Pugu Boys Secondary School a.k.a Pond boys

Mwl Juma Wasiwasi yupo. Mara ya mwisho nilikutana naye UDSM sijui alikuwa anasomea nini. Mwl KOBRA na Mwl CHARWE mmewasahau???? Kwa waliosoma miaka ya 90 MZEE WA SHAMBA aliekuwa anatuuzia mihogo mida ya saa 4 mnamkumbuka? Nikikumbuka DOCEBIT VOS OMNIA hadi nasisimka nywele. Ingawa yalikuwa maisha ya taabu lakini very interesting. Nalikumbuka sana bweni langu la MAENDELEO 2.
 

Du! very interesting, sredi hii imenikumbusha mambo mengi.
 
dah wakuu mmenikumbusha mbali sana..mi nilipiga pale olevo yani nikikumbuka kule BETO nachoka na wale fungus then mama p muuza chai na mihogo mnahabari alitutoka?ni hayo tu wakuu.
 
Pugu Boys, mnanikumbusha mbali sana. Mimi nilipiga O'level pale na Mwalimu Msungu alivyofariki nilikuwepo pale (RIP). Juma WasiWasi himself na Songombingo. Mabags, halafu kuna second master alikuwa hana noma sana yule mzee, Mr Mzava (RIP). Pugu kienyewe was interesting place aisee, ile mihogo ya sh. 20, au kusubiria ukoko wa wali kwa mama Pendo kule chini. Mitikasi ya kuchota maji ya kupikia pondi ilikuwa noma sana. Kuna wakati nakumbuka umeme ulikatika kama wiki mbili hivi, halafu wakafariki wanafunzi wawili mfululizo kighafla ghafla. Pugu palikuwa hapatoshi kipindi kile, story za kila aina.

Ebwana poa sana, sijui siku hizi pakoje--ila Pugu boys watu walikuwa wanapiga sana shule pale. Vijana wa PCB na mikate (kitabu cha biology) walikuwa wanatoboa kila siku. Ili mradi kieleweke. Docebit Vos Omnia. Nakumbuka Taasis ya elimu ya watu wazima ilianzishwa pale, vijana wa Pugu walikuwa wanapiga sana kambi mwisho wa lami kusalandia ngozi za taasisi. Good Memories..
 
selemani... i knew you were something special... kumbe wewe ni wa docebit, na mzee wa shamba

Ile mihogo si haba... tulikula sana ile mikate ya maabara tulikesha mkuu
 
Leoninefurahi sana kukutana na maveterani wa PEOPLE USUALLY GO TO UNIVERSITY

( PUGU)

WAKUU MIMI SI WAZAMANI KIASI HICHO ILA NINAKUMBUKA SIKU NILIFIKA NIKAKUTA JINA LANGU KWENYE NOTICE BOARDN NIMEPANGIWA MAENDELEO ONE. NIKADHANI KUTAKUWA NA KITANDA CHANGU BAATI MBAYA KUMBE YALEMAJINA YALIKUWA YAMEANDIKWA KISIASA. HAPAKUWA NA KITANDA WALA HATA SEHEMU YA KUWAKA MZIGO WANGU. NILIKUWA NATOKA MWANZA. KILICHO NISHANGAZA ZAIDI MIMI NILIKUWA NI MIONGONI MWA WANAFUNZI WALIOFIKA MAPEMA KUANZA FORM FIVE. SASA NIKAJIULIZA HAO WENGINE ZAIDI YA MIAMOJA WATAKUJA WALALE WAPI??????????????
HAPO NDIPO NILIPOJIFUNZA UBUNIFU WA KUTENGENEZA KITANDA HUKU CHAGA ZIKIWA NI MITI NILIYOIKATA PONDI.

NILITAMANI KURUDI MWANZA SEMA TU PALIKUWA NI MBALI.

