Punguza mazoea ukishaanza kuzisikia hizi kauli kutoka kwa mwanamke wako

Punguza mazoea ukishaanza kuzisikia hizi kauli kutoka kwa mwanamke wako

Vocal Fremitus

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Posts
1,287
Reaction score
6,648
1. Mimi hua sifuti namba za ma ex wangu, siwezi jua anaweza kua msaada mkubwa kwangu baadae (muongo, bado ana feelings na hao majamaa).

2. Siwezi kuacha kuwasiliana na ex/mzazi mwenzangu, hatujaachana kwa ubaya (ni suala la muda tu ila kiporo kitapashwa).

3. Acha kumkaripia mwanangu, hata kama amekosea. Zaa wako (Hii ni ya singo maza).

4. Tunawasiliana kwa ajili ya mtoto, sitoacha kumuheshimu, yeye ndio mwanaume wa kwanza kunipeleka leba (singo maza tena).

5. Mimi huwa napenda company na wanaume tu. Hata marafiki zangu wengi ni wanaume (ruuun!).

6. Yule mwanaume nilimpendaga sana. Sidhani kama nitakuja kupenda kama vile (maana yake wakianza kuwasiliana hauna chako).

Unaweza kuongezea nyingine. Vijana washtuke wasije kuweka kambi mazima katika hamna!
 
Mimi hua napenda company na wanaume tu. Hata marafiki zangu wengi ni wanaume.

Hii kauli nimeisikia mara nying mno karibu kila mwanamke
Kauli ya kujustify kwamba hata ukimkuta amesimamishwa na msela njiani uamini ni washkaji tu. Kumbe nyuma ya pazia wanakulana fresh tu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wapo singo maza wanaojitambua, hasa wale waliofiwa na waliowazalisha. Hawa ambao mabwana zao bado wanapumua [emoji706]
Kuna single mothers walizaa bila kupanga, ule usichana kurukaruka akanasa. Hata kama aliyezaa nae yupo ila hawana mpango waa mahusiano tena na wamepevuka Sasa wanajua wanachotaka. Hawa ni wengi sana na wanaolewa Kama kawaida.
 
Back
Top Bottom