Pugu Boys Secondary School a.k.a Pond boys

Mambo ya Mzee wa Shamba na mapande ya mihogo kwa uji yalikuwa ni maisha ambayo hayawezi kusahaulika. Nakumbuka mpambano uliokuwa unatokea siku ya kishoka pamoja na uhaba wa maji duh!!!.

Maisha Pugu kwa ujumla yalikuwa ni zaidi ya jeshini.
 
Nitakuwa sijaitendea haki hii thread kama sitachangia,

Mimi pia nilipita hapa na ni mmoja wa wana-POND, Pugu ilikuwa hata aliyepata Zero amejifunza maisha.

Kulikuwa na walimu kama Swai, Charo, Msungu etc.

Kuna mwalimu mmoja kwa jina la Mabagala, duuu huyo teacher noma kishenzi, mambo ya bed check, kuamsha watu asubuhi asubuhi na mboko kama kawa. Daa noma kishenzi.
 

Ha!ha!ha!ha!haaaaaa! Kumbe MC nawe ni walewale wa DOCEBIT VOS OMNIA heeee!

Mkuu Mwal. Msungu alishatangulia mbele za haki.......! Kamanda Mabagala aka Mabags aliendaga UDSM......sijui yupo wapi now! Ila huyu jamaa alikuwa noma.....bed check, akikuta mmelala wawili anauliza cheti cha ndoa kipo wapi....h!ha!ha!haaaaa! Aliwatukimbisa hadi Pond ya kule Mapinduzi.......!tukala forest, noma sana yule jamaaa!
 


Pugu boys oyeeee!hahahahaha
fungus boys wale...Na mimi ni mdau mkuu.Nilisoma Pugu form 5&6.Kwa kweli nimejifunza mengi sana na sitajasahau maisha ya Pugu.
 

Mazee huyo mukulu tulikuwa tunamwita Mwabagala aka Mwabaks.Jamaa ni noma.Kuna story nilisikia alimfumania mshkaji pond wakati wa assemble asubuhi.Basi akaanza kumfukuza jamaa kuelekea Kisarawe.Basi mshkaji kila akigeuka nyuma Mwabaks yuko mgongoni.Ni parefu na kabla hata hawajafika nusu ya mwendo jamaa alikuwa amechoka kishenzi na Mwabaks akawa anakaribia kumkamata.Mshkaji akadhani nishatiwa mikononi mwa Mwabaks na cha moto nitakiona.
Basi Mwabaks alipomkaribia na kuona jamaa kachoka hawezi tena kukimbia,akaanza kumwambia 'mtoto mimi nakwenda kisarawe mtoto sina shida na wewe rudi shule mtoto'
Mwaba mibange ilikuwa inampeleka pabaya!
 
Last edited:

Nawakumbuka hao kwenye bold mazee.Nzoi mtaalam wa physics practicals...ukiingia darasa lake umepaka lotion utamskia na lafudhi yake ya kisukuma 'baba unapaka lotion,unataka tukuutaamani'..hahaha
Mwabagala kama kawa mzee wa ndumu.Msungu alikuwa mzee mmoja safi sana,kukiwa na hitilafu kwenye tank la maji basi mara moja ataanza kushughulika(RIP).Mama Mbulanya mtaalam wa Biology sema kwenye vipindi humuoni,mara chache sana nilikula shule yake
Huyo Godfrey Wasiwasi nadhani atakuwa Juma Wasiwasi huyo.
Kuna Ogesa na yule jamaa tolu wa kihaya Songombingo mnawakumbuka?
 


Hahahahaha!
Nakumbuka kipindi kile mchezo wa tausi wa kina mjuba na siti ulikuwa unapendwa kishenzi bongo na tulikuwa tunaangalia kila jumapili usiku pale mbele na dining hall karibu na bweni la ujamaa.
Jamaa alikera kichizi!
 



Oyaa unamkumbuka mama dagaa??Bili za maandazi kwa mama Pendo??
 
Mkandawire ni DADA? Mi namkumbuka yule Mkandawire majasiriamali......mzee wa machemistry......, alikuwa maarufu sana miaka ya 97 hadi 2003 hivi......?


Nani aliwahi kwenda tution za Mkandawile pale Buguruni na watoto wa Jangwani?Jamaa alikuwa anawapigia debe kichizi mapugu boys kwa majangwani boys!!
Kuna mtu anajua huyu mjasiliamali yuko wapi na anafanya nini sasa?Manake alikuwa anaipenda pugu na mapugu boys utafikiri wanae!
Anyway namshukuru sana Mkandawile manake bila yeye nisingefaulu chemistry pugu.
 

MImi nilimuacha mkandawire dada pale miaka ya mwanzo ya tisini, alikuwa anajitahidi aisee!!

I wish tungekuwa na alumni ya Pugu kwenye yahoo groups na vilevile tungefanya bash moja la karne hasa katika kipindi cha kumuenzi nyerere

Hivi yule ticha nyoka yuko wapi?
 
