Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Hapa issue ni sera za nchi na sio Mgaya

Mgaya anatakiwa awajibike kwani aliwekwa hapo akitegemewa anajua anachotakiwa kufanya...afurukute kubadilisha hiyo sera ya nchi! Hivi ni sera ya nchi au ya chama? Anapashwa kujitoa mhanga kutetea walio chini yake sio kushikana mkono na JK! Ila sasa woga wa MTZ unashangaza kwani wa kumtoa Mgaya ni sisi sisi tunaolalamika. Wa kuiondoa CCM ni sisi sisi tunaopiga kelele ufisadi ufisadi and then what? Tunalala tunaamka CCM ni ileile, ufisadi ni ule ule du elimu ni kitu muhimu sana! Pata elimu pambana na maisha kichanyachanya sio ki-panya road, mbwa mwitu etc.
 
PAYE iko hv ,kwa mshahara wa kuanzia 0 hadi 720000,kodi yake ndo hiyo 12%na kinachozidi baada ya hapo kodi ni 30%
 
ccm hiwezi kuwaondolea watanzania umasikini maana ndio mtaji wao,hivi sasa wanajuta kwa wananchi wa Arusha sasa hivi wanafuta njia ya kuwafanya wawe sawa na wananchi wa chalinze inashindikana
 
barite hapo umeongea point sasa waseme ukweli hiyo 13 inamuhusu nani
 
Last edited by a moderator:
Ni afadhali wangetupa hiyo 1900 kwa kupunguza bei katika bidhaa fulani au waiweke kwenye matibabu!
 
Jaman nyie hacheni maisha kila sku yanapanda Bei sie ndo wanazidi kutufanyia maigizo eti unaniongezea mshahara hata sjui umeniongezea kiasi gani huu ni ushenzi ulio tukuka jaman!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naomba mnukuu usemi wa Mandela. "It is said that no one truly knows a nation until one has been inside its jails. A nation should not be judged by how it treats its highest citizens, but its lowest ones."

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Katika bajeti ya mwaka jana (2013/2014) serikali ilipunguza kodi ya PAYE kwa 1%, kiwango ambacho hakikukidhi haja, na mwaka huu tena wamerudia ujinga ule ule wa kupunguza kwa 1%!!! Na kibaya zaidi, Rais aliahidi kuongeza mishahara kumbe ilikuwa danganya toto. Wafanyakazi wa umma mnatakiwa kuwa makini na serikali yenu ‘sikivu’. Ni lini mtaamka kutoka usingizini na kukataa kutumikishwa na seikali kama punda huku mishahara yenu ikiwa haikidhi? Kada ya wafanyakazi inayonyonyeka zaidi ni WALIMU lakini, kwa bahati mbaya sana, hao hao walimu ndio wanaotumiwa na CCM kuiba kura na hatimaye kuirejesha madarakani. Acheni kulalamika, tafuteni njia mbadala ya kujiongezea vipato.

SULUHISHO
1. Wafanyakai wa umma, hasa sisi walimu, tunatakiwa tusitishe kazi. Cha kufanya ni kuwahi asubuhi kazini, ukifika unasaini kwenye kitabu cha mahudhurio na kuondoka mashuleni. Kama kuna shule za binafsi karibu na maeneo yenu ya kazi, jisajilini kufundisha huko. Kwa wale wa vijijini tafuteni mashamba ya kulima na waliopo mjini fungueni magenge au biashara ya naina yoyote ya kuwaingizia vipato. Muda wa kutumikishwa kama punda huku mafisadi pekee wakifaidi keki ya taifa, umekwisha.

2. Jiandikisheni kupiga kura na jitokezeni siku ya kupiga kura mkiwa na ndugu zenu, lengo likiwa moja tu—kuiondoa serikali hii dhalimu madarakani. Badala ya kushirikiana na CCM kuiba kura, shirikianeni na wananchi kuiba kura za CCM na kuzihamishia UKAWA ili kuwang’oa hawa mchwa madarakani katika uchaguzi wa mwaka ujao (2015). Bila kujitetea kwa namna hii tutaendelea kuumia mpaka Yesu atakaporudi.

1. Unadhan wakiamua kutofanya kaz na kwenda kufanya shughuli zao tu serikali itawaacha tu na kuendelea kuwalipa mishahara?? Soma vzr standing orders ndugu!

2. Unadhan tukiichagua CHADEMA na kuingia madarakani ndo tutalipwa mishahara ya mamilioni ya pesa km tunavyopenda?

POLITICS is who gets what,when and how,.......its an art of possible!
 
hapa tatizo sio mgaya.mtamlaum bule mzee wa watu.yeye hakusanyi kodi nawala hatoi hiyo mishara yenu.
 
Nilidhani hii topic ya PAYE ya mwaka huu ingetenganishwa na ya mwaka jana!
 
P.A.Y.E ya asilimia 14 na watu bado tunalalamika. Mimi naona karibu nchi nyingi duniani kodi kama hiyo iko zaidi ya asilimia 20.

Hapo nchi itaendelea vipi kama hatutaki kulipa kodi?

Ndio tupambane na wezi wa mali za umma lakini kulipa kodi ni muhimu.
 
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa


Ukilipwa directors fees ya TZS 12,000,0000 kwa mwaka na mwingine akalipwa TZS 12,000,000 kwa viwango vya kodi vya jana kodi ya directors' fees itakuwa ndogo kuliko ya anayelipwa kiwango hicho hicho kama mshahara.

Sasa hapa tunakwenda wapi? Maana anayelipwa directors' fees ni mtu "well off" hivyo anatozwa kodi yule mfanyakazi anayelipwa kiasi hichohicho kama mshahara analipishwa kodi kubwa zaidi
 
P.A.Y.E ya asilimia 14 na watu bado tunalalamika. Mimi naona karibu nchi nyingi duniani kodi kama hiyo iko zaidi ya asilimia 20.

Hapo nchi itaendelea vipi kama hatutaki kulipa kodi?

Ndio tupambane na wezi wa mali za umma lakini kulipa kodi ni muhimu.

Mtanzania wewe hujaajiriwa. Hakuna PAYE ya 14%, sehemu tuu ya mshahara ndio unatozwa 14%, kiwango kinachozidi 720,000 kinatozwa 30%
 
Kwa nini misamaha ya kodi ni kwa wawekezaji tu?

Kwa sababu rahisi tu , wao wanabembelezwa kuja kuwekeza hapa nchini, maana wananchi wa hapa wanaweza kuwekeza kwenye biashara ya juice nakadhalika, biashara ambayo haihitaji mtaji mkubwa.
 
Ahsante sirikali ya ccm.kwel.mtatawala milele kwa kuendelea.kutujali wafanyakaz wa sirikali nadhan.mpaka miaka 50 ijayo itakuwa mmepunguza kwa 5% bt hilo.deni la taifa pia mngeweka kwenye mishahara yetu ni % ngp ikatwe ili tupunguze mzigo sirikali:
Kigumu chama cha mapinduz
 
P.A.Y.E ya asilimia 14 na watu bado tunalalamika. Mimi naona karibu nchi nyingi duniani kodi kama hiyo iko zaidi ya asilimia 20.

Hapo nchi itaendelea vipi kama hatutaki kulipa kodi?

Ndio tupambane na wezi wa mali za umma lakini kulipa kodi ni muhimu.

mishahara yao inaeleweka siyo posho za huku kwetu bongo bana
 
Back
Top Bottom