MWISO SIKU NAONDOKA FORM SIX NILITOKA NIKIWA NIMEIVA KIMAISHA
 
ha ha ha haaaa! umenikumbusha mbali sana kijana.kuna washikaji mpaka leo hawavai chupi kutokana na fungus sugu walizopata pale pond.
afadhali umeanzisha topic hii kwani inatusahaulisha machungu ya uchaguzi.
 
selemani... i knew you were something special... kumbe wewe ni wa docebit, na mzee wa shamba

Ile mihogo si haba... tulikula sana ile mikate ya maabara tulikesha mkuu

Acid kaka kumbe na wewe Pugu Boy. Poa sana. Ili elimu dume tulipewa pale si haba. Sio mchezo kaka. Tulikuwa Ujamaa 2 pale karibia na mesini.
 

Kaka basi tulikuwepo wote miaka ile. Nakumbuka sana siku ile, tulitembea toka Pugu mpaka Karimjee. Usipime ile distance--kulikuwa na ambulance nyuma kubeba watu wakichoka. halafu Marehemu Dr. Omar Ali Juma akatupokea na speech nzito. Haa haaa, vijana tumezoea maji ya mfuko kwa Mwombeki, tukakuta makochokocho tele karimjee.

Kipindi kile kile Head Boy alikuwa yule jamaa wa EGM maarufu kama Osama. Jamaa alipiga bonge la kampeni, akampiga chini chaguo la walimu Bwana Mutayoba.
 

Mkufya mpiga picha? Jamaa alitengeneza sana hela na biashara yake ya kupiga picha. Nalikumbuka sana hilo darasa lenu kaka, si mlikuwa na Jibaba? yule jamaa kibonge anapenda sana soka? kina mutayoba. Chief umenikumbusha Pendo, shule nzima ilikuwa inamtaka.

Yeah wala wauza Chai na mboga mboga. Unamkumbuka "white"? watu walipita sana pale. Sie tulikuwa tunakunywa chai ya babu bwana, watu walianza kusema chai za kinamama zimewekwa limbwata. Hee heee. Jumamosi kudrop ilikuwa mbinde, jinsi makonda walivyokuwa wanatubania kupanda zile DCM mwisho wa lami. Halafu kama ukikosa inspection ya jmosi, jumatatu Songombingo na WasiWasi wanakuja resi ile mbaya.

Pugu boys mnakumbuka siku za kugawa barua (magoma)? watu walikuwa wanakosa usingizi aisee wasipopata barua. Haa haa.
 


Dah!! Umenikumbusha mbali sana. Mi nlipita pugu 1998-2000(A-LEVEL).
Naikumbuka sana mihogo ya sh 20, ilitusevu ingawa tulikuwa tunasinzia darasani.
Nakumbuka pia jinsi nlivyokuwa nkila ugali wa jana asubuhi kwa maharage ya jana kama kitafunwa cha chai iwapo sh 20 ya kunnua mihogo ilikosekana. Wenyewe tulikuwa tukiuita mchanganyiko wa ugali na maharage ya jana kwa jina la PROCESS. Sidhani kama kizazi hiki cha ubongo wa fleva kitayaweza maisha yale. Watoto wa mama walikuwa kila weekend wanadrop kwenda town kuchenji dayati, mwalimu mkandawile aliwatunga jina la DAYATI (DIET) BOYS.
Nakumbuka pia jinsi nyama ilivyokuwa adimu, ilipikwa tarehe 15 na 30 kila mwezi. Siku ya kupewa machungwa palikuwa hapatoshi, fujo mtindo mmoja. Mi nlikuwa napozi bweni la ujamaa.
Katika siku nnazozikumbuka ni hii: siku moja ulipikwa ugali kwa unga uliooza mchana. Kumbe unga ule tulikuwa tukiula usiku ndo maana hatukujua kuwa umeoza, sa that day walikosea wakapika mchana, palikuwa hapatoshi, ikabidi tule wali mchana kitu ambacho ni nadra sana kula wali mchana.
Nakumbuka tulipokuwa form 5, dent mwenzetu alianguka uwanjani na kufa papo hapo wakti wakicheza mpira.
Nakumbuka siku ya kufanya mtihani wa mwisho ilikuwa ni siku ya kumaliza physics paper 2, ndio siku alokufa mwalimu msungu, mtaalam wa network ya mabomba pugu. Masikini wanafunzi wengi hawakumzika msungu kwani walikuwa wameshaondoka, msungu alifariki mida ya saa 9 mchana.
Mwalimu wasiwasi nlisikia alikuwa ud kuongeza elimu, baadae nkawa namuona luningani katika maigizo na matangazo ya biashara.
Namkumbuka ticha wa bios, mama mbulanya na ticha wa physics practical, ticha nzoi.
Aiseee!!!! Nmekumbuka mbali. Wale ma-pcb boys mnawakumbuka mkandawile, kambwili na mzezele??????? Hao ni walimu binafsi, walitupiga tafu kusaka principles



