Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitakuwa sijaitendea haki hii thread kama sitachangia,
Mimi pia nilipita hapa na ni mmoja wa wana-POND, Pugu ilikuwa hata aliyepata Zero amejifunza maisha.
Kulikuwa na walimu kama Swai, Charo, Msungu etc.
Kuna mwalimu mmoja kwa jina la Mabagala, duuu huyo teacher noma kishenzi, mambo ya bed check, kuamsha watu asubuhi asubuhi na mboko kama kawa. Daa noma kishenzi.
Ninajua kunawadau wengi sana ambao katika maisha yao watakuwa wamepitia pale Pugu Secondary School kama wanafunzi, wafanyakazi, wakazi etc. Wadau hawa sasahivi wametawanyika sehemu mbalimbali ya nchi yetu na duniani kote.
Mimi binafsi ni mojawapo ya watu waliopitia pale kama dent wa high school...(form 5 to 6), ningependa tujikumbushe mambo mbalimbali kuhusu shule ile ambayo ina historia ndefu sana kwa Taifa letu. Ni shule ambayo viongozi wetu mbalimbali walishapitia pale kama wanafunzi au walimu kama vile Mwal. Nyerere, Mkapa (kama sikosei) na wengine wengi tu.
Kwa kuanza kabisa mimi nakumbuka wakati tukisoma pale, maji yalikuwa upatikanaji wake wa shida sana, kulikuwa na wadudu wa malaria na tryphoid sana, kulikuwa na Fungus acha kabisa....yaani tulikuwa tunakamatwa na fungus kiasi cha kushindwa kutembea au kutembea as if one has STDs.....jamaa mtaani mpaka wakawa wanatuita FUNGUS BOYS Mabafu halikuwa haba sana na machafu...so option ilikuwa kwenda kuogea kule mtoni tulikuwa tunakuita POND....hence tukawa tunaitwa POND BOYS.....!
Anything you remember here?
nimefurahi sana kusikia baghdad!!!!! niliacha kiatu pale masela waliomba hela ya ndumu na mimi nikawa hata 100 ya kupanda gari za chanika sina, pia kwa wale waliokuwepo till 2000 wanakumbuka jamaa mmoja alikua anaitwa Mabagala? anakukimbiza hata ukiwa uchi.
Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),Secondmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
Juma Wasiwasi vipi yupo? mara ya mwisho nilisikia alikuwa anasoma Open University or UDSM. Jamaa alikuwa na misemo ya kutukana, aliniboa pale alipochukua TV ya shule akaweka nyumbani kwake.....watu walipiga kelele lakini jamaa wapi harudishi.....kelele zilipofika mbinguni akaona noma akairudisha
Umesahau na wale kina mama wauza maji,mbogamboga na samaki,bweni la mapinduzi.Mbu kibao vijana wanapiga msuli wamevaa soksi na wamejifunika neti noma sana.Mabagala noma ana speed tofauti na umbo lake jamaa anakula ndumu yule,wakati anakukimbiza utasia akisema "Kijana ongeza speed na kuovateki".Pugu boy ukimuona ameingiza mkono katika mfuko wa suruali usifikiri anakupa pesa anajikuna fangasi.Nzoi mzee wa Physics jaribu kumwita teacher class ukitaka kumuliza swali utasikia "nani Teacher hivi ndivyo mnavyowanyea wazazi wenu?" "baba unafikiri hapa mnazi mmoja" akiwa anamana umesoma tution mnazi mmoja then unataka kum challenge.Currently Pugu Kuna geti na kaukuta ka kiushikaji.
Mkandawire ni DADA? Mi namkumbuka yule Mkandawire majasiriamali......mzee wa machemistry......, alikuwa maarufu sana miaka ya 97 hadi 2003 hivi......?
Nani aliwahi kwenda tution za Mkandawile pale Buguruni na watoto wa Jangwani?Jamaa alikuwa anawapigia debe kichizi mapugu boys kwa majangwani boys!!
Kuna mtu anajua huyu mjasiliamali yuko wapi na anafanya nini sasa?Manake alikuwa anaipenda pugu na mapugu boys utafikiri wanae!
Anyway namshukuru sana Mkandawile manake bila yeye nisingefaulu chemistry pugu.
Sikusoma pugu najua ni boys skul, ila nilisoma tution za Mkandawile alipokuwa anafundisha mtendeni primary school na mchikichini, alinipatia elimu nzuri sana kwenye organic chemistry. Ila Siku hizi ana shule yake binafsi ipo mitaa ya Pugu. Inaitwa jina lake Mkandawile high school. Mambo yake siku hizi yapo swafiii.Nani aliwahi kwenda tution za Mkandawile pale Buguruni na watoto wa Jangwani?Jamaa alikuwa anawapigia debe kichizi mapugu boys kwa majangwani boys!!
Kuna mtu anajua huyu mjasiliamali yuko wapi na anafanya nini sasa?Manake alikuwa anaipenda pugu na mapugu boys utafikiri wanae!
Anyway namshukuru sana Mkandawile manake bila yeye nisingefaulu chemistry pugu.
