri mbinguni tutavijua, vilifungwa hapa duniani kwa kusudi maalum

hakika.
 
Wanabodi,
Kwa kuanzia naileta tuu kwanza hii hoja hapa, ikipata watu wa kutosha, tutaomba kwa mode, ifunguliwe jukwaa lake, tutalitafutia jina muafaka, mfano, "Miujiza ya Ukweli!".

Kitu chenye nguvu kabisa katika mwili wa binadamu ni nguvu inayoitwa "Will Powers" ambayo kila binadamu, anazaliwa nayo, ila wengine wanabahatika kwa nguvu hizo kujionyesha bayana, huku wengine wengi wakiwa nazo bila kujijua kuwa wanazo nguvu hizo!.

Wale wahubiri wafanya miujiza ya uponyaji, wote wanatumia nguvu hizi, kufanya hayo wanayoyafanya, ila pia, wanga, wachawi, waganga, watabiri, wavumbuzi, matajiri wa kutisha, watawala wenye nguvu, nao pia hutumia nguvu hizi kupata mafanikio makubwa katika maisha yao!.

Matumizi ya neno "Katika Jina la Bwana", "Yesu", "Mungu" au jina lolote utakalotumia, ni kiashiria tuu cha kuufungua mlango wa nguvu hizo, ili ziweze kutenda miujiza, hata wasiotumia majina hayo, au maneno hayo huweza kutenda miujiza!.

Matumizi ya nguvu hizo, yanapotumika kutenda mema, huitwa nguvu za "Mungu", "Yesu", au "Roho Mtakatifu", na nguvu hizo zinapotumika kutenda maovu kama uchawi, majanga, magonjwa, etc huitwa "Nguvu za giza!".

Kwa vile nguvu hizi kila mtu anazo, hata hao wanaofanya miujiza ya uponyaji, wanachofanya ni kufungua tuu milango, ili nguvu zilizo ndani yako, ziweze kutenda hiyo miujiza, na ukipona, kilichokuponya sio huyo mponyaji, wala lile jina la Yesu, au jina Mungu, bali ni nguvu zilizo ndani yako!, "the powers from within!".

Hatua ya kwanza ya kufungua nguvu hizi ni "imani" kuamini kuwa "you have the powers" and that "you can do anything!", or "you can be anybody". Kuamini Mungu, Yesu, Mtume, Allah, Roho Mtakatifu, Bikira Maria, Watakatifu, Wachungaji, Wahubiri, Baba Mtakatifu, Sangoma, Sheriffu, Mlingotini, Chini ya Mti, Chini ya Mbuyu, Mlimani, Pangoni, Kisimani, Mtoni, Ziwani, Kwa Mganga, Vitabu Vitakatifu etc, ni njia rahisi ya kuanzia kufungua milango ya "higher power" to open up your doors for powers from within!" to act on you for you!.

"I know I can, be what I wanna be!"

Wale wenzetu wajanja, waliojitambua kuwa wanazo, wengi wanazitumia kutengezea mapesa kwa kisingizio chochote kiwe ni cha wahubiri, waganga, "wazee wa busara", "watenda miujiza", "wafukuza mapepo" kwa kukusanya sadaka na kujitajirisha, ambao mimi naita ni "wizi mtupu", huku waumini wakendelea kukamuliwa na kuachwa katika umasikini uliotopea!.

Nguvu hizi zimegawanyika matika makundi mengi tofauti, hivyo nimekuwekea baadhi ya makundi hapa chini, just take your time kuyatambua, ujiangalie na wewe unazo nguvu zipi, ili sasa uzitumie nguvu hizo, to "make things happen!".

This is a list of psychic abilities that have been attributed to real-world people. These are also sometimes known as extrasensory perception or a sixth sense. Inclusion in this list does not imply scientific recognition of the existence of an ability. Superhuman abilities from fiction are not included.


Psychic Powers- Ni Nguvu za Kufanya Miujiza-Wengi Wanazo Bila Kujitambua!-Jee Wewe Unazo?!,
Take time kujitambua kuwa you have the powers,
Nitakusaidia website za kukuelekeza ufanye nini kuhusu hizo powers ulizo nazo zikuletee mafanikio!.
Watu wote wenye mafanikio, wameisha jitambua, ila wengi wanafanya siri!.

