Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

nilisoma watu wakikuita DR,nimesoma michango yako kwenye nyuzi nyingi.wewe ni aina ya mtu ningekujua nje ya JF ningekukwepa kama ukoma.

Kijana. Mwenye tabia ya kumkimbia daktari basi maradhi yatamdhuru!
We hutakiwi kunikimbia. Bali km una matatizo na ninayo andika leta hoja zako jukwaani tujadili.

Wanasema "dont hate the game! Hate the player"

Mi mbona ni mtanzania wa kawaida tu! Unaniogopa kwa nini!?
 
kwanza sikuogopi kwa chochote kile.ila ninapotambua mtu ana mawazo "MFU" halafu hajitambui huwa namkwepa na wala si kumuogopa. Nimekusoma kwenye nyuzi nyingi ni aina ya mtu unayeishi kwa uliyokariri. Sio kila mtu dini ni kama ngozi,kuna watu wanazitazama dini kama kitu cha nje,kama mtu anavyotazama mpira au siasa.
 
kwa hiyo wachawi tunaoskia wanapaa na ungo, ni kweli?.....na hiyo nguvu yao inakuaje au inatokeaje?
 
Katika Quruan Mwenyezi Mungu anasema yeyote mwenye kwenda kinyume na mafunzo ya Mtume SAW na akafuata njjia isiokuwa ya waumini basi tutamuongoza kulekule anakotaka. Maneno haya ya Mungu yanaamanisha kwamba mtu akiacha njia sahihi ya kuamina ambayo kwa mujibu wa aya ni uislamu aliokuja nao Muhhamad SAW Mungu atakachokifanya ni kuongoza na kumfanikisha kulekule iman yake inakoegemea.Utaona wazee wetu wwa zamani waliokuwa na ibada za jadi walikuwa wakiomba shida zao kupitia njia mbalimbali kama mizimu,mapango,miti mikubwa n.k na walikuwa wanafanikiwa maombi yao pamoja na kwamba walitumia njia isio sahihi,hii ni kwa sababu ya iman yao kuwa watafanikiwa kupitia mizimu/njia hiyo. Na alichokifanya Mungu ni kuwafanikisha maombi yao kupitia njia isio sawa kama alivyoahidi katika aya hapo juu.
Mungu kupia aya nyigine ndani ya Quran ameeleza kuwa kuna watu hupata ufunuo wa mambo kupitia yeye mwenyewe kama alivyofanya kwa mitume na waja wema. Lakini pia kuna wengine watapata ufunuo kutoka kwa shetan na habari hizi watakazo funuliwa na shetani zitakuwa na ukweli ndani yake na uongo mwingi.Mifano ni habari za waganga wa kienyeji. Kwahiyo mimi nakubaliana kwa upande flani na Pasco juu ya uwepo wa nguvu hizo tofauti ni kwamba kuna zitokanazo na Mungu na nyingine na shetani.
 
Last edited by a moderator:
Unakubaliana na mimi kuwa kwa mujibu wa Biblia ulichoandika ni uongo mweusi kabisa?

Nimejaaliwa na nani kama wewe unaamini Biadamu ni miungu yaani wana "power within"?

Pasco ukishasema wewe ni Mkristo unakuwa subject chini ya Biblia. Huwezi kwenda below au above Biblia bado ukabaki kuwa Mkristo. Huwezi kufundisha mafundisho ya shetani haya ukabaki kujiita Mkristo. Sijui kuhusu Ukatoliki unaosema wewe ni mkatoliki sana kuweza kusema watakuja wakatoliki waseme, lakini kwa Ukristo wa Biblia, wewe sio Mkristo!
Nasema hivi kwa kuwa kama nilivyoonesha hapo juu Biblia inapinga mambo haya na huwezi kuwa Mkristo ukafundisha ushetani huu, let alone kuuamini!

