Mkuu Pasco heshima kwako kwa kurudi tena nimefatilia uzi huu tangu mwanzo swali langu ni hili shetani ana nguvu lakini mungu ana nguvu zaidi kwanini mungu asimuangamize shetani? maana maovu yote ni shetani na ana mbinu nyingi unaweza kuwa unamtumikia bila kujua ina maana mungu anafurahia maovu wakati anajua chanzo ni shetani na hili analijua hata kabla ya uumbaji.
Mkuu chaUkucha, hili swali lako liliwahi kuleta ubishani mkubwa sana huko nyuma kwenye topic haswa haswa kutoka kwa wale niliowaambia ni waumini vitabu, waumini maandiko.
Kama nilivyosema mwanzo, mwanzo wa Mungu ndio huo huo mwanzo wa shetani, source ya powers za Mungu, ndio hiyo hiyo source ya powers za shetani, Mungu ana powers zaidi ya shetani, ila hawezi kumuangamiza shetani as of now!, labda mpaka ile siku ya mwisho ambayo Mwana wa Adamu atakaporudi tena!.
Uwezo wa Mungu kwa sasa ni ama kumzuia shetani, asifanye uovu, au kutibu na kuponya uovu uliofanywa na shetani, au kumfukuza shetani na mapepo kutoka kwa watu wa mungu na sio kumteketeza!.
Wahubiri wote watoa mapepo, mwisho wa uwezo wao ni kufukuza tuu, na sio kumuangamiza shetani!.
Ikumbukwe hapo mwanzo Mungu na shetani walikuwa kitu kimoja, Mungu akiwa na madaraka zaidi, shetani akiwa the 2nd in command!. Ugomvi wa Mungu na shetani ni tamaa ya shetani, yeye ndie awe top in command hivyo akaorganize uasi kule mbinguni, malaika wamuasi Mungu, wamsikilize shetani!. Baadhi ya malaika walikubali na wengine walikataa kuaai, hivyo vikapiganwa vita kuukati ya malaika watiifu na malaika waasi, malaika watiifu wakashinda hivyo shetani na genge lake wakatimuliwa mbinguni, wakatupwa kuzimu, duniani kwenyejehanum ya milele!.
Mungu akaiwa na Neno, na Roho Mtakatifu, wakasemezana "na tujiumbie kiumbe kitakacho tutii" tuumbe binadamu kwa mfano wetu!. Mungu akamuumba binadamu Adamu kwa mfano wake akampa na nguvu ya uungu!. Adamu aliishi peke yake for sometimes! na kisha ndio Mungu akaona sii vema binadamu aishi peke yake, akamuumbia msaidizi Eva!.
Shetani akayaona mema yote aliyokuwa akiyafanya, na kwa kupoitia omni presence yake, shetani akamuibukia Mungu na kufanya nae majadiliano kuhusu utii wa binadamu!.Shetani akamwambia Mungu, huwezi kuupima utii wa kiumbe chako bila kukitengenezea kishawishi, tengeneza kishawishi kwa kumwambia hiki fanya na hiki usifanye, ili kumpima utii wake.
Japo haikuandikwa popote, ule mti wa mema na mabaya, mema ndio mpango wa Mungu na mabaya ni mpango wa shetani!.
Ndipo Mungu akauweka ule "mt" wa katikati na tunda, mti wa mema na mabaya!, na kuwaamuru binadamu wanaweza kula matunda kutoka miti yote, ila wasithubutu kula matunda toka mti wa katikati ni hakika watakufa!. By now naamini umeishafahamu i huo "mti" wa "katikati" ambao ni "mti wa uzima" na "tunda la katikati" ambalo ni tunda la mema na mabaya. utakuwa umeisha lifahamu!. Maneno hayo ni tamathali za semi tuu!.
Baada ya Mungu kutimiza hayo, sasa kazi ya shetani ilikuwa moja tuu, kuhakiisha mwabadamu anamuasi Mungu.
