Public Servant kukataa uteuzi wa Rais, not only embarrassment, but also insubordination of the Highest Order! They deserve summary dismissals

WENGI HAWAJUI HIKI KUWA MTUMISHI ANAPONDA CHEO ANATAKIWA KUANDIKA BARUA YA KUKUBALI AU KUKATAA CHEO AU DARAJA JIPYA
Ni nashangaa watu wanasema ukikataa eti sijui ni kosa,Cheo kinaendana na uwezo wa mtu kukitumikia,sasa kama siwezi nikubali tu kwa kumfurahisha mtu?

Halafu kumbuka huyu aliyekataa anatoka kuwa mwalimu anaenda kwenye nafasi ya kisiasa kabisa,ingekuwa anaenda wizarani kusimamia elimu labda tungesema mengine,mtu unaenda kwenye siasa kabisa ambayo haina uhusiano na ualimu,Kibaya zaidi unakuwa Chawa wa CCM.
 
Tuendelee kuwaza na kuangalia tofauti ili likija kupita hili basi kama jamii liwe limetufaidisha kwa kuingia zama mpya.

Katika kuwaza tofauti, mimi silioni hili kama ni insubordination kwa namna yoyote ile.
Haiwezekani iwe hivyo sababu mtu ana hiari ya kukataa au kuukubali uteuzi kwa sababu aonazo zinafaa.
Kulazimisha kwamba ni lazima Mtumishi wa umma akubali teuzi au chochote atakachoelekezwa, huko ni kuwageuza watumishi wa umma kuwa mateka.

Watu huwa na sababu zao hivyo hupelekea kukataa nafasi hata zile zilizo ndani ya taaluma zao.

Waalimu au watumishi wa umma wasichukuliwe kama askari, hao (askari) ndiyo wakikataa unaweza ukajenga hoja kama ulizozijenga, lakini siyo hawa.

Tena hawa ilipaswa waandikiwe barua ya kuombwa kupokea uteuzi, siyo wanakutana tu na manyotanyota huko mitandaoni
 
Kuna namna nakubaliana nawe,

KATIBA iliyopo imebadili Jina la kiongozi mkuu Kutoka kuwa MFALME na kumwita RAIS, bt kimamlaka ni MFALME.

Zamani kukataa AMRI ya mfalme lazima kivuli kichukuliwe.

KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA itaondoa Ombwe Hilo.

Aamen.
 
Mbona yule wa TIGO IRINGS ALIMKATSLIA MAGU. Maana MAGU slisema km unahisi hutamudu sema maprma ..jamaa alikua bosi wa kanda
 
Thread title iko biased, huu ni uandishi wa kishabiki, kujipendekeza, wakichawa, there is always a reason to say no or yes with freedom. Ungejisemea kuwa mlio tayari kutumikia ukuu wa wilaya mpo mamlaka iwaone. Utii na unyenyekevu hata katika kukataa jambo unaweza kuonekana na wengine huwa katika ugonjwa au majukumu na kuwasiliana na Mamlaka za karibu kmya kmya.
 
Hiki unachoongea kingekuwa na mashiko kama aliyekuteua ni kiongozi wa idara unayofanyia kazi

Lakini hapa ni swala la Rais na ambaye ni mkuu wa nchi.kuukataa uteuzi wake haina tofauti na kwamba amekutuma kwenda kufanya uwakilishi wake mahali na ukakaidi kutumwa.
 
Sio kila mtu anapenda kuwa croock wengine wako happy na maisha yao wewe utaanza vipi kumteua mtu bila kumpa taarifa kabla? nafasi zote za kuteuliwa ni kuuza uhuru wako na kuishi maisha yako kulamba viatu vya walio juu yako Shame
 
Musilazimishe kumfanya mkuu wa nchi ni li dude fulani la kutisha ambalo maamuzi yake hayapaswi kupingwa.

Hoja inarudi palepale, hiari ya mteuliwa kukubali au kukataa ni lazima iheshimiwe, siyo mateka yule.
Kumbuka, uteuzi huo unamtoa kabisa kwenye eneo lake la kitaaluma. Wengine hawawezani na siasa.
Hata wateuliwa wa hizo nafasi wakiangalia majukumu Ya hizo nafasi anaona wanakwenda kuwepo tu ofisini huku maisha yake aki9na ni kama vile yamesimama
 
Mi naona ingekuwa kosa kubwa sana kukataa huo uteuzi endapo wateuliwa wangekuwa ndiyo pekee wanaujuzi na hiyo nafasi,lakini kama nafasi yenyewe haihitaji hata ujuzi na watu wapo wengi sana wenye uwezo na wanahitaji hizo nafasi sasa wao wakikataa kosa lipo wapi hapo!
 
Jamaa ni snitch sana, anawachongea, huyu tungekuwa tunaishi naye kitaa, kitambo angeshakula bisibisi la koromeo
 
Paskali, sikubaliani na wewe asilani. Hata kama ni public servant si busara kumkurupusha kwa kitu ambacho hakutarajia. Hata kama siyo kupewa advance notice ya uteuzi angalau wangepewa muda wa kujiandaa kwenda kuripoti kituo kipya cha kazi hivyo kuweza ku-hand over shughuli zao na kuziacha familia zao salama. Kweli mfumo wetu wa utawala unahitaji kufumuliwa.
 
Masalia ya watumwa nchii hii ni mengi katiba inayomlinda raia ndio inayomlinda Rais, uhuru na haki ni msingi wa maisha.
 
Nashukuru kwa kutujuza
 
Mkuu umeongea vema sana, haya haya matanzania ndiyo yaliofurahia baadhi ya wakuu wa wilaya kutengeliwa, mijitu ya ajabu mbona haijashirkiana kulalamika Rais kutengua wakuu wa wilaya, unasomaje sheria na uwe na mindset ya kifalme na kidikteta. Hii hali ni hatari sana
 
Tatizo la jukwaa hili wachangiaji wengi wamekuwa na mihemko kuliko weledi.......tuchangie mada Kwa kuzingatia weledi na hoja za msingi kama watu wazima waliotoa tongo tongo.......na sio kumshambulia mtoa mada..........
 
Kwa nini kulazimishana kazi? Kwani hao walioteuliwa ndio pekee wenye uwezo wa kazi hiyo?
 
Tena ni waalim, taaluma inayozaa mapooza.

Kumbe hata wale watoto wanaojibu matusi kwenye mitihani yao hawana kosa, ujinga unaanzia kwa waalim wao.

Huo ujasiri wa kukataa amri ya mkuu wa nchi wameutoa wapi?
Koma. Unapata wapi ujasiri wa kumlazimisha mtu kufanya kazi asiyoitaka? Au unataka kulazimisha udikteta tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…