Kwa mabandiko yako nikusaidie tu wewe sio mkristo, wewe ni aidha Mhindu au Mwana vuguvugu la kizazi kipya (New ager) basi. Haya ndiyo unayofundisha. Na hii ni dini aliyoiasisi shetani mwenyewe na ndio "mungu" unayemfundisha hapa. Well shetani ana nguvu zake na watakaojaribu unayofundisha wataonja joto ya jiwe lakini usijifanye unafundisha nguvu ya Mungu.

Unafundisha mafundisho ya Ibilisi kabisa na kwa kuwa wote wanaosoma wameonywa, atakayejaribu akakiona hatakuwa na wa kumlaumu!

Najua una maana gani kwa imani yako ya New agers. Uje utufafanulie na Yesu wako feki "Ascended Master Jesus" ili uunganishe vizuri na musa bandia na miaka bandia ya Yesu ako bandia ambayo "inakosekana" katika Biblia.

I know all these, they are dangerous poison wrapped in iced cake!

Stephano, nakutafutia muda nikujibu, kwa sasa naacha kwanza hawa "vichaa" watulie, tukiendelea mwisho wa siku wote tutaonekana vichaa!, nilisisitiza sana, kuwa kichaa mtu sio lazima mpaka aokote makopo!, watu mnajibishana na vichaa humu hadi thread kutaka kupoteza lengo!, the more mnawajibu, the more vichaa vinawapanda!.

Hilo la powers za Uuungu ndani yetu na meditation kwenye Bible, nimekuwekea mpaka vifungu!, ila unapoamua kukaa ndani ya box, limits zako ni kuta tuu za box, ilimomo, anything out of the box ni devilish!. Nimekuuliza Yesu aliishi wapi toka akiwa na umri wa miaka 12 hadi 30?, na alifanya nini?!, hutaweza kujua kwa sababu ndani ya box lako ulimo, haipo!.

Kama ambavyo huthubutu kujua mwanzo wa Mungu ni nini na source hizo powers za Mungu ni nini!, usijisumbue kumjua shetani ni nani, mwanzo wake ni upi na sources za powers zake ni nini!, kama shetani alidiriki hadi kumchukua Mwana wa Adamu na kumjaribu!, who are you?!. Unajua kuna wakati shetani anaji disguize kama Mungu, na kuna wengi mnamtumikia shetani bila kujijua mkidhania mnamtumikia Mungu!, ili kuweza kumtenganisha Mungu na shetani, you need enlightment!, hii enlightment ndizo powers ninazozizungumzia, jitambue USIDANGANYWE WALA USIDANGANYIKE!.
Pasco.

kwa hiyo wachawi tunaoskia wanapaa na ungo, ni kweli?.....na hiyo nguvu yao inakuaje au inatokeaje?
Tall gal, hizo habari za kupaa, ni kweli kabisa, ila sio kula kupaa ni kwa uchawi, wala sio kila kupaa ni kwa kutumia ungo!.

Kuna kupaa kwa aina 4,
1. Kwa vile mwili wetu una sehemu kuu 2, yaani mwili na roho, (physical body na spiritual body/astral). Aina ya kwanza ni pale physical body inapolala, spiritual body inaamka. Wewe unajiona kama vile ulikuwa unaota, kumbe haikuwa ndoto bali spiritual body ilipaa na kuyashuhudia hayo uliyoshuhudia, kisha ikarudi na kujiunga na physical body. Ila kesho utakapoamka kama jana yake uliona msiba, ajali, tukio au hatari yoyote, na kesho yake ukapokea taarifa kitu fulani kilitokea, wewe ukakumbuka kama uliota, in fact hukuota, spiritual body ilitoka ikaona. Hili humtokea kila mtu, ila tatizo ni communication kati ya spiritual body a physical body ni ndogo kwa wengi wetu, hivyo hubakizi kumbukumbu yoyote, wachache wenye kumbukumbu, watakuambia kuna vitu waliota na vikatokea. Kupaa huku ni normal na sio uchawi!. Kupitia mazoezi, unaweza kukucontol kupaa huku at will, na kuiacha physical body yako mahali na spiritual body ikatoka na kwenda popote!. Hii ndio hiyo inaitwa Astral projection or mental projection - An out-of-body experience in which an "astral body" becomes separate from the physical body.

