Pumzika kwa amani Emsley "Baba T" Smith

Pumzika kwa amani Emsley "Baba T" Smith

Apumzike Kwa Amani. Nakumbuka kila alipopita hapa Posta umachingani kwetu alikuwa lazima atusalimie. Jamaa wengi tulipenda kuongea naye ingawa alitupa sana shida kwa lugha yake hiyo "patois' . Nakumbuka 2016 alipokuwa anatimiza miaka 80, alipita na kutujulisha hilo kila mtu hakuamini kuwa kagonga 80. Actually kamzidi father wangu miaka 10.
Ila makaka wengine walikuwa wanamuona mjivuni yaani sio mtu wa ku_socialize na wengine. Kwani haiingii akilini mtu aliyeishi nchini zaidi ya miaka 30 awe hajui Kiswahili.

Ila miaka kama mitatu iliyopita alikuwa analalamika kuwa uhamiaji hawamtaki hapa nchini hivyo alikuwa amepanga kuhamia Ghana. Sijui iliisha vipi suala hilo. Ni hayo tu.
 
Natoa pole kwa wafiwa, natamani kabla hajafa angemkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake, kwasababu kufa bila Kristo ni hasara ya maisha. Rastafari wanaamini Haile Selasie yule muethiopia waliyemuassasinate ndio kristo wao/masihi wao, they don't believe in the God of Ibrahim Isaac and Jacobo. Mungu atusaidie wanadamu. kama kuna rasta yeyote humu ndani, jipambanue na uchukue hatua.
Umehadithiwa habari za uongo
 
Apumzike Kwa Amani. Nakumbuka kila alipopita hapa Posta umachingani kwetu alikuwa lazima atusalimie. Jamaa wengi tulipenda kuongea naye ingawa alitupa sana shida kwa lugha yake hiyo "patois' . Nakumbuka 2016 alipokuwa anatimiza miaka 80, alipita na kutujulisha hilo kila mtu hakuamini kuwa kagonga 80. Actually kamzidi father wangu miaka 10.
Ila makaka wengi walikuwa wanamuona mjivuni yaani sio mtu wa ku_socialize na wengine. Kwani haiingii akilini mtu aliyeishi nchini zaidi ya miaka 30 awe hajui Kiswahili.

Ila miaka kama mitatu iliyopita alikuwa analalamika kuwa uhamiaji hawamtaki hapa nchini hivyo alikuwa amepanga kuhamia Ghana. Sijui iliisha vipi suala hilo. Ni hayo tu.
Hakua mjivuni alipenda sana watu ila hakua mtu wa kila mtu
 
Natoa pole kwa wafiwa, natamani kabla hajafa angemkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake, kwasababu kufa bila Kristo ni hasara ya maisha. Rastafari wanaamini Haile Selasie yule muethiopia waliyemuassasinate ndio kristo wao/masihi wao, they don't believe in the God of Ibrahim Isaac and Jacobo. Mungu atusaidie wanadamu. kama kuna rasta yeyote humu ndani, jipambanue na uchukue hatua.
Mfia dini wew, wew mwenyew unauhakika gani kama yesu ndiye masihi.. au mzungu ndivyo alivyokwambia ivyo
 
Natoa pole kwa wafiwa, natamani kabla hajafa angemkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake, kwasababu kufa bila Kristo ni hasara ya maisha. Rastafari wanaamini Haile Selasie yule muethiopia waliyemuassasinate ndio kristo wao/masihi wao, they don't believe in the God of Ibrahim Isaac and Jacobo. Mungu atusaidie wanadamu. kama kuna rasta yeyote humu ndani, jipambanue na uchukue hatua.
Ujinga huu

Kila mtu ana Imani yake
 
Wanamuamini Mungu wa Isaka, Yakobo na Ibrahim, ila wana mchukulia Heil Selassie I kama mtume wa Mungu.
Kama waislam wanavyomchukulia Mohamed na wakristo wanvyomchukulia Yesu.
They are one of twelve tribes of Israel.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2007731
Emsley "Baba T" Smith
Picha: Ukurasa wake wa Facebook

Miaka kadhaa iliyopita nilipata fursa ya kuonana na Baba T pale East Africa Radio. Tulishikana mikono. Alikuwa ni pande la mtu, na kiganja changu kilimezwa mkononi mwake. Nilikuwa mtembeaji tu na kijana mdogo niliyependa kusikiliza Reggae na mwenye mahaba na utamaduni wa Rasta na Carribean.

