Pumzika kwa Amani Mwalimu Nisetas Dimoso wahusika lazima wachukuliwe hatua!

Pumzika kwa Amani Mwalimu Nisetas Dimoso wahusika lazima wachukuliwe hatua!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Nimeguswa sana na kifo cha kikatilli cha mwalimu huyu ambaye alipigania "standards" kuhakikisha kuwa eneo la shule ni eneo kama yalivyo maeneo mengine yanayotambulika kama "smart area"

Mwalimu huyu amedhulumiwa uhai wake na wanaojidai kuwa ni wafugaji wenye fedha na wasioguswa au kuheshimu sheria.

Hakika wazalendo tutakukumbuka daima na ninaamini wanaohusika wote kwa kifo chako watakamatwa na kufanywa mfano.

Poleni sana walimu wote kwa kifo hiki kibaya na ninaamini mamlaka zitachukua hatua kali dhidi ya wahuni wote waliofanya tukio hili.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
==
Wananchi walimkimbiza Mwalimu Dimoso katika Kituo cha Afya Mbuyuni Wilayani humo kwa huduma ya kwanza, kabla ya kuhakikisha Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, ambako alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu

Diwani wa Kata ya Galula, Mikozi Mwavilundo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lihusisha watu wanaodaiwa kutoka katika familia ya mtu aliyetambulika kwa jina la Charles Matelemko Mwavilundo amesema licha ya taarifa kutolewa mapema katika Kituo Kidogo cha Polisi Galula na watuhumiwa wanaodaiwa kufahamika, hadi sasa hakuna aliyekuwa amekamatwa, jambo lililozua hofu na maswali miongoni mwa wananchi

Diwani huyo ameongeza kuwa tukio ni la pili kwa mtumishi kushambuliwa katika eneo hilo, kwani mwezi wa tatu mwaka huu, mtendaji wa kitongoji katika kijiji hicho alishambuliwa na wafugaji na kupoteza maisha.
1785390315351.png
 
Back
Top Bottom