Kiendo cha kutoka point A hadi point B mfano Dar-New York, kinachukua muda mrefu kwa sababu ya mass, distance and time, mass ni uzito wako, distance ni umbali na time ni muda kutoka point A to point B. Kwenye ulimwengu wa roho, hakuna mass, distance wala time!, ukithink NewYork, in a split of a second, uko New York, the next second, Tokyo, the next popote utakapofikiria tuu just by blink, utakuwepo!. Kule miaka 1000 ni kana siku moja na siku moja ni kama miaka 1000!. Hivi ndivyo wanavyoisafiri malaika, au wale watu wanaotokewa na mizimu, Yesu, Malaika na Watakatifu. Hatua hii ya kupaa pia huwakuta binadamu wote wakati roho inaacha mwili!.

2. Kupaa kwa pili, ni kupaa kwa levitation, ambapo unapaa na mwili wako jumla kama Yesu ilivyopaa, Bikira Maria, Musa, Eliya na wengine walio palizwa. Hii levitation kufanyika kwa ku change body frequency inakuwa iko lighter than gravitational force inayotupull down, hivyo unaelea hewani. Hii pia inafanywa kwa mazoezi na sio uchawi!. Marshal arts zote zinafundisha hii kitu, wale ma ninja, wanapigana mpaka hewa na kuvanishi into thin air in a split of a second, wanatumia hii change of body vibration at will, hivyo normal sense za uoni hazimuoni, kisha kuruka sehemu nyingine.
Hata ukiangalia feni wakati ikianza kuzunguka, utaona panga boy zikizunguka, ikishika kasi kubwa hutaona tena pangaboi utaona tuu mviringo wa kama upepo!. Kikundi cha sectet society cha Rosecrusians, wanafundishwa technick hii sambamba na jamaa wa kule Tibet, wanao wanachapa miguu kama wanatembea haraka, lakini kiukweli wanapaa, miguu haigusi juu ya ardhi, na huwezi kutembea juu ya maji kama aliyokua akifanya Yesu!. Kumezungumzwa hapa Transvection - Bodily levitation or flying.

3. Kundi la tatu ni la wanga, hawa pia wanapaa kwa lengo la kuwawangia tuu watu, japo wanga wanatumia uchawi kuwanga, lakini hawana madhara kwa sababu nao pia wanaishi kwenye spiritual world ya nguvu za giza kwa lengo la umbea tuu kuona watu wanafanya nini usually usiku, hupenda tuu kuwaangalia watu kwenye faragha zao na kuangalia senema za bure atc, lakini hawana any physical harm kwa sababu wana deal na spiritual body yako. Kwenye kundi hili, mapemo pia wapo, majini yapo na mashetani yapo!. Ukichukuliwa na wanga, wanachukua tuu spiritual body na physical body inaachwa imejilalia!.

4. Kundi la mwisho ni la wachawi!, kiukweli hawapai kwa ungo, ila ila huo ungo unatumiwa kuzugia tuu, wanajipaka mafuta fulani ya kichawi yaliyotengenezwa kwa mafuta ya binaadamu!, hawa ndio wanaopaa na miili yao kiukweli, na kujikusanya kucheza ngoma za kichawi, kufukua makaburi na kula maiti na kufanya mambo mengine mengi ya kichawi.
lengo kuu la uchawi ni matumizi ya nguvu za giza kufanya destruction na mara nyingi yanahusisha kafara za watu, tena mara nyingi hutakiwa kumtoa mpendwa wako!. Wako matajiri kibao, ama wamewatoa kafara wapendwa wao ama wanaishi na ndondocha ndani ya familia zao ili kupata utajiri kwa nguvu za giza!. Mambo ya uchawi yamezungumzwa sana hapa Esoteric/Occult , Evil, Alchemy, Shamanism, Neopaganism/Wicca.
Warning!. Please just read to gent info!, and don't ever try any of these! kwa sababu zinahusisha nguvu za giza, kujaribu kufanya chochote kati ya haya ni kukubali kumtumikia shetani!.
Ushauri! Kama wewe umesoma mafundisho ya kitabu kimoja tuu cha dini yako!, nakushauri achana kabisa na kufungua hizo links, ili udumu na kuwa imara kwenye dini yako!. Nimeziweka ili wale ambao wako tayari to get the knowlwgw kuujua ukweli zaidi ya ule waujua, ndio wawe informed, wele wangine, tudumu tuu katika kile tulichofundishwa na viongozi wetu wa dini tunaowaamini.