Sikuongea naye sana zaidi ya kumsalimia, "Wah gwaan, Baba?" Alitabasamu na kujibu, "I'm blessed, my yute. I'm blessed. You alright?" Nikajibu "Irie, Baba". Iliishia hapo. Nilifurahi kuona akitabasamu. Nilihisi tu kuwa alijua sina hazina ya msamiati wa Patois, hivyo akaona tuishie hapo.

Pale EA Radio nilikuwa ziarani nikiambatana na marafiki kadhaa. Na ni mimi miongoni mwao niliyemuulizia Baba T kwa mama mmoja ambaye simkumbuki jina lake, ila alijitambulisha kwa cheo kizito.

Baba T hakuwepo wakati namuulizia. Mama yule alinijibu kuwa alikuwa bado hajafika kazini. Ilikuwa majira ya saa 4 asubuhi. Baada ya kumaliza jambo letu pale, wenyeji wetu walitusindikiza nje tukiwa tayari kuondoka. Tukiwa tumesimama nje ya jengo kuagana, ndiyo Baba T alikuwa akifika. Alikuwa amebeba mfuko na bakora mkononi mwake; kichwani alikuwa kavaa kofia ya red-green-and-gold huku miguuni akiwa na kobazi.

Yule mama alivyomuona na kumsalimu akauliza, "Ni nani alitaka kumuona Baba T?" Nikajitokeza. Wenzangu hawakujua Baba T ni nani, ila walifurahia muonekano na haiba yake. Alikuwa mtu mwema kama alivyosikika redioni.

Nilimfahamu Baba T kama mtangazaji na DJ miaka mingi nyuma na nilipenda ukweli kwamba nilikuwa nikisikiliza Reggae kutoka kwa mtu aliyeufahamu vizuri muziki huo, na pengine aliyewajua magwiji wa burudani ya Reggae na harakati za Rasta kwa karibu sana.

Kwa hapa nyumbani, kupitia segment ya East African Selection, nilijifunza kuwa kuna wasanii wengi na wazuri sana wa Reggae hapa Afrika Mashariki — hususan Tanzania — ambao bahati mbaya sana hawapati jukwaa la kufahamika vizuri. Baba T alicheza muziki wao na kufanya mahojiano nao. Nilipata fursa ya kuwajua na kufuatilia kazi zao.

Lovers' Rock chini ya unahodha wa Baba T ilikuwa si kipindi cha muziki wa unao-trend tu kama wafanyavyo wengine wasio na uelewa mpana wa Reggae. LiIlikuwa ni jukwaa la kuwafahamu na kufahamu historia za magwiji wengine usiowasikia sana lakini wenye mchango mkubwa katika Reggae.

Tutaikosa sana ile sauti nzito yenye mamlaka. Tutaikosa ile lafudhi safi ya Kijamaika. Madini na busara zake zitaendelea kubaki nasi siku zote.

Baba T ni nani?

Baba T alizaliwa nchini Jamaica mwaka 1936 (ni miaka ambayo harakati za Rastafari ndiyo zilianza kushika kasi) lakini baadaye alihamia Uingereza alikofanya kazi kwa miaka 20 ambapo pia alikuja kumiliki passport ya nchi hiyo. Baba T aliwahi kusema kuwa, baada ya Vita Kuu ya II ya Dunia, Uingereza ilihitaji nguvukazi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Madola.

Mama yake alimshawishi kwenda Uingereza, wakati huo akiwa na miaka 20. Emsley alimchukua girlifriend wake, ambaye mpaka anaondoka duniani amekuwa mke wake. Kwa mliokuwa mkisikiliza shout-outs za Baba T kwenye Lovers Rock mtakubaliana nami kuwa alikuwa akimtaja mkewe, akisema: "Shout out to my beloved wife, Mama T, in Tegeta" Wakati anaondoka Jamaica tayari walikuwa na mtoto. Walifunga ndoa wakiwa Uingereza.

Huko alifanya kazi nyingi: kwenye sekta ya mawasiliano na umeme, lakini pia kama 'fundi rangi' (painter), fundi bomba (plumber) n.k. Alifanya kila aina ya kazi ili familia yake ipeleke mkono kinywani.

Baadaye alienda maeneo mengine ambapo alifanya kazi mbalimbali ikiwemo kuwa Selekta (Deejay). Alihamia Tanzania mwaka 1988, na kama walivyo Marasta wengine, Baba T alijiona yupo huru kwenye ardhi ya nyumbani -- Afrika.

Emsley Anthony Smith aka Baba T hatimaye ameungana na ancestors wake akiwa na umri wa miaka 85.

May his soul find rest and comfort with Jah.

Rastafari Liveth. One Perfect Love!
Baba T lived his entire life showing Love to all people of any walkover, hakuwahi kubagua, May Baba T Gentle Soul rest in Eternal peace
 
Back
Top Bottom