Wale Wachina walihamia Pugu toka china.Nafikiri baba yao alikuwa ofisa kwenye ubarozi wa Tanzania nchini China,nakumbuka walipohamia pale walilala njaa sana kwa kukosa chakula,kwenye kundi la akina peter kulikuwa na kijana mmoja anaitwa Mboka.Nilisikia huyo Peter Shija alikuwa anakaa kigamboni,na mwingine kwenye kampani hiyohiyo alikuwa anakaa Ukonga,namkumbuka Mkandaliwe na Chemisty yake,those time alikuwa bint mdogo nafikiri ndio alikuwa katoka chuoMimi nilihamia pale mwaka 1993 nikiwa form 4, nilisoma mwaka mmoja lakini ilikuwa kama miaka 10. Nakumbuka siku ya kwanza nilipofika pale baada ya chakula niliona kila mmoja anatoa dumu la maji ya kunywa kutoka katika locker lake, kwa siku hii nilipewa maji na rafiki yangu tuliyesoma nae primary school. Then after ilibidi kila jioni baada ya chakula kwenda kunywa maji mwisho wa lami (imagine that distance), jumamosi yake nami nilitoka nyumbani Dar na dumu langu la maji. Yaani ilikuwa ukipanda basi siku ya jumapili kutoka Dar kila mwanafunzi na galon ya maji ya kunywa. IT WAS TERRIBLE!!!!....!!
Nawakumbuka baadhi tuliokaa nao pale Ujamaa 5 or 3 kama sikosei, bweni lililokuwa linakaa wajanja ambao walikuwa na special attention, nawakumbuka jamaa wawili walikuwa wanaitwa WACHINA nimesahau majina yao. Nawakumbuka Peter Shija, Michael Nandonde, David Mahalu.......,
Kama hapa jamvin yupo aliyemaliza f4 mwaka 1993 naomba tukumbushane majina.
Mimi nilihamia pale mwaka 1993 nikiwa form 4, nilisoma mwaka mmoja lakini ilikuwa kama miaka 10. Nakumbuka siku ya kwanza nilipofika pale baada ya chakula niliona kila mmoja anatoa dumu la maji ya kunywa kutoka katika locker lake, kwa siku hii nilipewa maji na rafiki yangu tuliyesoma nae primary school. Then after ilibidi kila jioni baada ya chakula kwenda kunywa maji mwisho wa lami (imagine that distance), jumamosi yake nami nilitoka nyumbani Dar na dumu langu la maji. Yaani ilikuwa ukipanda basi siku ya jumapili kutoka Dar kila mwanafunzi na galon ya maji ya kunywa. IT WAS TERRIBLE!!!!....!!
Nawakumbuka baadhi tuliokaa nao pale Ujamaa 5 or 3 kama sikosei, bweni lililokuwa linakaa wajanja ambao walikuwa na special attention, nawakumbuka jamaa wawili walikuwa wanaitwa WACHINA nimesahau majina yao. Nawakumbuka Peter Shija, Michael Nandonde, David Mahalu.......,
Kama hapa jamvin yupo aliyemaliza f4 mwaka 1993 naomba tukumbushane majina.
Stan, kweli wewe ulikuwa mtoto wa mama!!!
Mimi nimesoma Pugu A-Level miaka hiyohiyo kwa raha sana na zile adventure za kwenda mwisho wa lami au Gombs kwenye mnanda na watoto wa gombs ilikuwa tamu tupu. nakumbuka tulikuwa tunakutana na wale wanajeshi pale mwisho wa lami, na kutimua mbio maana jamaa walikuwa wana njaa ya kufa mtu.
Shija nadhani yuko Uk, walikuwa wadogo zetu wa O-level by then...
Unakumbuka tulikuwa na timu nzuri sana ya footbal miaka hiyo?
Kaka unanikumbusha timu ya kina Juma Ally!
Wazee wa Docebit, naskia pugu imeshapata maji, ni kweli??
Wazee wa Docebit, naskia pugu imeshapata maji, ni kweli??
Mazee huyo mukulu tulikuwa tunamwita Mwabagala aka Mwabaks.Jamaa ni noma.Kuna story nilisikia alimfumania mshkaji pond wakati wa assemble asubuhi.Basi akaanza kumfukuza jamaa kuelekea Kisarawe.Basi mshkaji kila akigeuka nyuma Mwabaks yuko mgongoni.Ni parefu na kabla hata hawajafika nusu ya mwendo jamaa alikuwa amechoka kishenzi na Mwabaks akawa anakaribia kumkamata.Mshkaji akadhani nishatiwa mikononi mwa Mwabaks na cha moto nitakiona.
Basi Mwabaks alipomkaribia na kuona jamaa kachoka hawezi tena kukimbia,akaanza kumwambia 'mtoto mimi nakwenda kisarawe mtoto sina shida na wewe rudi shule mtoto'
Mwaba mibange ilikuwa inampeleka pabaya!
Oyaa unamkumbuka mama dagaa??Bili za maandazi kwa mama Pendo??
Mkuu ulikuwa unasoma kombi gani?Nilikuwa PCB na niligudua 2000.