Naendelea kusisitiza Pasco wa JF ni Mkristo Mkatoliki Die Hard!, nayaweka haya wazi, ili muweze kubainisha nguvu za mwanga za kufanya meme, na kuzibaini nguvu za giza zinazofanya uovu!.
Pasco
 
Pasco, hii mada naiunga mkono. Nimesoma nguvu zako ulizotaja. Siko deep kivile ila zote ulizonazo ninazo.
Nimetenda mambo makubwa sana na sasa nimeamua kuokoka ili kutumia nguvu hizo kwa manufaa ya jamii.
Naweza pia kusaidia kueleza jinsi ya kuzitumia.

Kesho ijumaa nitakonfirm a new miracle, then nitaeleza hapa hapa.
You are, who you are, asante, tunakusubiria!. Ila pia ni kweli nguvu zangu sio kivile, na matumizi yake hayakuwa ya maana kiasi kwamba karma imenishugulikia na hivi ninavyoandika bado niko kwenye mapito ya kufidia niliyoyatenda nyuma!.
Pasco
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.

mkuu nimeipenda comment yako. najua pasko ameleta uzi kutusaidia tufikiri tofauti though haya mambo yanapingana na imani zetu, kiasi wamba ni rahisi kupata bash kwa fundamentals. kiufupi naona pia hata hii ya kuzijua hizi nguvu ni aina ya imani pia kama zile nyingine na za kwetu, nimewahi kupata rafiki aliyejaribu kunishawishi niwe member wa hii cult ya meditation na kunielezea mambo mengi ikiwemo binadamu anamiili saba, na mambo ya kula vegetable na kuacha nyama na pombe, ku-meditate.mfano wanasema mungu yupo lakini hafanyi chochote katika watu na hata mkifa watu milioni ni sawa tu hakuna kinachoharibika bali mnakuwa mmeamia kwenye mfumo wenye nature nyingine. kimsingi imani yao ni ya ajabu sana.
japo ningeomba kujua uliona unabadilika kitu gani hapo mkuu. kwakuwa imani hii ya meditation inasemekana ukiifuata unaachana na imani yako ya kawaida hapo baadae. na nijuavyo imani hii ipo tanzania na ndiyo naelewa pia inatumia hii mifumoo ya kuzikusanya nguvu za asili kwa namna ya meditation.
 
Pasco, hii mada naiunga mkono. Nimesoma nguvu zako ulizotaja. Siko deep kivile ila zote ulizonazo ninazo.
Nimetenda mambo makubwa sana na sasa nimeamua kuokoka ili kutumia nguvu hizo kwa manufaa ya jamii.
Naweza pia kusaidia kueleza jinsi ya kuzitumia.

Kesho ijumaa nitakonfirm a new miracle, then nitaeleza hapa hapa.

Mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo.
 
Stephano, nakutafutia muda nikujibu, kwa sasa naacha kwanza hawa "vichaa" watulie, tukiendelea mwisho wa siku wote tutaonekana vichaa!, nilisisitiza sana, kuwa kichaa mtu sio lazima mpaka aokote makopo!, watu mnajibishana na vichaa humu hadi thread kutaka kupoteza lengo!, the more mnawajibu, the more vichaa vinawapanda!.

