Shikamoo mkuuHA HA HA HA HAAAAAA!!!! NEXT LEVEL.
At least we now have something in common!
Nilikuwa Pugu in 1975 High School.
It was a very challenging place.Chakula hamna, maji hamna na tarehe sitaishau ni 5/5/1975 wanafunzi wote tuliandamana kwa mguu toka Pugu hadi kwa Mkuu wa Wilaya Mama Kunambi kuprotest hali mbaya ya maisha pale shuleni.
Marehemu Mama Kunambi alituonea huruma sana na akakodi maba si ya UDA kuturudisha shuleni.
Kwa miezi kadhaa baada ya hapo chakula na na maji yalirudi kwa fujo!!
Mwalimu Mkuu aliyejulikana kama Mbise wakati huo alitushukuru kwa undertones kwa kuwezesha tatizo kujulikana na hatua kuchuliwa haraka.
Vile vile hivyo mwaka huo 1975, Mozambique ilipata uhuru wake na tulisherehekea sana na kwa fujo kubwa na kikundi cha ngoma ya sindimba ya kimakonde toka Gongo la Mboto!!!!
Mm nilikuwa EGM lkn namkumbuka sana MkandawilleDuh long time! Mabagala anakufukuza halafu anakupita then anakwambia mtoto mtoto geuza mwenyewe urudi shule. Alikuwa noma sana na kitambi chake cha kiaina!
Wale wa PCM na PCB wa miaka ya 1990 - 2000 mnamkumbuka Mkandawile?
R.I.P walimu nawakumbuka sana hawaSwai, Chalwe, Mama Mtera & Mumewe, Mnzava, Rwezaura, Msungu hao wote wameshafariki
Kiongozi tulikuwa pamoja mwaka huo hivi unakumbuka unyama aliotufanyia Angelo kwenye practical ya chemistry? Siwezi msahau. Buberwa alikuwa mtu wangu wa karibu sanaDah!! Umenikumbusha mbali sana. Mi nlipita pugu 1998-2000(A-LEVEL).
Naikumbuka sana mihogo ya sh 20, ilitusevu ingawa tulikuwa tunasinzia darasani.
Nakumbuka pia jinsi nlivyokuwa nkila ugali wa jana asubuhi kwa maharage ya jana kama kitafunwa cha chai iwapo sh 20 ya kunnua mihogo ilikosekana. Wenyewe tulikuwa tukiuita mchanganyiko wa ugali na maharage ya jana kwa jina la PROCESS. Sidhani kama kizazi hiki cha ubongo wa fleva kitayaweza maisha yale. Watoto wa mama walikuwa kila weekend wanadrop kwenda town kuchenji dayati, mwalimu mkandawile aliwatunga jina la DAYATI (DIET) BOYS.
Nakumbuka pia jinsi nyama ilivyokuwa adimu, ilipikwa tarehe 15 na 30 kila mwezi. Siku ya kupewa machungwa palikuwa hapatoshi, fujo mtindo mmoja. Mi nlikuwa napozi bweni la ujamaa.
Katika siku nnazozikumbuka ni hii: siku moja ulipikwa ugali kwa unga uliooza mchana. Kumbe unga ule tulikuwa tukiula usiku ndo maana hatukujua kuwa umeoza, sa that day walikosea wakapika mchana, palikuwa hapatoshi, ikabidi tule wali mchana kitu ambacho ni nadra sana kula wali mchana.
Nakumbuka tulipokuwa form 5, dent mwenzetu alianguka uwanjani na kufa papo hapo wakti wakicheza mpira.
Nakumbuka siku ya kufanya mtihani wa mwisho ilikuwa ni siku ya kumaliza physics paper 2, ndio siku alokufa mwalimu msungu, mtaalam wa network ya mabomba pugu. Masikini wanafunzi wengi hawakumzika msungu kwani walikuwa wameshaondoka, msungu alifariki mida ya saa 9 mchana.
Mwalimu wasiwasi nlisikia alikuwa ud kuongeza elimu, baadae nkawa namuona luningani katika maigizo na matangazo ya biashara.
Namkumbuka ticha wa bios, mama mbulanya na ticha wa physics practical, ticha nzoi.
Aiseee!!!! Nmekumbuka mbali. Wale ma-pcb boys mnawakumbuka mkandawile, kambwili na mzezele??????? Hao ni walimu binafsi, walitupiga tafu kusaka principles
Duh!!! jamaa alikuwa muongeaji kinoma, akachukua uhead boy.
Washikaji wengine walikuwa wakijiandikia barua wenyewe na kujitumia ili waonekane nao waakumbukwa.
Je, wee ndo yule seleman mfupi?????, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari???? Tulikuwa class 1, 5G/6G kama sikosei. Kama ndo wee unakumbuka ulivyokuwa ukilia baada ya kutoka katika physics paper 2???. Unamkumbuka some body buberwa????, saa hizi ni mganga mkuu msaidizi tmk hospital, dsm.
Not Mungu Mwl Msungu bingwa wa kiswahili na Geography RIP.Nilikuwa O level 1982-85,Maji yalijuwa shida,Gongs Maji ya kunywa,Pond kuoga,siku nzima zamu ya kusomba Maji no vipindi,Second master Swai,Mabagala ndiyo young tu ,Head Mosha,Mkwizu,Wajimila,Mungu,Mukulu duuh long time ,Class mate wa mwakahuo Mni PM, mfano Robert Luseba,Julius Mkodo, nikiishi Maendeleo 1.
Naona uzi umepoa sana huu. Wadau mpo wapi?Not Mungu Mwl Msungu bingwa wa kiswahili na Geography RIP.
Tupo. PUGU BOYS, JULY 1998 - MAY 2000. Kuna kipindi ni niliumwa fungus mpaka nilichanganyikiwa.Naona uzi umepoa sana huu. Wadau mpo wapi?
mwenge na jembe vimeanzia mbali.......View attachment 515698View attachment 515699
Napakumbuka sana mahala hapa. Japo palikuwa na changamoto za maji, walimu na purukushani za hapa na pale kama migomo na maandamano hadi Wizara ya elimu enzi za Mungai (PCB class 2001-2003) lakini all in all kwa kusoma pako poa sana
Nampanda.
HAHAHAHHAAA Mwl Nampanda anakutandika bakora na kukwambia kamwambie mamako mimi ndio NampandaAchana na mabagara asee, Nzoi, Angelo, Rwezaula,Nampanda..., pugu ilikuwa raha saana asee
Mzee wa Ku drop!!Madogo mwaka huu wametetea chama langu la msuli mrefu(PCB) vizuri sana, kutoa DIV I-10 za PCB sio kazi rahisi asee.
Big up kwa madogo, karibuni sana kwenye Afya.
Hahhaaa.Mzee wa Ku drop!!