As a Kenyan living in Tz,I have to say thumbs up to Tz_dians coz of two things. Kuna vituo vingi vya daladala kwa mfano, Makumbusho, K/koo Gerezani, Mawasiliano etc ambavyo ni muundo msingi muhimu katika swala zima la uchukuzi. Kenya vituo kama hivyo havipo ila matatu hu_park barabarani pembeni na wakati mwingine/mara nyingi huchangia msongamano katikati ya jiji. Pili,ni ishu ya nauli. Ninachopendea Tz ni kuwa nauli ipo standardized. Ni ile ile Asubuhi, mchana,usiku alfajiri tofauti na kwetu ambapo inapanda na kushuka kutegemea na jua,mvua, asubuhi au jioni..... Hongereni Tz. Ila sasa,nadhani BRT ingekabidhiwa Wakenya sidhani kama kungekuwa na uzembe ambao mara nyingi mimi hushuhudia pale Gerezani. Yaani basi zimefika,wasafiri kibao,madereva wapo wapo tu,hamna basi kuondoka........ Sijui nisemeje. Swala lingine kuna kusimama kwenye daladala hadi kero. Daladala za Bongo sio comfy isipokuwa Coasters za kwenda Bagamoyo,Posta nk. Ma DCM ya kuvunja migongo yamejaa hadi basi. Hapo tumewazidi Tz. Kenya Bajaj sio nyingi,Dar zimejaa sana. Barabara ya BRT nzuri ila sasa management ndio ishu. Matatu za Kenya nzuri, zina makonda ambao ni wazuri kwenye customer care(sio wote) tofauti na wa Tz.Treni zinafanya kazi,usafiri kwenda estates tofauti tofauti upo. Bodaboda zipo za kumwaga, ila sijui hadi kufikia sasa wamepigwa ban kuingia city centre kama huku. Kama @Anneal utahitaji evidence /reference, sina ni mimi mwenyewe..... Nawasilisha.