Kuna ka ukweli hapa
Hilo la powers za Uuungu ndani yetu na meditation kwenye Bible, nimekuwekea mpaka vifungu!, ila unapoamua kukaa ndani ya box, limits zako ni kuta tuu za box, ilimomo, anything out of the box ni devilish!. Nimekuuliza Yesu aliishi wapi toka akiwa na umri wa miaka 12 hadi 30?, na alifanya nini?!, hutaweza kujua kwa sababu ndani ya box lako ulimo, haipo!.
Pasco,
Kuna mambo ambayo hata ukijua hayana msaada kwako,kujua Yesu alifanya nini kuanzia alipokuwa na miaka 12 mpaka 30 hakuna maana yoyote
Hakuna maana yoyote kwakuwa kuja kwa Yesu kulikuwa na lengo maalum na lengo hilo hakulifanya akiwa na umri huo hivyo hakukuwa na sababu ya kurekodi maisha yake wakati huo

Hivi ni kwanini hujiulizi ni kwanini maisha yake yasiandikwe kwa kipindi hicho lakini alipofikia umri wa miaka 30 yaandikwe?
Kama yaliandikwa kabla ya hapo naomba utuambie ni wapi na impact yake ni nini,sio kutaka vitu visivyokuwa na maana ilimradi tu umejua
Huko ni kupoteza muda
Kama ambavyo huthubutu kujua mwanzo wa Mungu
Kwanza acha ku assume mambo
Amekuambia wapi hajathubutu?

Halafu pia
Unamjua Mungu ni nani/nini?
Akiwa na mwanzo anakuwaje Mungu?

Lets say mungu ana mwanzo
Unadhani utaweza kuujua?
Ni sawa na gari litake kumjua aliyelitengeneza
Litaweza kweli?
ni nini na source hizo powers za Mungu ni nini!
Brother,
Unataka kusema wewe unazijua mwanzo wake?
Hebu tuambie ni nini na utapewa tuzo ambayo hakuna binadamu aliyepewa tangu Adam
Na hakika ukiweza kujua wewe ndio utakuwa ndio Mungu kwakuwa ukishajua chanzo cha hizo nguvu za Mungu hawezi kuwa Mungu tena
, usijisumbue kumjua shetani ni nani, mwanzo wake ni upi na sources za powers zake ni nini!,
Haya tunayajua
Hakuna kipya hapo,wala hatujisumbui
kama shetani alidiriki hadi kumchukua Mwana wa Adamu na kumjaribu!, who are you?!.
Hivi wewe ni Mkristo kweli?
Kama ungekuwa ni Mkristo wala hili swali usingejiuliza kwasababu majibu yake kwenye maandiko
Au hata Yesu hujui ni nani?
Unajua kuna wakati shetani anaji disguize kama Mungu, na kuna wengi mnamtumikia shetani bila kujijua mkidhania mnamtumikia Mungu!
Kama sisi kwa kushindwa kufikiri kwetu tunamtumikia shetani bila kujua wakati maandiko yanazungumza kwa uwazi mkubwa tatizo ni la nani?
, ili kuweza kumtenganisha Mungu na shetani, you need enlightment!,
What enlightment?
Hizi ulizoziandika hapa?
Kama ni hizo hapana

Hakuna njia nzuri ya kuweza kumtofautisha Mungu na Shetani tofauti na maandiko matakatifu ya Biblia
Sifa za Shetani zimeelezwa humo na sifa za Mungu zimeelezwa humo na hata jina la Mungu limeelezwa humo

Bila kukitumia hicho kitabu huwezi kumtofautisha kwa sababu kuna wakati nae anajiita mungu ndio maana kuna watu wanamuabudu shetani na kujidanganya kuwa ni mungu
hii enlightment ndizo powers ninazozizungumzia, jitambue USIDANGANYWE WALA USIDANGANYIKE!.
Pasco.
Kwanini kama ni hizo zinakwenda kinyume na maandiko matakatifu?
 