Mungu aliweka malaika mawili wenye upanga wa moto makali kuwili kuhakikisha shetani hawezi kupenya kule bustanini, lakini shetani kwa kutumia uwezo wake, alijigeuza nyoka, akapenya na kuingia bustanini, (huku Mungu akishuhudia) alipofanikiwa kule bustanini alijigeuza mwanaume tena very "hb!".
Akamfuata Eva, akamuuliza vipi kuhusu hili "tunda" ambalo linaliwa na huu "mti" Eva akamwambia tumekatazwa na Mungu!, kwanini?, tuliambiwa tukila tutakufa!. Shetani akamdanganya Eva na kumwambia huo ni uongo!. Kati ya matunda yote hili ndio "tunda tamu" kuliko yote!, na mkilila tunda hili, mtakuwa na uwezo wa Kumungu kujiumbia viumbe wadogo "procreation" kama Mungu alivyowaumba!.
Eva hana hili wala lile, shetani akamwambia hebu "njoo nikuonjeshe!" shetani "akamega" lile tunda na Eva!, Eva "akaonja!" akakuta kumbe kweli "tunda lile ni tamu kweli!", baada ya kuonjesha na shetani, Eva akamfuata Adamu na kumlazimisha "kumega!" huku na kule, Adamu "kamega!" na kama kawaida hufuatiwa na usingizi mzito!, wakaishia usingizini!.
Wakati yote hayo yakiendelea Mungu na jeshi lake lote la malaika wa mbinguni wanashuhudia!. Walipopata mapumziko ya kutosha Mungu akamuita Adamu, ndipo waliposhtuka kuwa wako uchi!, kabla ya pale walijiona ni kawaida tuu hadi "tunda la mti wa katikati!", lilipomegwa!".
Mungu kwa hasiri kutokana na uasi huo wa binadamu, akawafukuza ndani ya bustani ya Adeni, akawwaadhibu kula kwa jasho lao, na Eva atapata adhabu ya ziada ya kubeba kiumbe miezi 9!, na kuzaa kwa uchungu kuufidia ule "utamu wa ile dhambi!", hivyo kile kitendo cha "kumegwa kwa lile "tunda" ndio "dhambi ya asili!", sisi binadamu wote tunazaliwa baada ya ile "dhambi" ya asili kutendeka!, hivyo mtoto akiisha zaliwa hutakiwa kubatizwa ili kumuondolea hiyo "dhambi ya asili" na kwa sisi Wakatoliki, masister na Makasisi wetu, hujitolea "sakramenti" ya "upadirisho" na kiapo na "utawa" kwa kutofanya hiyo "dhambi" ya asili!. Binadamu pekee aliyekingiwa "dhambi ya asili" ni Bikira Maria, alikingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu" "bila tunda lake kumegwa!". Na kwa kitendo cha shetani kumdanya mama yetu Eva, Mungu aliweka uadui kati ya shetani na "mzaliwa wa mwanamke!".
Hadithi ndefu yote hiyo ni kukupa uthibitisho kuwa ni kweli Mungu ana nguvu, ila hawezi kumuangamiza shetani, na ni kwa jinsi hii hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtuma Mwanaye wa Pekee, kuja kuukomboa ulimwengu, na Mwanaye huyo alipitia mateso ya shetani kwa kusulubiwa hadi kufa msalabani, na siku ya tatu akafufuka katika wafu, akayashinda mauti, hivyo kuwa na uzima wa milele, akapaa mbinguni, toka huko ataja tena kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho!, ila pia hata shetani, hatateketezwa, bali maisha yote ya shetani, na watu wake, wataishi milele kwenye lile ziwa la moto ya jehanum ya milele, wakiteseka kwa matezo ya kuungua tuu lakini hawafi, huku watu wa Mungu wakipata raha ya milele, mbinguni, peponi kwa Mungu!.
Pasco