........Wale wahubiri wafanya miujiza ya uponyaji, wote wanatumia nguvu hizi, kufanya hayo wanayoyafanya, ila pia, wanga, wachawi, waganga, watabiri, wavumbuzi, matajiri wa kutisha, watawala wenye nguvu, nao pia hutumia nguvu hizi kupata mafanikio makubwa katika maisha yao!.
Matumizi ya neno "Katika Jina la Bwana", "Yesu", "Mungu" au jina lolote utakalotumia, ni kiashiria tuu cha kuufungua mlango wa nguvu hizo, ili ziweze kutenda miujiza, hata wasiotumia majina hayo, au maneno hayo huweza kutenda miujiza!.
Matumizi ya nguvu hizo, yanapotumika kutenda mema, huitwa nguvu za "Mungu", "Yesu", au "Roho Mtakatifu", na nguvu hizo zinapotumika kutenda maovu kama uchawi, majanga, magonjwa, etc huitwa "Nguvu za giza!".
Kwa vile nguvu hizi kila mtu anazo, hata hao wanaofanya miujiza ya uponyaji, wanachofanya ni kufungua tuu milango, ili nguvu zilizo ndani yako, ziweze kutenda hiyo miujiza, na ukipona, kilichokuponya sio huyo mponyaji, wala lile jina la Yesu, au jina Mungu, bali ni nguvu zilizo ndani yako!, "the powers from within!".
Hatua ya kwanza ya kufungua nguvu hizi ni "imani" kuamini kuwa "you have the powers" and that "you can do anything!", or "you can be anybody". Kuamini Mungu, Yesu, Mtume, Allah, Roho Mtakatifu, Bikira Maria, Watakatifu, Wachungaji, Wahubiri, Baba Mtakatifu, Sangoma, Sheriffu, Mlingotini, Chini ya Mti, Chini ya Mbuyu, Mlimani, Pangoni, Kisimani, Mtoni, Ziwani, Kwa Mganga, Vitabu Vitakatifu etc, ni njia rahisi ya kuanzia kufungua milango ya "higher power" to open up your doors for powers from within!" to act on you for you!.
"I know I can, be what I wanna be!"