Occult powers zipo nane,
astral travelling,clairvoyance,telepathy with animals,viewing the akashic record,psychometry,telepathy with humans,ability to know when and how you will die,

halafu zipo eight yoga powers,kama anima,etc,
 
Kuna ka ukweli hapa

Pasco,
Kuna mambo ambayo hata ukijua hayana msaada kwako,kujua Yesu alifanya nini kuanzia alipokuwa na miaka 12 mpaka 30 hakuna maana yoyote
Hakuna maana yoyote kwakuwa kuja kwa Yesu kulikuwa na lengo maalum na lengo hilo hakulifanya akiwa na umri huo hivyo hakukuwa na sababu ya kurekodi maisha yake wakati huo

Hivi ni kwanini hujiulizi ni kwanini maisha yake yasiandikwe kwa kipindi hicho lakini alipofikia umri wa miaka 30 yaandikwe?
Kama yaliandikwa kabla ya hapo naomba utuambie ni wapi na impact yake ni nini,sio kutaka vitu visivyokuwa na maana ilimradi tu umejua
Huko ni kupoteza muda

Kwanza acha ku assume mambo
Amekuambia wapi hajathubutu?

Halafu pia
Unamjua Mungu ni nani/nini?
Akiwa na mwanzo anakuwaje Mungu?

Lets say mungu ana mwanzo
Unadhani utaweza kuujua?
Ni sawa na gari litake kumjua aliyelitengeneza
Litaweza kweli?

Brother,
Unataka kusema wewe unazijua mwanzo wake?
Hebu tuambie ni nini na utapewa tuzo ambayo hakuna binadamu aliyepewa tangu Adam
Na hakika ukiweza kujua wewe ndio utakuwa ndio Mungu kwakuwa ukishajua chanzo cha hizo nguvu za Mungu hawezi kuwa Mungu tena

Haya tunayajua
Hakuna kipya hapo,wala hatujisumbui

Hivi wewe ni Mkristo kweli?
Kama ungekuwa ni Mkristo wala hili swali usingejiuliza kwasababu majibu yake kwenye maandiko
Au hata Yesu hujui ni nani?

Kama sisi kwa kushindwa kufikiri kwetu tunamtumikia shetani bila kujua wakati maandiko yanazungumza kwa uwazi mkubwa tatizo ni la nani?

What enlightment?
Hizi ulizoziandika hapa?
Kama ni hizo hapana

Hakuna njia nzuri ya kuweza kumtofautisha Mungu na Shetani tofauti na maandiko matakatifu ya Biblia
Sifa za Shetani zimeelezwa humo na sifa za Mungu zimeelezwa humo na hata jina la Mungu limeelezwa humo

Bila kukitumia hicho kitabu huwezi kumtofautisha kwa sababu kuna wakati nae anajiita mungu ndio maana kuna watu wanamuabudu shetani na kujidanganya kuwa ni mungu

Kwanini kama ni hizo zinakwenda kinyume na maandiko matakatifu?
Mkuu Royer, niko kwenye mobile nakutafutia muda nitakujibu hoja kwa hoja nikianzia na hili la Yesu. Lengo la historia ni kuyajua yaliyopita, kulinganisha na yaliyopo sasa ili kujua yajayo!.

Katika Biblia Takatifu Maisha ya Yesu tangu kuzaliwa, hadi Kifo, yameandikwa katika vitabu vya zile Injili 4. Kuna gap tangu a lipokuwa miaka 12-30, sio kuwa details zake hazipo ziliandikwa bali compilers waliamua wasiyawe for a porpose!, sambamba na private life yake katika kipindi cha île miaka mitatu ya utume wake.

Kwa vile details hizo zimeachwa kwa makusudi ili zisisomwe lakini zipo na ziliandikwa, naomba mimi ni site ndio chanzo cha kukueleza yaliyo nje ya Biblia ili only wenye quest for information outside the box ndio waitafute.

