pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 18,406
- 14,643
Kodi ni kwa ajili ya wanyonge tu? raisi, makamu wa raisi, waziri mkuu, mawaziri, wabunge na wakuu wa Mikoa na wilaya hawakatwi payee! Hii ni haki? kweli inauma sana sana jamani.:frusty:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu serikali kandamiz ndivyo zilivyo , bado wameona kodi hizo bado hazitoshi wameamua kufuta increment ya mwaka katika mishahara ambayo ipo kisheria, mfano siku hizi watu wote wa tgs D wameachwa D1 hakuna kwenda D2 hatA kwa miaka zaidi ya 5. huu ni ukandamizaji wa waziwazi
Hesabu za haraka haraka, kama ongezeko hilo la mshahara limesababisha ongezeko hilo la kodi basi mshahara wako wa mwanzo ulikuwa ama ni TZS 800,000 kamili au zaidi ya apo.
Kumbuka kiwango cha chini elekezi kutoka serikalini ni TZS 170,000.
Unapaswa kumshukuru Mungu kwa kipato hiki badala ya kuanza kulalamika, kuna watanzania mamilioni ambao hawapati hata shilingi kwa mwezi, si wafanyakazi, si wakulima, si wajasiriamali, si lolote, wako kama vile wanasindikiza wenzao (katika ulimwengu huu wa fedha na tamaa).
Nachokushauri, kwa ongezeko hili, na Mabenki outomatically yameongeza kiwango yaliyotayari kukukopesha, usiwasikilize, hao ni wabaya kuliko hata serikali.usiingie tamaa ya kufanya biashara kwa sababu unaweza kukopa pesa nyingi, wala usiwatenge wenzako uliowapita kipato na usijiunge na wale uliowafikia kipato katika matumizi.
Ongeza bidii kazini, inshalah, labda Mshahara utaongezeka tena muda si mrefu.
Naunga mkono hoja huu wizi wa serikali. Mfano anayepokea zaidi ya laki saba analipa kodi asilimia 30 ya fedha inayozidi. Hatukatai kulipa kodi lakini basi kuwe na usawa. Wafanyabiashara na viongozi wa juu serikalini pia walipe kodi. Sio wananyonywa tu wanaofanya sekta binafsi.
Consigliere, si hiyo tu, Kwa nini mimi nilipe kodi na wengine hawalipi na wao wana kipato kikubwa kuliko mimi?kwa nini wanifanyie dhihaka?
1%? Kweli?
Watoze PAYE sawa sikatai, lakini mbona sioni dhati yoyote ya kupunguza mfumuko wa bei ili niyamudu maishi? Unadhani mfumuko wa bei ungedhibiwa ningelalamika kuwa PAYE ipunguzwe?
Kwenye uchaguzi 2015 lazima mgombea urais aseme wazi kwamba atapunguza paye kutoka 14% hadi 3% mbona migodi wanachajiwa 3% tena kwenye net profit iweje sie tunalambwa kwenye gross? Hilo neno paye lifute iwe tax tu.
kama kweli wamepunguza asilimia 1 wafanyakazi kwa pamoja kuna haja ya kuitoa serikali hii madarakani kwa kuinyima kura ccmPunguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.
Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.
Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezetaamkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari.
Tafakari, chukua hatua!
-------
Mwananchi (Juni 14)
Kwani mshahara ni nini? Mbona una mwambia amshukuru Mungu? Yes anamshukuru lakini hayo ni malipo halali kwa kazi anayofanya pengine kazi anayofanya ni kubwa zaidi ya malipo sasa hapa amshukuru Mungu kwakutopewa haki yake au achukue hatua ya kumponda huyo shetani anayeiba haki yake?
Haya mambo ya kuwafanya watu kutokuwajibika kwa kichaka cha Mungu ni baya mno kwa attitude za raia.....
