PUMZI/UHAI: Kitu cha gharama kubwa zaidi kinachothibitisha ukuu wa MUNGU; Tuitumie vizuri hapa duniani

PUMZI/UHAI: Kitu cha gharama kubwa zaidi kinachothibitisha ukuu wa MUNGU; Tuitumie vizuri hapa duniani

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
3,147
Reaction score
2,513
Ndugu zangu watanzania kwa wanaoamini MUNGU na wasioamini

Ni ukweli ulio wazi kuwa, kinachomfanya binadamu awe hai ni PUMZI yake, bila pumzi maana yake hakuna uhai

Mtu kufa maana yake pumzi imefikia ukomo, hata wanasayansi pamoja na ujanja wao wote lakini wameshindwa kabisa kutengeneza pumzi ya kiumbe hai.

Matajiri wengi wanatamani maisha yao yasiwe ya ukomo lakini wanashindwa kununua pumzi.

Viongozi maarufu duniani walitamani wawe na pumzi ya kutosha lakini hawakuweza kumudu kushikilia pumzi yao.

PUMZI ndo humfanya mwanadamu afanye kila jambo hapa duniani.. pumzi ndiyo huamua binadamu kupata nafasi ya kutenda mema au mabaya, MUNGU AMETOA NAFASI HIYO YA BINADAMU KUTUMIA PUMZI KWA KADRI ANAVYOPENDA LICHA YA KWAMBA YEYE NDIYO MMILIKI.

Tunaposema Mungu ndiye tajiri kuliko tajiri yeyote na mmiliki wa vyote, tuwe tunaelewa... Mungu ni mwenye upendo alitoa pumzi bure kwa wanadamu, kama angeamua kwamba kila tunavyopumua tulipie hata shilingi moja kwa sekunde ni wazi kuwa dunia isingekuwa na watu.

ukisoma Biblia Mungu anasema AMETUUMBA, TUMTUMIKIE NA KUMCHA YEYE TU...... Kumcha Mungu ni pamoja na kufuata maagizo yake, kwa kutenda yale yaliyo mema na kuepukana na dhambi.

kuna watu watauliza dhambi ni nini? Dhambi ni kutenda kinyume na maagizo ya Mungu. Ikumbukwe kuwa dhambi ilitangulia kabla ya uwepo wa mwanadamu, Mungu alishampa mwanadamu uwezo wa kujua lipi jema na lipi baya (HIVYO HAKUNA ANAYETENDA DHAMBI BILA KUJUA)

Kwa
kumalizia, tuitumie pumzi yetu vizuri kwa kuwa ipo siku MUNGU atachukua pumzi yako na hutokuwa na nafasi tena ya kurekebisha makosa yako. UKITAKA KUJUA UMUHIMU WA PUMZI TEMBELEA ICU angalau hata mara moja kwa wiki.

msisitizo; MUNGU AMETUAGIZA KUTUMIA PUMZI KUTENDA YALIYO MEMA TU, KINYUME CHAKE NI MAUTI YA KUDUMU YA HAPA DUNIANI NA MILELE

Nawatakia kwaresma njema, MUNGU ATUWEZESHE KUWA NA IMANI YA KUTUMIA PUMZI YETU VIZURI

AMEN.
 
Kwanza kabisa athibitishe Mungu yupo kweli na si hadithi za bure za watu tu, kama hajathibitisha hivyo madai yake ya kwamba Mungu ndiye katupa pumzi hayana msingi unaoweza kuthibitishwa.
Ooh oh, here we go
 
Kwanza kabisa athibitishe Mungu yupo kweli na si hadithi za bure za watu tu, kama hajathibitisha hivyo madai yake ya kwamba Mungu ndiye katupa pumzi hayana msingi unaoweza kuthibitishwa.

Hili zee kubwa ila Bado fala Sanaa.
 
Kwanza kabisa athibitishe Mungu yupo kweli na si hadithi za bure za watu tu, kama hajathibitisha hivyo madai yake ya kwamba Mungu ndiye katupa pumzi hayana msingi unaoweza kuthibitishwa.
KAMA MUNGU HAKUPI PUMZI TENGENEZA YA KWAKO
 
KAMA MUNGU HAKUPI PUMZI TENGENEZA YA KWAKO
Kwanza kabisa, thibitisha huyo Mungu unayemsema yupo.

Mimi hata kama nashindwa kutengeneza pumzi, hilo halithibitishi Mungu yupo.

That is a logical non sequitur.

Unaunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano wowote unaoweza kuthibitika.
 
Back
Top Bottom