Sikusoma pugu najua ni boys skul, ila nilisoma tution za Mkandawile alipokuwa anafundisha mtendeni primary school na mchikichini, alinipatia elimu nzuri sana kwenye organic chemistry. Ila Siku hizi ana shule yake binafsi ipo mitaa ya Pugu. Inaitwa jina lake Mkandawile high school. Mambo yake siku hizi yapo swafiii.
 
Wale Wachina walihamia Pugu toka china.Nafikiri baba yao alikuwa ofisa kwenye ubarozi wa Tanzania nchini China,nakumbuka walipohamia pale walilala njaa sana kwa kukosa chakula,kwenye kundi la akina peter kulikuwa na kijana mmoja anaitwa Mboka.Nilisikia huyo Peter Shija alikuwa anakaa kigamboni,na mwingine kwenye kampani hiyohiyo alikuwa anakaa Ukonga,namkumbuka Mkandaliwe na Chemisty yake,those time alikuwa bint mdogo nafikiri ndio alikuwa katoka chuo
 
Last edited:
Duh kweli Pugu tulikua na experience za kila namna! Miaka ya karibuni waliintroduce elimu ya watu "wazima" ambayo ilikua ni shule ndani ya shule. Yaani baada ya masomo wao wanaingia mchana. Kasheshe ilikua hao watu "wazima" walikua ni same age na ma-pugu boys alafu ilikua mchanganyiko. Basi ma-pugu boys walikua wanapenda sana kuwasindikiza hao wasichana mpaka mwisho wa lami na kuwanunulia chips!

Namkumbuka sana Mama Pendo na Mama Khalidi, walitusaidia sana na misosi yao. Nakumbuka siku moja dogo mmoja wa O-level alienda pondi akaja na upupu akaweka bweni zima kisa kuna mtu alikua anamdai alafu hataki kumlipa!

Pugu ilikua na sifa sana siku izo hasa kwa A-level kwani walikua wanajua wanachofanya...kwa O-level wengi hawakua siriaz sana na kitabu. Halafu Mabagala was the perfect ticha for such a school sababu hakukua na sheria wala fensi.Mtu ukitaka 'kudrop' town unadrop tu anytime....

Sitasahau my two years of A level at Pugu....the best part is ..kila unapokua town unakutana na Pugu boys wanakukumbusha mlikua darasa moja au uliwatangulia darasa inatia furaha sana!!! Long live Pugu...Docebit Vos Omnia... ("He-The Holy Spirit, will teach you all")

So many memories za Pugu...ngoja niishie hapa....
 

Stan, kweli wewe ulikuwa mtoto wa mama!!!

Mimi nimesoma Pugu A-Level miaka hiyohiyo kwa raha sana na zile adventure za kwenda mwisho wa lami au Gombs kwenye mnanda na watoto wa gombs ilikuwa tamu tupu. nakumbuka tulikuwa tunakutana na wale wanajeshi pale mwisho wa lami, na kutimua mbio maana jamaa walikuwa wana njaa ya kufa mtu.

Shija nadhani yuko Uk, walikuwa wadogo zetu wa O-level by then...

Unakumbuka tulikuwa na timu nzuri sana ya footbal miaka hiyo?
 

Kaka unanikumbusha timu ya kina Juma Ally!
 
Wazee wa Docebit, naskia pugu imeshapata maji, ni kweli??
 
Wazee wa Docebit, naskia pugu imeshapata maji, ni kweli??

Kaka mara ya mwisho kufika Pugu Semi University ni mwaka 1995 that time Head Master alikuwa anakaimu, lakini maji yalikuwa bado!
 
Wazee wa Docebit, naskia pugu imeshapata maji, ni kweli??

Mkuu hizo ni ndoto, nimepita pale last year hakuna kitu hicho, ila wapewa maji ya kisima kipo karibu na bwalo au kiduka cha shule or kibaa cha maticha ile njia ya kwenda masjid........!
 

Mkuu P53 Respect! Hapo kwenye bold nimecheka sana mzee......lile lijamaa lilikuwa noma sana!

Oyaa unamkumbuka mama dagaa??Bili za maandazi kwa mama Pendo??

Ha!ha!ha!haaaaa.....Mama Pendo + Pendo mwenyewe we acha tu....ile miandaazi yake ilikuwa poa kweli si tulikuwa tunampiga bao kweli.....ila kale ka Pendo.....mzee kalikuwa kametulia........! mzee unawakumbuka wale chokoraa...watoto wama ex Pugu boys.....hawana baba now? ...wakuu yeyote aliyegonga demu pale, si tulikuta vitoto vingi sana vya ma ex Pugu boys so please rudini mkacheki kuna damu zenu pale!

Mkuu ulikuwa unasoma kombi gani?Nilikuwa PCB na niligudua 2000.

Mzee nilikuwa next to your class....EGM na mzee Msungu, Shire na yule teacher Mhaya wa Hesabu! Mkuu utakuwa ulikuwa na kina Mwatebele, Matobogolo Masalu etc sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…