Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu STEIN, hawa jamaa siku zote ni watu wa kufanya mzaha na maisha yetu. Nakumbuka mwaka jana walipunguza shilingi elfu nne na mamia kadhaa tu! Sasa unapunguza elfu mbili halafu unaleta kodi ya laini ya simu ya shilingi 1,000 na mimi uliyenipunguzia hiyo 2,000 nina laini tatu za simu na kwa maana hiyo bado inabidi nitafute 1,000 nyingine ya ziada. Kazi tunayo hapa manake unafuu wa maisha haupo kabisa na badala yake ndo wanayafanya yanazidi kuwa magumu zaidi.
PAYE imepunguzwa kutoka 14% hadi 13%, wataalamu wakasema hilo punguzo halina tija, sasa tunaona kwenye figure ni Bk 2000 tu.
Mbona humalizii hiyo 2,000 kutoka kodi ya shillingi ngapi?
We mama bora uwe unachangia kule kwenye jukwaa la mahusiano na mapenzi, kila kitu ushabiki tu, umeambiwa imepunguzwa Tsh 2000 tu, hivi ambacho hujaelewa hapo ni nini? Mfano kama ulikua unalipa Tsh 100,000 umepunguziwa Tsh 2000, maanake utalipa Tsh 98000/= Ugumu uko wapi hapo? Ndio maana tunasemaga ukiona mtu anapenda ccm assumption kichwani ni either huyo mtu ni mjinga au fisadi au anafaidika na mfumo wa kifisadi.
Binafsi sioni tatizo hapa, kwani kama ilivyoada ya wafanyakazi pamoja na vyama vya wafanyakazi huwa wanajipendekeza kwa serikali. Sasa kama mtu unajipendekeza kwake acha akupe za uso kavu kavu. Binafsi ningependa wafanyakazi wazidi kunyonywa na kupandishia kodi kubwa ili wajitambue na waamke kupigania haki zao.
Eti kila sherehe za mei mosi wanamualika rais akapige politiksi. Hata ningekuwa mimi kama mijitu inajipendekeza yenyewe na mimi na ichinjia baharini tu kwani si ni waoga hawawezi nifanya kitu. Tena hakuna watu majuha na majununi kama wafanyakazi na vyama vyao. Ni heri hata kungekuwa hakuna mambo ya vyama vya wafanyakazi kwani hivi vyama vipo tu kama miamvuli ya kufichia maovu ya serikali.
Chukueni hatua la sivyo mtabaki tu kama vifaranga vya kuku mkisubiri kunyonya hadi mtakapo gundua kumbe mwafanyiwa usanii kweupe mchana. Kuna haja gani ya kujipendekeza kumualika rais wa jamuhuri ya muungano awe mgeni rasmi? Hivi mnafikiri atasema nini zaidi ya kuwadanganya tu na kupiga siasa na fiksi nyingi? Hebu jaribuni ikifika siku ya wafanyakazi basi mkusanyike na kujadili dhuluma mnazofanyiwa. Fanyeni makongamano kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi. Alikeni wanaharakati, wanasiasa, na wadau wengine wengi katika hilo kongamano. Ikosoeni serikali mchana kweupe na pia muipe mapendekezo yenu mnayoona yataboresha maslahi yenu. Na kama hamuwezi basi ni bora mkanyamaza kulalamika kwani tumechoka kuwasikia kila mwaka na malalamiko haya haya.
Mwisho kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwatakia pole kwa maumivu mnayopata kwa kodi zitozwao katika mishahara yenu. Lakini niwaache na usemi usemao kuwa wajinga ndio waliwao.
unaomba maiti msaada??? punguza hizo
kweli kwa wabunge kupitisha kodi ys simcard, wakatwe mishahara na posho ya siku hiyo irejeshwe; mbona halmashauri zikipata hati chafu au DED wakifanya fyongo wanakatwa mishahara, mrema alishadadia hili la DED, sasa ni zamu yako kushadadia wabunge mkatwe mishahara kwa kuborongo kiasi hicho.
kwa niaba ya wafanyakazi nchini napenda kuwasilisha maombi maalum ya kujua matumizi ya kodi ya PAYE kama ilivyokuwa kwa kodi mpya ya simcards.
Ni vyema tukaambiwa ni % ngapi ya PAYE inakwenda kwenye afya,elimu,miundombinu,maji,nishati n.k
ni wakati wa kushinikiza ili tupatiwe ufafanuzi wa kodi tunazolipa.isije ikawa tunalipa kodi mara mbili au zaidi katika suala moja yaani umeme!Mkuu usijiumize kichwa, usitegemee Pinda atakuambia kitu kilichokwenda shule hata siku moja....naye yule ni janga lingine la taifa kwani hajuwi akifanyacho na haelewi nini anachokisema. Kwa kifupi, pole sana.