Katika bajeti ya mwaka jana (2013/2014) serikali ilipunguza kodi ya PAYE kwa 1%, kiwango ambacho hakikukidhi haja, na mwaka huu tena wamerudia ujinga ule ule wa kupunguza kwa 1%!!! Na kibaya zaidi, Rais aliahidi kuongeza mishahara kumbe ilikuwa danganya toto. Wafanyakazi wa umma mnatakiwa kuwa makini na serikali yenu sikivu. Ni lini mtaamka kutoka usingizini na kukataa kutumikishwa na seikali kama punda huku mishahara yenu ikiwa haikidhi? Kada ya wafanyakazi inayonyonyeka zaidi ni WALIMU lakini, kwa bahati mbaya sana, hao hao walimu ndio wanaotumiwa na CCM kuiba kura na hatimaye kuirejesha madarakani. Acheni kulalamika, tafuteni njia mbadala ya kujiongezea vipato.
SULUHISHO
1. Wafanyakai wa umma, hasa sisi walimu, tunatakiwa tusitishe kazi. Cha kufanya ni kuwahi asubuhi kazini, ukifika unasaini kwenye kitabu cha mahudhurio na kuondoka mashuleni. Kama kuna shule za binafsi karibu na maeneo yenu ya kazi, jisajilini kufundisha huko. Kwa wale wa vijijini tafuteni mashamba ya kulima na waliopo mjini fungueni magenge au biashara ya naina yoyote ya kuwaingizia vipato. Muda wa kutumikishwa kama punda huku mafisadi pekee wakifaidi keki ya taifa, umekwisha.
2. Jiandikisheni kupiga kura na jitokezeni siku ya kupiga kura mkiwa na ndugu zenu, lengo likiwa moja tukuiondoa serikali hii dhalimu madarakani. Badala ya kushirikiana na CCM kuiba kura, shirikianeni na wananchi kuiba kura za CCM na kuzihamishia UKAWA ili kuwangoa hawa mchwa madarakani katika uchaguzi wa mwaka ujao (2015). Bila kujitetea kwa namna hii tutaendelea kuumia mpaka Yesu atakaporudi.