Ninajua kunawadau wengi sana ambao katika maisha yao watakuwa wamepitia pale Pugu Secondary School kama wanafunzi, wafanyakazi, wakazi etc. Wadau hawa sasahivi wametawanyika sehemu mbalimbali ya nchi yetu na duniani kote.
Mimi binafsi ni mojawapo ya watu waliopitia pale kama dent wa high school...(form 5 to 6), ningependa tujikumbushe mambo mbalimbali kuhusu shule ile ambayo ina historia ndefu sana kwa Taifa letu. Ni shule ambayo viongozi wetu mbalimbali walishapitia pale kama wanafunzi au walimu kama vile Mwal. Nyerere, Mkapa (kama sikosei) na wengine wengi tu.
Kwa kuanza kabisa mimi nakumbuka wakati tukisoma pale, maji yalikuwa upatikanaji wake wa shida sana, kulikuwa na wadudu wa malaria na tryphoid sana, kulikuwa na Fungus acha kabisa....yaani tulikuwa tunakamatwa na fungus kiasi cha kushindwa kutembea au kutembea as if one has STDs.....jamaa mtaani mpaka wakawa wanatuita FUNGUS BOYS Mabafu halikuwa haba sana na machafu...so option ilikuwa kwenda kuogea kule mtoni tulikuwa tunakuita POND....hence tukawa tunaitwa POND BOYS.....!
Anything you remember here?
Dah!! Umenikumbusha mbali sana. Mi nlipita pugu 1998-2000(A-LEVEL).
Naikumbuka sana mihogo ya sh 20, ilitusevu ingawa tulikuwa tunasinzia darasani.
Nakumbuka pia jinsi nlivyokuwa nkila ugali wa jana asubuhi kwa maharage ya jana kama kitafunwa cha chai iwapo sh 20 ya kunnua mihogo ilikosekana. Wenyewe tulikuwa tukiuita mchanganyiko wa ugali na maharage ya jana kwa jina la
PROCESS. Sidhani kama kizazi hiki cha ubongo wa fleva kitayaweza maisha yale. Watoto wa mama walikuwa kila weekend wanadrop kwenda town kuchenji dayati, mwalimu mkandawile aliwatunga jina la
DAYATI (DIET) BOYS.
Nakumbuka pia jinsi nyama ilivyokuwa adimu, ilipikwa tarehe 15 na 30 kila mwezi. Siku ya kupewa machungwa palikuwa hapatoshi, fujo mtindo mmoja. Mi nlikuwa napozi bweni la ujamaa.
Katika siku nnazozikumbuka ni hii: siku moja ulipikwa ugali kwa unga uliooza mchana. Kumbe unga ule tulikuwa tukiula usiku ndo maana hatukujua kuwa umeoza, sa that day walikosea wakapika mchana, palikuwa hapatoshi, ikabidi tule wali mchana kitu ambacho ni nadra sana kula wali mchana.
Nakumbuka tulipokuwa form 5, dent mwenzetu alianguka uwanjani na kufa papo hapo wakti wakicheza mpira.
Nakumbuka siku ya kufanya mtihani wa mwisho ilikuwa ni siku ya kumaliza physics paper 2, ndio siku alokufa mwalimu msungu, mtaalam wa network ya mabomba pugu. Masikini wanafunzi wengi hawakumzika msungu kwani walikuwa wameshaondoka, msungu alifariki mida ya saa 9 mchana.
Mwalimu wasiwasi nlisikia alikuwa ud kuongeza elimu, baadae nkawa namuona luningani katika maigizo na matangazo ya biashara.
Namkumbuka ticha wa bios, mama mbulanya na ticha wa physics practical, ticha nzoi.
Aiseee!!!! Nmekumbuka mbali. Wale ma-pcb boys mnawakumbuka mkandawile, kambwili na mzezele??????? Hao ni walimu binafsi, walitupiga tafu kusaka principles
Kaka basi tulikuwepo wote miaka ile. Nakumbuka sana siku ile, tulitembea toka Pugu mpaka Karimjee. Usipime ile distance--kulikuwa na ambulance nyuma kubeba watu wakichoka. halafu Marehemu Dr. Omar Ali Juma akatupokea na speech nzito. Haa haaa, vijana tumezoea maji ya mfuko kwa Mwombeki, tukakuta makochokocho tele karimjee.
Kipindi kile kile Head Boy alikuwa yule jamaa wa EGM maarufu kama Osama. Jamaa alipiga bonge la kampeni, akampiga chini chaguo la walimu Bwana Mutayoba.
Duh!!! jamaa alikuwa muongeaji kinoma, akachukua uhead boy.
Mkufya mpiga picha? Jamaa alitengeneza sana hela na biashara yake ya kupiga picha. Nalikumbuka sana hilo darasa lenu kaka, si mlikuwa na Jibaba? yule jamaa kibonge anapenda sana soka? kina mutayoba. Chief umenikumbusha Pendo, shule nzima ilikuwa inamtaka.
Yeah wala wauza Chai na mboga mboga. Unamkumbuka "white"? watu walipita sana pale. Sie tulikuwa tunakunywa chai ya babu bwana, watu walianza kusema chai za kinamama zimewekwa limbwata. Hee heee. Jumamosi kudrop ilikuwa mbinde, jinsi makonda walivyokuwa wanatubania kupanda zile DCM mwisho wa lami. Halafu kama ukikosa inspection ya jmosi, jumatatu Songombingo na WasiWasi wanakuja resi ile mbaya.
Pugu boys mnakumbuka siku za kugawa barua (magoma)? watu walikuwa wanakosa usingizi aisee wasipopata barua. Haa haa.
Washikaji wengine walikuwa wakijiandikia barua wenyewe na kujitumia ili waonekane nao waakumbukwa.
Je, wee ndo yule seleman mfupi?????, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari???? Tulikuwa class 1, 5G/6G kama sikosei. Kama ndo wee unakumbuka ulivyokuwa ukilia baada ya kutoka katika physics paper 2???. Unamkumbuka some body buberwa????, saa hizi ni mganga mkuu msaidizi tmk hospital, dsm.