Mkuu Masaki, msingi mkuu wa imani nyingi ni mafundisho ya dini ambayo yako limited kwa kile tuu wanachotaka wanafunzi wake wakijue!. Dini kubwa huku kwetu ni Ukristo na Uislamu na zote mbili hazina mafundisho yoyote kuhusu Mwanzo wa Mungu!, inaelezwa tuu kuwa Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho!, Alfa na Omega!.
Sambamba na kutosema Mungu alianzanzaje, pia mafundisho ya dini hizi mbili kuu, hazisemi, mahali haswa Mungu alipo, zaidi ya kutaja, mbinguni, peponi, mawinguni, ahera etc, hivyo Mungu ni Omnipresent, yupo kote!.
Kama ambavyo dini hizi haziendi too deep kuhusu orgin ya Mungu, pia hazisemi orgin ya shetani zaidi ya kusema jina lake ni lusiferi, na ndiye alikuwa malaika mkuu.
Wengi wa waumini watiifu wa dini, wao wanaamini kile tuu kilichoandikwa katika vitabu vitakatifu vya dini zao, hawaamini kitu kingine chochote ambacho hakijaandikwa!, hawa ni waumini wa imani ya vitabu not logic!. Ukifanya deep meditation hata kwa kutumia vitabu hivyo hivyo vya dini, ukisoma unaweza kufunuliwa ukweli wa ziada ambao sio wengi wanaoujua!. Huu ukweli wa ziada kuhusu Mungu na shetani, ni ukweli mgumu na mchungu kumeza kwa hawa wenzangu na mimi wenye imani za vitabu!.
Dunia ni earth, hapa tulivyo na vyote vilivyotuzunguka, Mungu na shetani, wako over and above hapa duniani tulipo, na ndio maana kuna extra terestrials, viumbe wa sayari nyingine.
Mungu aliumba dunia na kila kilichopo, ila vile ambavyo viko over and above the universe hii tuliopo,sio lazima viwe viliumbwa na Mungu, na moja ya viumbe hivyo ambayo havikuumbwa na Mungu ni pamoja na shetani, ibilisi, majini, mapepo etc!.
Mungu ni omniscience, omnipotent na omnipresence so does shetani!. Mungu ana nguvu, na shetani ana nguvu, ila Mungu ana nguvu zaidi ya shetani!. Mwanzo wa Mungu ndio mwanzo huo huo wa shetani!, source ya powers za Mungu ndio hiyo hiyo source ya powers za shetani!, ila Mungu ndio mwenye powers zaidi na shetani ndie the 2nd in command kwenye ulimwengu wa powers!. Mungu ndie Bwana wa Majeshi ya Malaika wa Mbinguni, na shetani ndiye bwana wa majeshi ya nguvu za giza!.
Shetani baada ya kumuasi Mungu, alitimuliwa tuu kutokuwa malaika mkuu, alivuliwa madaraka tuu, hakuvuliwa powers!.
Ukiondoa uwezo wa uumbaji ambao ni Mungu tuu mwenyewe mwenye uwezo huo, na uwezo wa ku end life ni Mungu tuu ndie mwenye uwezo huo, vituvingine vyote ambavyo Mungu anavifanya, shetani pia ana uwezo wa kuvifanya!.
Kuna wahubiri wengi, wana uwezo wa kufanya miujiza mikubwa ya ajabu, ukiwepo kufanya uponyaji, huku wakilitumia jina la Mungu, lakini kiukweli ni watumishi wa shetani na wanamtumikia shetani kwa kujijua au bila kujijua!.
Mungu alipotuumba, na kutupulizia ile pumzi ya uzima, ndani ya pumzi hiyo, umeweka nguvu zake za Uungu, hivyo Mungu yuko ndani ya kila binadamu aliye hai regardless unamwamini, au haumwamini, na shetani nae ni omnipresent, anaweza kuingia kwa yotote na kumpa majaribu, regardless anamwamini Mungu, ana mtumikia Mungu na yuko na Mungu ndani ya yake ndio maana alidiriki hata kumjaribu "Mungu Mwana!", akamchukua na kupaa nae hadi juu ya mlima mrefu kwenda kumpa majaribu!.
Ndani ya miili yetu, tumepewa uwezo wa Ki Mungu kufanya kila kitu, ila pia, shetani nae ana uwezo wa kuingia ndani ya miili yetu na kutuwezesha kufanya aina ya uovu kwa kutumia nguvu za giza. Mema yote hufanyika kwa nguvu za Mungu na maovu yote hufanyika kwa nguvu za shetani na wanaofanya yote haya ni binadamu kupitia nguvu iliyopo ndani yao, iwe ni ya Mungu ambayo imewekwa automatically siku ya uumbwaji na nguvu za shetani ambazo ni induced!.
NB. Members wa darasa hili, tusameheaneni tuu wajemeni, siku za hivi karibuni nimejikuta bize hadi kukosa muda kuliendeleza darasa!.
Pasco