Kila mtu afanye kazi na akishafanya ni wajibu wa serikali toa malipo sahihi kwa kila mfanya kazi pengine niwajibu wa serikali pia kulipa hata wasiofanya kazi kama haijawapatia kazi ya kufanya. Ni wajibu wa serikali ku coordinate raia kufanya kazi kama kuna failure in coordination aka bad governance ndiyo tunaishia kudanganya watu kumshukuru Mungu kwa kunyonywa..... Ushindwe kabisa katikajinavla Yesu aliye hai!
AME twende taratibu. Unataka kuniambia katika nchi yetu, na karibia zote katika dunia ya tatu, swala la kupata fursa ya kufanya kazi sio la kumshukuru Mungu, achilia mbali mshahara wote huo??
PAYE ni kodi wanayokatwa wafanyakazi na Muajiriwa wao kutoka kwenye kipato walichokubariana katika Mkataba wa Kazi, sasa wabunge wanamkataba na nani? Bunge?Serikali? Mkataba wa kufanya nini?
Haitakiwi kuwa hivi kama kwa wengine si hivyo kwanini na ss tusiikatae hii hali ya kidunia ya tatu? Mbona korea wametoka, Singapore, Malasiya na kwingine?
Ss tunaanza lini kuondokana na haya mawazo? Swala la ajira ni la serikali ikikubali jukumu lake basi hiyo pekee ni hatua kubwa kuliko kuendelea kukusanya kodi huku wakiacha kuturatibisha kwenye kazi na malipo!
Hata kama uchumi ni ndogo katika udogo huo kila mtu apate kidogo kidogo na kila mtu apatiwe kazi yakufanya!
Ili nisiwe mlalamikaji bali mchangiaji chanya basi wizara ta TAMISEMI, wizara ya viwanda na buashara na hii ya Uwezeshaji hazija onyesha ni vipi kila raia ame wezeshwa!
Naiona dhamura ya Rais katika kutaka kuwasaidia raia lakini patronage inamfanya asifikie malengo yake. Mtu kama ni rafiki yako akashindwa kukusaidia kutimiza wajibu wako kwa raia ww ndiye mkosaji maana uwezo wa kuchagua na kuondoa umo mabegani mwako. Kama unalalamika pamoja ba walio kupa huo uwezo na mamlaja ya kitendaji basi ww ni msaliti na dhamura hiyo njema inaonekana kuwa si njema tena!
Hajachelewa, akubali kuondoa patronage na atimize wajibu wake!
akiitisha mgomo utam-support au ndo ule woga wa mtanzania unaoambatana na "fikra za hayanihusu!" Mgomo wa Barrick Gold ulitufundisha hulka ya Mtanzania kwamba ni mwoga! Pia mgomo wa madaktari Muhimbili, Mwambepande tu iliwanyamazisha! Usiwatupie lawama viongozi tu, jiulize kama upo tayari kwa mkong'oto kutokaa wenye nchi?tunasema toka kwa sababu uneshindwa kazi bajeti inesomwa leo hakuna jipya ujinga ule ule nakato ya kodi kwa mtumishi wa umma bado mzigo
wanasiasa wamegeuza mtumishi wa umma zezeta unamwambia umeongezewa mshahara pasipo kumtajia kuwango kipi
walimu wetu wameendelewa dharaulika baada waongezewe posho serikali inaongeza majengo na madawati si ujinfa huu hayo majengo na vifaaa vya kufundishia atavitumia nani ikiwa mwalimu hana moyo wakufundisha
tunasema mgaya toka kwa sababu matatizo haya unayajua na umekuwa unakaaa vikao na serikali sasa umeshindwa toka huna msaada kwa watumishi wa umma.
kupitia kwa magamba hakuna rangi tutakayoacha kuiona. tulichagua wenyewe sasa tusilalamike. tutulie tunyolewe kwa kutumia panga.je hapa ndio wametupinguzia makali ?
je hapa ndio wametupinguzia makali ?