Sambamba na mwanzo wa Mungu na source of Godly powers ambazo na sisi bunadamu tumepewa, ila kitu kimoja ambacho wengi hamkijui ni kuwa Mwanzo wa Mungu ndio huo huo mwanzo wa shetani!, Mungu hakumuumba shetani!.

Mungu ana nguvu zaidi ya shetani, ila shetani naye ana nguvu ambazo amepata kibali cha kukitumia kwa wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu na nguvu za ufunguzi!, na alianzia kukitumia kwa Adam na Eva kuwashauri kumuasi Mungu kwa kumega lile tunda!.

Mungu ni omniprésent so does shetani. Yumo ndani yetu in a form of power!.
Kubali,kataa!.
Pasco
 
Mkuu Royer, niko kwenye mobile nakutafutia muda nitakujibu hoja kwa hoja nikianzia na hili la Yesu. Lengo la historia ni kuyajua yaliyopita, kulinganisha na yaliyopo sasa ili kujua yajayo!.
Kwanza mimi sio Royer ni Eiyer
Halafu unapokuwa unazungumzia mambo ya kiimani unatakiwa ujue ni tofauti na unaposoma historia shuleni
Ukijua hiyo tofauti ndipo utajua ni kwanini kuna mambo hayapo kwenye Biblia
Katika Biblia Takatifu Maisha ya Yesu tangu kuzaliwa, hadi Kifo, yameandikwa katika vitabu vya zile Injili 4. Kuna gap tangu a lipokuwa miaka 12-30, sio kuwa details zake hazipo ziliandikwa bali compilers waliamua wasiyawe for a porpose!, sambamba na private life yake katika kipindi cha île miaka mitatu ya utume wake.
Kwanza haya ni mawazo yako binafsi hivyo hatuwezi kuyachukulia serious
Pili unajua biblia iliandikwa kiaje na kwa nguvu gani?
Haya unayoyaleta hapa yapo kinyume na ukristo kabisa
Kwa vile details hizo zimeachwa kwa makusudi ili zisisomwe lakini zipo na ziliandikwa, naomba mimi ni site ndio chanzo cha kukueleza yaliyo nje ya Biblia ili only wenye quest for information outside the box ndio waitafute.
Haya mambo sijui mnayatoa wapi
Inamaana Mungu alishindwa kulilinda neno lake ambalo alisema halitapita kamwe?
Ndio maana nakuambia wewe uko kinyume kabisa na ukristo
Hizi hoja ni za Waislam na wale wasioamini uwepo wa Mungu
Sambamba na mwanzo wa Mungu na source of Godly powers ambazo na sisi bunadamu tumepewa, ila kitu kimoja ambacho wengi hamkijui ni kuwa Mwanzo wa Mungu ndio huo huo mwanzo wa shetani!
Siongezi neno hapa umejidhihirisha sasa kwa uwazi kabisa kuwa wewe ni nani
Nimwehu tu atakaekubaliana na wewe kuwa Mungu na shetani ni uleule
, Mungu hakumuumba shetani!.
Khaaaaaa!!!!!!!!!!!!!
Mliokuwa mnatusakama kuwa tunamhukumu kwa kumsema huyu mtu sio mkristo sasa mnajionea wenyewe
Mungu ana nguvu zaidi ya shetani, ila shetani naye ana nguvu ambazo amepata kibali cha kukitumia kwa wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu na nguvu za ufunguzi!, na alianzia kukitumia kwa Adam na Eva kuwashauri kumuasi Mungu kwa kumega lile tunda!.
Well,
Kwanini shetani nguvu zake ni kidogo kuliko Mungu kama Mungu hahusiki na mwanzo wa shetani
Hizo nguvu za shetani alizitoa wapi?
Hicho kibali cha kuzitumia hizo nguvu alikitoa wapi?
Mungu ni omniprésent so does shetani. Yumo ndani yetu in a form of power!.
Labda yupo ndani yako wewe
Lakini kwangu hapana
Kubali,kataa!.
Pasco
Nakataa!
 
Back
Top Bottom