Punguza gharama za kutumia mafuta kwenye gari lako. Sasa unaweza kutembea kilomita 180 kwa gharama ya Tsh.15,000 tu

Mtungi kwenye gari ndogo ni kilo 11 na hii kilo 11 itakupeleka umbali mara 2 zaidi ya ule wa lita 11 za Petrol.

Wakijitahidi kupeleka hizi huduma mikoani watasanya wateja wengi sana.

Yaah maana unaeza ukataka kwenda mkoani kabla hata hujafika ukarudi kwenye wese
 
Duuha kwaio mtu ameona IST aweke gesi hela ya mafuta inamshinda duuh?
 
Swali bora kabisa!
Kwa jamaa yangu alieweka kwenye IST yeye full tank ni Tshs.17,000 tukienda kwa hesabu kuigawa hii kwa 1,550 itatupa 10.9 ambayo hii ni Kg’s.

So approximately ni kilo 11 ambazo anasema kwa wastani zinakupigisha 200km before taa ya gas haijawaka then unaweza kupiga extra 40km taa ikiwa still on! Ameshafanya hii trial and it works like charm!

Ili uzipate 200km kwa Petrol itakubidi utumie 13 ltr kwa gari inayokwenda kwa wastani wa 15km/l ambayo itakugharimu kama Tshs.32,000 kulingania na bei ya sasa ya Tsh.2429
 
Gesi kwenye IST inakupa uroda wa 200km with full ac kwa Tsh.17,000 tu! Kwa petrol ungetumia takriban Tsh.45,000 for the same joy ride. Wacha watu waweke gas tu aisee its meaningful than it might sound!
Ila at the same time una sacrifice boot capacity sio? Kwaio ukitaka kubeba vitu unatakiwa ukodi kirikuu? Jambo moja watu wanapaswa wafahamy ukiwa na gari unatakiwa uondoe maswala ya cheap mentality kichwani
 
Ila at the same time una sacrifice boot capacity sio? Kwaio ukitaka kubeba vitu unatakiwa ukodi kirikuu? Jambo moja watu wanapaswa wafahamy ukiwa na gari unatakiwa uondoe maswala ya cheap mentality kichwani
Watu wanaangalia unafuu!

Na kamwe maisha hayafanani!

Hii huduma wajitahidi kuitanua watapata wateja wengi sana.
 
Nawaza sana the future of petroleum industry biashara inaenda kufa hii nimefuatilia Toyota wao wanadai kuwa hadi 2030 nusu ya version za gari zao zitakuwa za umeme while the rest zitakuwa hybrid na chache zitabaki kwenye asili ya mafuta wakaongezea kuwa ifikapo 2040 hakutakuwapo na gari za mafuta Kwa sababu za kimazingira Sasa competition dhid ya mafuta imeanza mapema gas inakuwa substitute ya mafuta wanajamvi anaelewa future ya petroleum industry Kwa miaka ya baadae. Makes wa magari wa ulaya vw, Benz Audi nadhani wao hadi 2030's swala la mafuta litakuwa limejifunga
 
CNG inawaka ndio, lakini gesi hii nyepesi kuliko hewa...

Hivyo, kama ikitokea kuna leakage huwa inapotelea hewani na kupaa juu haraka (darasa la form 1, physics kama wakumbuka kitu chenye density ndogo huwa juu)...
Umenikumbusha "nyoya" au "new year" enzi hizo, Mambo ya, "It's less density than air".
 
Vituo vitatu Dar Dar nzima?
Wataalamu walioidhinishwa watatu?

Wateja wakihitaji service au support watipata kwa wakati kweli , considering idadi yenu ya vituo kwa hapa Dar wilaya zote hizi?
 
Hii ishu tangu nimeanza kuisikia nadhani huu ni mwaka unaenda wa 10 sasa, mimi nilitegemea mpaka sasa muwe mmeshapanua huduma kufika mikoani, wilayani, mpaka vijijini lakini naona bado vituo ni vile vile viwili nchi nzima tangu mwaka 2013. Hivyo vituo viwili ikitokea asilimia 5% tu ya magari yote dar waamue kufunga, mtaweza kuwahudumia? Je mtu akitaka kusafiri nje ya dar atajazia wapi?

Hebu kueni serious bana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…