Hii ni fursa kwa wewe kujitambua, kuzitumia powers ulizo nazo, kubadili maisha yako!.

Karibu tujadiliane!.

Pasco.
Pasco mimi kuna hii kitu huwa inanitokea ninapokuwa nimekaa na mtu let say kiti kimoja, tumegusana either miguu au mikono,nilichogundua ni kwamba ninapokuwa aware kuwa huyu mtu tumegusana naye tena mahali fulani let say kwenye mguu,nikifanya concentration ya pale tunapogusana unakuta yule mtu kama vile nimepeleka taarifa kuwa tumegusana pale mahali,naye utakuta kama ilikuwa kwenye mkono au mguu au paja utaona anasogeza mguu kuashiria kuwa naye ame notice pale tulipogusana.Sasa hii nayo tunaiwekaje kwenye hizo powers,jingine ni kuwa jambo fulani linatokea najikuta kuwa hili jambo au tukio nilishawahi kuliota before halijatokea yaani unakuta mpaka najua litaishaje na linakuja kuishia vilevile,hii imeshanitokea mara nyingi sana.Pls nipe ufafanuzi hii nayo ni nini?
 
Last edited by a moderator:
i' had already open third eye and close that ernegy with rituals bath successifull but i dont suggest any to do that

Chief, nilimsoma Samuel Sagan MD na kitabu chake cha Awakening the Third Eye... I agree with you activation ya Pineal gland/third eye/Ajna Chakra can be dangerous. Nawaona wale curious chaps wanataka kuifungua hii kitu.I opted not to practise.
 
kaka Pasco nimekufuatilia huu uzi mwanzo mwisho, nimejifunza mambo mengi sana na mimi nimekua interested kujua what is within me, ngoja nianze kuyatafuta haya maarifa ktk baadhi ya vitabu vilivyoainishwa na baadhi ya wadau ktk comments zilizopita
 
Last edited by a moderator:
Chief, nilimsoma Samuel Sagan MD na kitabu chake cha Awakening the Third Eye... I agree with you activation ya Pineal gland/third eye/Ajna Chakra can be dangerous. Nawaona wale curious chaps wanataka kuifungua hii kitu.I opted not to practise.

i' had already open third eye and close that ernegy with rituals bath successifull but i dont suggest any to do that

Sasa jamani nyie mnaojua THE BAD SIDE ya haya mambo tujuzeni basi..maana inakua ka mnatutisha pasipo kutupa picha iliyowazi..mi naamini mnania nzuri ya kutukinga na matatizo ila fungukeni basi.. Pasco ye kafunguka kwa kirefu mpaka katujaza wengi wetu hamu ya kutaka kuyajua haya mambo kwa ukaribu ka mnavyoona watu wanavyotoa shuhuda zao afu ni kawaida ya wanadamu kutaka kujifunza mambo mapya.
All in all tusaidieni nyie mnaoyajua haya mambo tusije kujiletea mabalaa maishani.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu MpiganiaUhuru naomba unijibu haya maswali yangu mawili la kwanza hili
(1)Unapouacha mwili wako huwa unaenda wapi na unatumia mwili upi tofauti na huo uliouacha hapo ulipokuwepo kabla ya kujinyofoa ndani ya huo mwili.
(2)unapouacha barabarani watu wanauona au hauonekani na magari yakipita hayaugongi huo mwili?
Mimi ninazo 2:
  1. Astral projection: Nimewahi kuhama kutoka ndani ya mwili wangu kama mara 2 hivi, moja ni pale nilipokuwa natembea barabarani halafu nikajaribu kuhama kutoka kwenye mwili, nilipourejea nikaukuta umelala chini kwenye vumbi katikati ya barabara, sikufurahia tendo hilo zaidi ya kuogopa! Pili, ni pale nilipokuwa nimekaa kwenye kiti nikisikiliza mziki laini na kujaribu kuzama kwenye huo mziki na kuuacha mwili wangu ambao baadaye nilijikuta nimelala sakafuni!
  2. Hii ya pili bado sijaijua jina au haipo kwenye list hapo juu: Nina uwezo wa kuwaona watu walio uchi ambao wenzangu huwa hawawaoni kila ninapojaribu kuwaonesha, wamefikia mahali wanadhani mimi ni mchawi!

Nimeipenda mada hii, nadhani ni ukweli mtupu ingawa inaweza kuonekana kituko kwa wengine!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom