Public Relations Advice: Rais Samia alipaswa kuiambia dunia maneno haya kuhusiana na World Cup 2026

Public Relations Advice: Rais Samia alipaswa kuiambia dunia maneno haya kuhusiana na World Cup 2026

Nina Akili Ndogo Sana

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
865
Reaction score
1,125
NB: Nina Akili Ndogo Sana

Habari za wakati huu,

Ndugu zangu.

Bila shaka wote mpo wazima kabisa wa afya na poleni sana kwa shughuli za ujenzi wa taifa.

Katika kipindi hiki ambacho Tanzania bado inapona makovu ya vurugu pamoja na mauaji ya October/November 2025 na sasa inaendelea kupambana kurejesha uhusiano mwema na global western powers (The International Community), washauri wa Rais walipaswa kumshawishi aandike maneno haya katika accounts zake za mitandao ya kijamii.

KOMBE LA 2026.

"Leo ni ufunguzi wa mashindano ya kombe la dunia la mchezo wa mpira wa miguu kule nchini Mexico, mashindano yanayoleta pamoja mataifa mbalimbali kutoka katika mabara yote kwa lengo la kutaka kutukumbusha ya kuwa, licha ya tofauti zetu za kiuchumi, rangi, dini na hata lugha, sisi sote bado ni wamoja.

Ingawa nchi yangu ya Tanzania si moja kati ya Mataifa yatakayoshiriki mashindano haya kwa mwaka huu, ila kutokana na uwekezaji mkubwa wa kifedha na kiujuzi tunaoufanya katika sekta ya michezo, hususan mchezo huu wa kandanda, bado tuna imani kubwa ya kuwa ipo siku nasi tutakuwa miongoni mwao, hivyo ninaomba kuyatakia kila la kheri Mataifa yote yaliofanikiwa fukuzu na Mwenyezi Mungu akayasimamie vema wao pamoja wenyeji waandaaji wa michuano hii."

WORLD CUP 2026.

"As the World Cup kicks off today in Mexico, we are reminded that football brings nations together, transcending our economic, cultural, and linguistic differences.

While Tanzania is not competing this year, our ongoing financial and technical investments in sports give us confidence that we will soon grace this global stage. I wish the best of luck to all competing nations and success to the host organizers."

NB: Nina Akili Ndogo Sana.
 
Upo sahihi sana boss wangu. Hakika Nina Akili Ndogo Sana
Angalia watakuita Iskareote shauri yako maana Yuda ndio alikua na akili ndogo sana kati ya wale wanafunzi 12 wa Yesu yeye ndio alikua Muhasibu yeye ndio alikua Muweka Hazina yeye ndio alikua Mtunza Fedha yeye ndio alikua Mkaguzi wa Mapato na Matumizi ila Yuda alikua na akili ndogo sana kiasi cha kuhongwa vipande 30 vya Fedha na kumsaliti Yesu, ni akili ndogo sana
 
Form Six nilipata division 4
1781247597012.gif
 
Back
Top Bottom