Pumzika kwa amani Emsley "Baba T" Smith

Rest Easy legend.

The legacy lives on.

I will always cherish what he told me, waay back then.

"Write down your stuff, record, publish".
You're lucky to have heard that from the wise man.

I also hear his favorite advice to people was "Live clean and let your work be seen"

How righteous!
 
Baba T lived his entire life showing Love to all people of any walkover, hakuwahi kubagua, May Baba T Gentle Soul rest in Eternal peace
Yeah. He chose to walk the path of righteousness.

Thanks for this! Big up yourself, TAU 1
 
Kama ni kweli Uhamiaji walitenda hayo, basi tuna shida pahala.

Alikuwepo Rasta mmoja aliyeitwa Prof. Ken Edwards aka Joshua Mkhululi. Waliosoma UDSM miaka ya nyuma sana wanamfahamu. Huyu alikuwa Mjamaika aliyesoma Stanford University, moja ya vyuo bora zaidi vya biashara duniani. Alisaidia uundwaji wa kitivo cha biashara pale UDSM na akawa Dean wa kwanza kabisa. Baadaye alikuja kuwa Principal wa kwanza wa IAA lakini cha kustaajabisha alibaniwa uraia hadi umauti unamkuta. Alizikwa Arusha.

Tuna shida ya kuringia uraia wetu.

Ahsante sana kwa ku-share nasi unachofahamu, JAYJAY. Respect!
 
Hii nchi ina ujinga mwingi hua tunajiona wakipekee sana
 
Unaweza kusikia huyo jamaa alikua anatumika na CIA Ndio maana tukamnyima uraia😄😄,JF watu wanapenda story za uongo na kweli za usalama
 
Hiki kitu kama umeambiwa na watu basi bora ukaushe tu kila mmoja ababe msalaba wake. Ingawa ukipatwa na shida mara nyingi tunamkumbuka Mungu.
 
Honestly naweza kusema hili suala lilimnyong'onesha sana marehemu. Kwani hata alipokuwa akija maskani ukimuuliza suala hilo alikuwa anakuambia jamaa walikuwa wanampiga mpira huko wizarani mara kamuone huyu mara kamuone yule, mara wamvue kofia mara kumpekua pekua dreads zake halafu wanaofanya hivyo ni vijana wadogo tu. Actually alikuwa anaona anadhalilishwa. Naweza kusema alipoteza furaha akawa sio yule aliyekua anapenda maongezi.

Apumzike Kwa Amani. Pole nyingi pia kwa Mama T ambaye alikuwa anapita naye pia mara moja moja.
 
RiP baba T

Je alifahamu kuongea Kiswahili?
Sina hakika. Sikuwahi kumsikia akizungumza sentensi ndefu za Kiswahili. Hata hivyo, kuna jumuiya kubwa tu ya wasioizungumza hii lugha hapa Tanzania. Huenda waliomzunguka walipenda zaidi kuzungumza naye kwa Kiingereza na hivyo mawasiliano na watu wake wa karibu ikawa si shaka. Kama Kiswahili ni kigezo, basi hatuna budi kudhani ilikuwa ndiyo sababu. Lakini je, usahihi wa hiki kigezo una hoja gani za msingi? Kiingereza pia si moja ya lugha rasmi za Taifa?

Adrian Stepp, wewe ulifanya kazi ofisi moja na Baba T kwa muda mrefu. Unaweza kutia neno hapa, kaka? Lengo ni kujua kama alizungumza Kiswahili (angalau kidogo)

Heshima kwako!
 
Lack of exposure inatufanya kuona mihadarati kwa kila mwenye dreadlocks. Kuna mataifa ambapo wenye locks wana nyadhifa za juu serikalini na sekta binafsi. Hutoshangaa kuona Waziri au CEO wa kampuni kubwa akiwa ana "rasta" zilizosheheni.

Suala si muonekano bali uwezo wa ku-deliver, siyo?

Ahsante kwa kutushirikisha taarifa hii, JAYJAY. One Big Love, Iyah!
 
Mungu si wa wakristu au wafuasi wa Yesu tu, mwanadamu yeyote tayari ni mwana wa Mungu, hata Wahindu hawamwamini Yesu na makabila mbali mbali hawamwamini na sisi Waafrika tuna dini zetu za asili, kwenda kwa Mungu ni imani na kila mtu ana imani yake si kila wokovu uendane na kumkiri Yesu.
 
Miaka ile Amos "Amo Blaze" Bondo akimkaribisha Baba T kwenye kipindi baada ya yeye kumaliza session yake "give it up for Baba T.."
 
RiP baba T

Je alifahamu kuongea Kiswahili?
Mara nyingi ukimsalimia kwa Kiswahili atakujibu "salama kaka" kisha fasta anakurudisha katika kilugha chake yaani hata kama ulikuwa unajaribu kumkazia muendelee kuchonga kiswahili lazima akuchomoke. Ni wazi hakuwa comfortable na Kiswahili.
 
Mazishi ni Jumanne bila shaka nitashiriki kama Mungu akijalia uzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…