Huwezi kutumia (Psychic Powers): Ni Nguvu za Kufanya Miujiza Pasipo na wewe kuwa na Pepo anaye kupa Nguvu mwilini mwako. bila ya hivyo hutoweza kufika popote pale Ukimuona Binadamu anafanya Miujiza ujuwe anashirikiana na Mapepo mwilini mwake ndio yanayo mpa Nguvu za Giza ili uweze kufanya Miujiza pasipo na hivyo hutoweza kufanya miujiza yoyote ile.
Mkuu Mzizi Mkavu, nguvu "powers from within" kila mtu anazo!, ziliwekwa na Mungu Muumba, (God the Creator) they are on you!, popote ulipo nguvu hizi ziko ndani yako, na huhitaji kufanya jambo lolote au kutumia kitu chochote ili kuziamsha zitumike bali ni kuwa na imani tuu!. Nguvu hizi ndizo huitwa Nguvu za Mungu, Nguvu za Yesu, Nguvu za Roho Mtakatifu, Nguvu za Mwanga, Nguvu za Kweli, Nguvu za Uzima, Nguvu za Uponyaji, Nguvu za Heri etc etc.
Sambamba na nguvu hizi za Mungu zilizomo ndani yetu, mwovu shetani naye yupo na ana nguvu zake. Nguvu za shetani ziko inje yetu, hizi ndizo nguvu za giza, nguvu za majini, nguvu za mapepo, nguvu za uchawi, ulozi, unajimu, kupandisha maruhani, kupandisha mapepo, wanga, ushirikina na kila aina ya uovu. Kwa vile nguvu hizi ziko nje yetu, ili kuweza kuzitumia ni lazima uziite, kuita majini, mashetani, mapepo kwa kutumia kitu chochote , iwe ni mipete, mishumaa, au conditions zozote, au masharti yoyote.
Tofauti pekee kati ya nguvu za Mungu na nguvu shetani, nguvu za Mungu ni unconditional, hukitaji kufanya chochote kuzitumia nguvu hizi, lakini kwa upande wa nguvu za shetani, ni pale unapopewa conditionalities za aina yoyote!, sijui fanya hivi!, fanya vile!, tumia kitu hiki ana kile!, geukia upande huu ama ule!, etc, etc.
Uwezo wa "psychic" ni njia tuu ya kuzifungulia hizo powers na kuzielekeza unataka zifanye nini!. Sehemu kuu ya kwanza ambayo ndipo tatizo kubwa lilipolalia, ni njia tuu ya kuzifungulia hizo powers na determinant kama ni nguvu za Mwanga au za giza, inapimwa kwa matumizi ya nguvu hizo.
Ukizifungulia unconditional, zinazofungunguka ni nguvu za Mungu zilizo ndani yako!. Ukizifungulia kwa conditional yoyote, kupitia hiyo conditional, unakuwa umekaribisha nguvu za giza kutenda unayoyataka, kwa kujijua au bila kujijua!.
Nyingi ya yale mafundisho yako Mkuu Mzizi Mkavu, ni matumizi ya nguvu hizi with conditionalities.
Pasco.