Duh!!! jamaa alikuwa muongeaji kinoma, akachukua uhead boy.


Washikaji wengine walikuwa wakijiandikia barua wenyewe na kujitumia ili waonekane nao waakumbukwa.
Je, wee ndo yule seleman mfupi?????, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari???? Tulikuwa class 1, 5G/6G kama sikosei. Kama ndo wee unakumbuka ulivyokuwa ukilia baada ya kutoka katika physics paper 2???. Unamkumbuka some body buberwa????, saa hizi ni mganga mkuu msaidizi tmk hospital, dsm.
 
Kulikuwa na kale kanyumba ambako kalitumiwa na Mwalimu Nyerere - sijui bado wamekahifadhi?
 



na wewe ulikuwepo? Vp majambazi yalipokuja kuchukua hela wakashindwa kuvunja makabat ya kijeruman?
Naona siku hizi watu wanalipia benki
 
Jamani kwa wle wliokuwepo kwenye matukio ya kupata mjusi, mara panya kwenye sufuria la maharage wakati karibu nusu wameshagawiwa na wanakula! Pugu ilikuwa noma. Kwenye ****** unaacha shati nje, vinginevyo utatembea harufu siku nzima. Ukienda town ukalala huko unakuja kusimulia jinsi ulivyooga maji ya kunywa! hapo una galon ya lita tano ya maji unaifungia kwenye locker huku hela umeacha nje!

Nilichokifurahi Pugu ni ule ufree wake...unaweza toka zako hata saa nane usiku hakuna hata fence!
 
Selemani,

Yeeeah nimekupata unono....tena wewe jamaa utakuwa ni yule mshikaji ulikuwa PCB na kina Mwatebele, Matobogolo masalu etc etc.....! Osama tulikuwa naye pale kwenye cube ya EGM....ile darasa na f.5 lipo kule chooni....wakati lile la f.6 lipo hapo karibu na admin block!

Osama sahivi ni lecturer ITA na Matayoba alikuwa US sijui kama karudi au laahh!

PUGU ....what a school?????
 
Dah, mi nilikuwa sifahamu kama mwl Mnzava amefariki. Wakati sisi tunasoma pale, yeye ndo alikuwa amerejea kutoka Zimbabwe na ndiye alikuwa anaonesha video. Nawakubuka sana walimu wangu: Mwl Maliki, mamilo, kesi, fisoo, shangwe, elias nk
 
Dah, mi nilikuwa sifahamu kama mwl Mnzava amefariki. Wakati sisi tunasoma pale, yeye ndo alikuwa amerejea kutoka Zimbabwe na ndiye alikuwa anaonesha video. Nawakubuka sana walimu wangu: Mwl Maliki, mamilo, kesi, fisoo, shangwe, elias nk

.....Vipi Mwal. Salum humkumbuki? aka mzee wa vidishi na mnazi?
 
Kaka ukienda toilet unaacha nguo nje maana ukiingia nazo zitanuka mavi,kweli pugu!!!!!maji shida
 
Hahaaa,wadau mmenikumbusha mbali"MIMI NDO NAMPANDA,NAKUPIGA HALAFU UNAENDA KUMWAMBIA MAMA'ko NAMPANDA"mapinduz 5 hallah...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…