PUBLIC RELATIONS: Waziri Kabudi alikosea kuikana kauli yake juu ya kifo cha Azory

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiJorums.

Ninajua fika baada ya kuandika thread hii kuna watu watanitukana sana, wengine watasema ninajipendekeza kwa wakubwa, wengine watasema ninatafuta uteuzi, wengine watasema mbona ninajishushia hadhi.

Ila ninachosema mimi ni kuwa sipo hapa jukwaani kwa minadi ya kufurahisha watu. Bali nipo hapa kuongelea ukweli kama ambavyo unapaswa kusemwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi aliwahi kukanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas alimnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia alisema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi alisema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

USHAURI WANGU WAZIRI KABUDI ANGESEMA MANENO HAYA
=====
Nilichokisema ni kweli kuwa Azory Gwanda alikufa. Azory alikufa ndani ya mawazo, akili na mioyo ya wanaharakati ambao kila uchwao walikuwa wakiisumbua serikali kwa kuihoji juu ya taarifa sahihi za mahali alipo na hatua za upelelezi zilizofikiwa na jeshi letu la Polisi.

Sisi kama serikali tunatambua vema mchango wa makundi haya ya watetezi wa haki za binadamu pamoja na asasi za kiraia katika kutukosoa na kutukumbusha juu ya wajibu wetu kwa jamii ya watanzania iliyotupa dhamana ya kuwaongoza.

Kwa niaba ya waziri wa mambo ya ndani, ninapenda kutoa tena salamu za pole kwa familia ya Azory kwa kupotelewa na mpendwa wao na taarifa kamili juu ya tukio hili zitatolewa pindi upelelezi utakapokuwa umekamilika.

Tunaahidi kuwa tutahakikisha kunaendelea kuwa na mazingira bora, salama na rafiki kwa wanataaluma wote wa tasnia hii ya habari kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.

=====

Ni bora baba yangu mzee Kabudi angesema maneno haya.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
mbona sasa ishu nyepesi sn isiyohitaji maelezo mengi ya kuhofia kutukanwa
 
Ninahofia kutukanwa kwa maana siku hizi JF imevamiwa na vijana wengi wenye tatizo la malezi mabovu huko makwao. Tena hili jukwaa la siasa ndio wamejaa sana.
 
kwann unawaza vijana wenye malezi mabovu ukashindwa kutafakari wazeee wamekuwa wanafiki zaidi,mfano paschal wa juzi ndo paschal wa leo?so tatizo lipo kubwa af kotekote
 
Hao wazee wanafiki mimi siwajui mkuu
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiJorums.

Ninajua fika baada ya kuandika thread hii kuna watu watanitukana sana, wengine watasema ninajipendekeza kwa wakubwa, wengine watasema ninatafuta uteuzi, wengine watasema mbona ninajishushia hadhi.

Ila ninachosema mimi ni kuwa sipo hapa jukwaani kwa minadi ya kufurahisha watu. Bali nipo hapa kuongelea ukweli kama ambavyo unapaswa kusemwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi aliwahi kukanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas alimnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia alisema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi alisema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

USHAURI WANGU WAZIRI KABUDI ANGESEMA MANENO HAYA
=====
Nilichokisema ni kweli kuwa Azory Gwanda alikufa. Azory alikufa ndani ya mawazo, akili na mioyo ya wanaharakati ambao kila uchwao walikuwa wakiisumbua serikali kwa kuihoji juu ya taarifa sahihi za mahali alipo na hatua za upelelezi zilizofikiwa na jeshi letu la Polisi.

Sisi kama serikali tunatambua vema mchango wa makundi haya ya watetezi wa haki za binadamu pamoja na asasi za kiraia katika kutukosoa na kutukumbusha juu ya wajibu wetu kwa jamii ya watanzania iliyotupa dhamana ya kuwaongoza.

Kwa niaba ya waziri wa mambo ya ndani, ninapenda kutoa tena salamu za pole kwa familia ya Azory kwa kupotelewa na mpendwa wao na taarifa kamili juu ya tukio hili zitatolewa pindi upelelezi utakapokuwa umekamilika.

Tunaahidi kuwa tutahakikisha kunaendelea kuwa na mazingira bora, salama na rafiki kwa wanataaluma wote wa tasnia hii ya habari kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.

=====

Ni bora baba yangu mzee Kabudi angesema maneno haya.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Rubbish. Professor Palamagamba is right to speak the truth. Azorygwanda alipotea Kibitilindi lakini hatujui alipoteaje but we can make a good shrewed guess. Who was he? A journalist, not "proper" journalist but a freelance, not much better than a petty informer. He was working for Kenyan newspapers, kazi yake kubwa ilikuwa breaking news. We assume he was being paid well for his scoops as they call them. Who knows, labda majambazi waligutu au walihisi anawatibulia mipango yao breaking news kuzitoa prematurely?

One more thing: breakingnews ilikuwa magazeti ya Kenya tu, si ya Tanzania, hata ya Kubenea nduhu. Pili, zilikuwa breaking news tu kama polisi au kada wa CCM kanyongwa au kachinjwa porini na magaidii su kituo cha polisi kimevamiwa. You must remember that Kibitilindi kilikuwa kitovu cha magaidi, walikimbizwa Mombasa wakaenda Tanga wakaenda Sitakisheri, mhamsishaji wao akiwa ni kikundi cha Uamsho toka Zanzibar.

Walikamatwamatwa wakakimbilia Kibitilindi kwa Azorigwanda, baadaye wamekimbilia Msumbiji. Kama unatafuta ukweli waulize watu watatu: 1. Magazeti ya Kenya; 2. Chadema (walisema Bungeni kuwa CCM wenyewe wamejitakua); 3, wa tatu waulize Uamsho kupitia ACT wazalendo (walipofukuzwa CUF na lilipumba walihamua huko) ndiyo watetezi wao.

Jiulize: Kibitilindi hakuna mtu wa CUF au ACT au Chadema aliyeuliwa na magaidi. You don't have to be a Policeman to see it is an organised racket for political ends.
 
Back
Top Bottom